Ukijenga nyumba baada ya muda inazeeka na muonekano wake unakuwa si mzuri sana. Kinachofuata either ni kubomoa na kujenga upya au kufanya ukarabati au kuendelea kuacha hivyo ilivyo na haitakuwa na dhamani sana. Kuna mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyakwepa lazima akubali mabadiliko yanayotokana na nyakati kubadilika. Utazuia lakini haitakuwa rahisi maana ni kama kuzuia maji wakati huko milimani mvua zinaendelea kunyesha.
Usemayo ni kweli, kwa huo mfano wako wa nyumba ulioutumia kueleza hoja yako.
Lakini pia kumbuka kwamba kuna wamiliki wa nyumba wa aina nyingi. Kuna wale wanaotengeneza na kukarabati nyumba mara kwa mara, ili idumu na iendelee kupendeza; na kuna waele wengine ambao wakishamaliza ujenzi, hawana tena habari ya kuihudumia nyumba iendelee kuwa bora.
Hili kundi la pili, ndilo lililo kiangukia CCM, kwa nyakati mbalimbali katika uhai wake na viongozi wake tofauti tofauti.
Ukiamnza na Mwinyi, utaona kwamba hakuwa na umakini sana wa kuitengeneza CCM iendelee kuwa chama imara, zaidi ya kuitumia tu kuwa chama cha manufaa kwa viongozi, kinacho wahakikishia kuendelea kubaki madarakani.
Mkapa kidogo alikuwa tofauti. Aliweka mkazo mkubwa katika ukarabati wa chama, pamoja na kwamba mwelekeo wa chama ulisha badilika.
Kikwete, hakuwa tofauti sana na Mwinyi, lakini yeye alitambua zaidi kukitumia chama kama ngao kwa viongozi na kuendelea kuhakikisha kuna mbinu mpya za kubaki madarakani (hizo mbinu ni pamoja na za haramu) zinazotumika sasa.
Magufuli yeye, CCM aliiona ni dubwasha tu la kubeba maguvu yake. Alitumia chama kufanya kila aina ya ubabe na uovu.
Samia! OOOoooh! huyu ndiye kaja kukimaliza kabisa chama. Kama ni nyumba, huyu kazidisha nyufa kwenye nyumba nzee nzee na kutaka kuimaliza moja kwa moja
Nilikuwa na hofu kubwa, kwamba CCM kama chama chenye nguvu, kingeishia katika mikono ya Kikwete. Lakini kwa bahati sijui iliyoje, kikabaki hadi kumfikia Samia.
Sasa kilicho baki ili hii nyumba iporomoke moja kwa moja chini ya mikono ya huyu mama; ni kwa waTanzania kuiweka pembeni ya madaraka na kushika dola.
Iwapo itatokea hivyo (nafasi pekee ya kupona ni kuua waTanzania wengi wa kutosha ili Samia aendelee miaka mitano)
Mbali ya hapo, CCM itaanza kusambaratika, kama isipopata viongozi mahiri wa kuiokoa.
Hiyo ndiyo "nyumba" aliyomo sasa hivi Samia Suluhu Hassan. Mwenye nyumba asiyejaali kabisa matunzo ya nyumba anamoishi mwenyewe.