KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,590
- 4,603
Mpaka sasa najaribu kutafuta makosa ya Hayati JPM nikiri kusema sijaona makosa yoyote labda pengine macho yangu yameamua kuangalia yanayopendezwa nayo au kwa sababu nyingine yoyote ila sijaona.
Nakumbuka Hayati aliwahi kusema alikuwa anafuatwa na makandarasi na kumuahidi mabilioni ya shilingi ili kupata upendeleo kwenye tenda za ujenzi lakini aligoma kufanya hivyo kwa mapenzi aliyokuwa nayo kwa nchi hii.
Kama angeamua kuchukua kutoka kwao bilioni 1 kwa kila mkandarasi ukizidisha kwa jumla ya wakandarasi labda wapo 4000 au 5000, Hayati angekuwa na utajiri wa shilingi trilion 4 au 5 za kitanzania ni kusema kwamba angekuwa tajiri namba moja Tanzania lakini hakuwa na utajiri huo wala wa hata robo wala hata 0.2% ya huo utajiri.
Hii yote ni kuonesha mapenzi makubwa aliyokuwa nayo Hayati JPM ,shujaa anayeliliwa kila leo na kila mtu. Hakuwa na makosa yoyote Bali aliacha alama ya kudumu.
Neno la Mungu kupitia Biblia linasema ni furaha gani mtu aliyonayo anapojitoa maisha yake kwa ajili ya wengine. Si furaha ndogo ni kubwa sana na JPM alipo anaiona ,anahihisi furaha hiyo kuu kama ambavyo nasi tunavyoiona.
Narudia Tena kosa pekee alilonalo Hayati Magufuli ni kulipenda Taifa hili kwa uhai wake , upendo wa juu kabisa wa mwanadamu kwa wengine. Mnaoona makosa kwake nionesheni, maana mimi sijayaona?