Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 15,320
- 24,189
Mpaka hii leo nafikiria, tena critically, ilifanyika vipi hadi John Pombe Mgufuli akafikia hatua ya kuwa Rais wa Tanzania?
Sijamfahamu Magufuli akiwa Rais, nilikuwa namfahamu toka akiwa Naibu Waziri pale Wizara ya Ujenzi. Kuingia ofisini tu siku alipoteuliwa na Rais mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ujenzi, kuna mhandisi walisoma wote chuoni akamtania kuwa anafanya nini pale wizara ya mainjinia, Magufuli akamwambia hamjui yeye nani, na akaagiza atimuliwe, akatimuliwa.
Na huko alikopata ubunge, tunaambiwa kuna watu wamepotea au wamepotezwa.
Pale Wizara ya ujenzi, uwekaji mipaka ya barabara zimeliwa fedha nyingi sana nchi nzima. Uuzaji wa nyumba za serikali ndio usiseme, wakubwa wote walifaidika. Serikali ilikuw wapi?
Mimi nashindwa kuelewa kuwa kama vyombo vilikuwa vinamjua Magufuli ni kwa nini Mkapa na hata Kikwete walifumbia macho mapungufu yake?
Sitagusa mapungufu ya Magufuli akiwa madarakani, maana hata hawa viongozi wa leo serikalini walionja joto la jiwe.
Imefika wakati lazima tupate post mortem ya kisiasa ya kwa nini hii blunder ilifika kupata Rais ambaye hata uraia wake ulikuwa na maswali? la sivyo Magufuli no. 2 yupo round the corner.