Uchaguzi 2020 Mpaka sasa Halima Mdee ameshashinda Jimbo la Kawe, Dar-es-Salaam

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Baada ya CCM kumpitisha Gwajima , nina uhakika Mdee atashinda uchaguzi katika Jimbo hilo tena kwa kura nyingi zaidi safari hii kuliko ilivyokuwa mwaka 2015 unless haki isitendeke.

Ukiacha watu kuichoka CCM, Gwajima bado ataponzwa na kauli zake ambazo pia zinapatikana mitandaoni, na uzuri hapa Dar wenye smartphone ni wengi, hivyo itakuwa rahisi watu ku-share clips zake na kufanya aliyoyasema, hasa yale yenye element za udini, kuwafikia watu wengi zaidi na hivyo kumgharimu.

Sababu nyingine itayochangia ashindwe ni kutokuwa chaguo la wana-CCM bali amekuwa chaguo la viongozi wa CCM kwani hakushinda katika kura za maoni, hivyo ni wazi wako baadhi ya wana-CCM ambao hawatampigia kura.

Kingine: Waumini wa Gwajima ni sehemu ndogo sana ya wakazi na wapiga kura wa Jimbo la Kawe, hivyo advantage ya yeye kuwa kiongozi wa dini ni ndogo sana kumbeba bila kusahau ukweli kuwa watanzania hawana sana utamaduni wa kuchagua mtu kwasababu tu ni kiongozi wa kidini.

Kuanzia leo na kuendelee, tutarajie kuona clip za Gwajima zikiibuka upya na kwa kasi mitandaoni.

Halima huko aliko bila shaka atakuwa anachekelea kupata mpinzani ambae teyari ameshajiharibia kwa kauli zake mwenyewe.

CCM inaangamia kwa watu wake kusosa maarifa yakiwemo hata maarifa madogo tu ya kusoma alama za nyakati!

Muda utaongea.
 
Subirini mziki wa gwajima..mmeshau hadi maalim seif alikuwa anahudhuria kwa gwajima?
images%20(32).jpg
 
Mdee ana kazi tena kazi nzito sana, huko alipo anatafakari mpaka kichwa kinapata moto yani kuna mtu anaweza akawa hajui kitu ila mdomo anaweza kuutumia ipasavyo. Gwajima n sawa na Msukuma part 2. Upinzani mbona kazi wanayo awamuu ijayo,huko bungeni wajipange.
 
Samahani Mdee,Gwajiboy humwezi
Sio kwa jimbo la Kawe la wasomi na watu wenye uwezo wa kifedha kwa wingi!

Gwajima ana makandokando mengi sana, hawezi kupita jimbo la Kawe, labda ingekuwa jimbo lingine!

Watu wa Kawe ninaowajua mie sio wa kwenda kumchagua mtu anayejirekodi akifanya mapenzi na mwanamke. Hapana!!! Sio Kawe hii. Bora wangempitisha yule Mkurugenzi wa Mwananchi, Francis Nanai
 
Back
Top Bottom