Mpaka sasa sielewi hatma ya maisha yangu ni ipi

Mpaka sasa sielewi hatma ya maisha yangu ni ipi

Pole sana mkuu.

Dar ndo nyumbani? Umepanga? Una utayari wa kufanya biashara? Kiasi cha pesa ulichonacho kinatosha kuanzisha biashara ndogo ndogo kadhaa na kuweza kukusukuma kimaisha? Ukiona inafaa tuwasiliane PM, naweza kujitolea kukupa skills za biashara flani ikakupush. Ukiwa na hata laki tano tu unaanza vizuri
Mkuu kwanini usitoe hizo skills hadharani na sisi tupate japo kitu
 
Sina la kukushauri mkuu ila acha na Mimi niongeze yangu.
Haya mambo haya dah.... Sijui ni ulozi au ni kitu gani.
Hali unayopitia na ninayopitia nazani zinataka kufanana ila yangu ni mbaya zaidi!
Sijawahi kuajiliwa ila kiasilia Mimi ni mpambanaji sanaa. Nimefanikiwa kujenga, nimefanikiwa pia kununua shamba hapa hapa dar kwa Sasa sio shamba tena kwani limekuwa eneo la makazi na ninakiwanja kingine hapa hapa town. Na Nina kibiashara Cha tigo pesa+ ges na vitu vidogo vidogo.
Shida inaanzia hapaa...
Tangu miaka mitatu iliyopita maisha yangu yamekuwa hayaeleweki kabisa. Kila nnalofanya haliendi, pesa kwangu haiingii wala haikai.

Mbaya zaidi sasaivi hata uwezo wakutoka kwenda kupiga mishe Sina. Nimekuwa mtu wa home tu yaan sijui nielezeje nieleweke.
Nina hofu isiyomfano na sijui sababu. Najitahidi kukaza lkn daah.. sielewi kabisa.
Kiduka kimefilisika kwa kasi ya ajabu ila bado kipo kiaina kinachechemea, na nibaada yakumuachia dogo wa mshahara.
Kuna kipindi nahisi heri nife manake Sina amani wala furaha. Hakuna nnalofanya nikalikamilisha. Nimekuwa mtu wakuishia katikati.
Haya maisha haya... Ni full mahangaiko na vituko.
Mkuu pole Sana punguza uoga utafanikiwa tu
 
Siamini macho yangu kama inafika kipindi mtu unafilisika mpaka mawazo, yaani hujui nini cha kufanya ili maisha yasonge mbele lkn ukweli mtupu haya ndo ninayopitia Mtanzania mwezenu.

Historia yangu kiufupi ni hivi, Mimi ni muhitimu chuo kikuu (UDSM) kada ya ualimu wa sanaa (Art), na kama mjuavyo hii fani ina changamoto katika ajira.

Nilihitimu mwaka 2018 na baada ya nilijaribu kutuma maombi shule mbalimbali bila mafanikio, lakini Mola hamtupi mja wake nilipata kibarua kimoja hivi ambacho nashukuru Mungu kilifanikisha kunivusha sehem A kwenda B japo nilifanya kwa muda wa miaka 2.

Niliweza ku-save kiasi cha sh mil 2 hivi ndani ya huo muda na kibarua kilikoma mwezi wa kumi mwaka huu (2020).

Mpaka sasa nna mwezi wa tatu huu niko tu ndani kiufupi nimenasa katika jela ya mawazo yani kila biashara ninayoifikiria nahisi haiwezekani mpaka imepelekea naugua ulcers kwa mawazo nilonayo.

Jamani jela ya kifikra ni mbaya mno, maana nafikiria hiki kitu nilichokitafuta kwa miaka 2 kikipotea itakuaje!

Bahati mbaya sina hata wazazi wa kunipa motisha kwamba wapo nyuma yangu kwani walifariki nikiwa mdogo.

Mpaka najuta kabisa kwanini nilitumia muda mwingi kwenye kusoma halafu nakuja kufanya kazi ambazo ni out of field.

Sasa basi naombeni ushauri wenu jamani nifanye nini mana dahhh hela nilonayo ndiyo inazidi kupukuchuka, maisha ya Dar kila siku ni hela yani nahisi kukata tamaa.
Yaan we jamaa unajihurumia mno. Kuna wenzio jawana hata hela ndani, hawajasoma, wanafanya vibarua wale kesho yao hawaijui na wala hawasononeki kama wewe maisha yanasonga tu. Sasa wewe mwanzo unao bado unapata ulcers, za nini sasa? Kuna watu wameanza biasgara za sh 20000 na maiaha yanaenda. Elimu yako ya chuo iliishia kwenye daftari???
Inatakiwa ufikiri nje ya box kama msomi tengeneza ideas za hela. Sio unajihurumia mwanaume, we vp bana.
 
Back
Top Bottom