Uchaguzi 2020 Mpaka sasa Halima Mdee ameshashinda Jimbo la Kawe, Dar-es-Salaam



Baada ya CCM kumpitisha Gwajima , nina uhakika Mdee atashinda uchaguzi katika Jimbo hilo tena kwa kura nyingi zaidi safari hii kuliko ilivyokuwa mwaka 2015 unless haki isitendeke.

Ukiacha watu kuichoka CCM, Gwajima bado ataponzwa na kauli zake zilizoko mitandaoni na uzuri hapa Dar wenye smartphone ni wengi, hivyo itakuwa rahisi watu ku-share clips zake.

Sababu nyingine itayochangia ashindwe ni kutokuwa chaguo la wana-CCM bali amekuwa chaguo la viongozi wa CCM kwani hakushinda katika kura za maoni, hivyo ni wazi wako baadhi ya wana-CCM ambao hawatampigia kura..

Kingine,waumini wa Gwajima ni sehemu ndogo sana ya wakazi na wapiga kura wa Jimbo la Kawe, hivyo advantage ya yeye kuwa kiongozi wa dini ni ndogo sana kumbeba bila kusahau ukweli kuwa watanzania hawana sana utamaduni wa kuchagua mtu kwasababu tu ni kiongozi wa kidini.

Kuanzia leo nakuendelee tutarajie kuona clip za Gwajima zikiibuka upya na kwa kasi mitandaoni.

Halima huko aliko bila shaka atakuwa anachekelea kupata mpinzani ambae teyari ameshajiharibia kwa kauli zake mwenyewe.

Muda utaongea.
 
Gwaji aanze kushona suti tu mapema aachane na hivyo vizibao bungeni.

Kama kampeni yenyewe mnategemea clips zake akitia,kibongobongo hiyo siyo habari labda ingekuwa kainamishwa.
 
Kwanza waumini wa Gwajima sio wakazi wa Kawe Kwa ivyo kujaza kanisa lake aina maana kujaza wapiga kura.

Wajumbe wa Kawe CCM wanaweza kuwa watu wa ovyo lakini si wapiga kura wa Kawe.

Gwajima sio tu atashindwa Kawe mchana kweupe ata kumtumia kwenye campaign Dar za CCM ni kuichefua jamii ya waisalamu na kitendo kitakacho wapotezea baadhi ya wapiga kura.

Ata mimi ningekuwa naishi Kawe ningeenda kulinda kura za Mdee.

I can’t lie hate this Gwajima guy with all my zest.
 
Kwanza waumini wa Gwajima sio wakazi wa Kawe Kwa ivyo kujaza kanisa lake aina maana kujaza wapiga kura.

Wajumbe wa Kawe CCM wanaweza kuwa watu wa ovyo lakini si wapiga kura wa Kawe.

Gwajima sio tu atashindwa Kawe mchana kweupe ata kumtumia kwenye campaign Dar za CCM ni kuichefua jamii ya waisalamu na kitendo kitakacho wapotezea baadhi ya wapiga kura.

Ata mimi ningekuwa naishi Kawe ningeenda kulinda kura za Mdee.

I can’t lie hate this Gwajima guy with all my zest.
Jiandae tuu maana usiempenda kaja
 
Salary Slip,

Umesahau kwamba Halima Mdee alikuwa ni mmoja wa viongozi wa kutohudhuria bungeni.

Hivyo Gwajima anairemba hii hoja huko aliko na kuitia nakshi na akija kuitoa inakuwa Gwajima 1 Mdee 0

Alivyo mjuzi wa kujieleza ataifafanua kwa kila kona na kisha kuuliza umati kama unaungana nae.

Umati ukijibu basi Kawe itatikisika.

Hivyo hiyo ni hoja namba 1.

Pili na kuendelea tumsubiri Gwajima mwenyewe atakapoanza kampeni uwanjani Tanganyika Packers.
 
Jimbo la Kawe limejaa wanaojielewa na wanaojielewa wengi wanapenda haki kwahiyo wataihagua Chadema watamchagua Mdee, Mikocheni,Mbezi Beach, Ununio,Mbweni JKT, Bunju Beach, watu wenye uwezo hawawezi kumchagua Mcheza PONO.
 
Gwajima ana kashfa yenye ushahidi na makandokando mengi, Mdee ana kashfa za kusemwa tu zisizo hata na chembe ya ushahidi.

Gwajima angeweza kushinda jimbo la Mbagala au Ubungo huko, sio jimbo la Kawe ambalo lina wasomi wengi na watu wengi wenye uwezo wa kifedha!!!!
Oktoba siyo mbali
 
Back
Top Bottom