Moyo wangu una majonzi, yako wapi mapenzi ya dhati?

Hayo ndio malipo yakumuonyesha mwaamke kua unampenda sana. Jiamini, huyo wako hakupendi anatamani umuache, sasa cha msingi acha kupepelea sana fanya kawaida, akiwepo poa akikuacha poa. Ujue hakupendi na hajawahi kukupemda.
Au mzoee na hali yake na usilalamike. Wala usimlalamikie Mungu.
Endelea kuomba acha lawama.
 
Sawa mkuu, nitafanyia kazi ushauri wako
 
Ndu zangu wana jamvi....

Naomba nieleweke hivi, nimechoka, sijui tatizo langu ni kwamba napenda sana bila kiasi, nimepitia kwenye mahusiano kama matatu sasa toka nijue mapenzi ni nini, mwanamke wa kwanza aliniumiza sanaa, nililia mwanaume machozi ya kila aina, sikuwa tayari aniache, nilikuwa naona kam maisha yangu yatakuwa magumu sana nikiachana na huyo dada.
Niliteseka kwa zaidi ya mwaka mmoja nambembeleza turudiane, alinitesa mno, siwezi kuelezea. Siku moja nilijifungia chumbani kwangu saa 11 jioni hadi kesho yake, nilifunga simu, nikapiga magoti, nilisali sana, nilimlilia Mungu moyo wangu upate amani, nikamshi Mungu kama sio mapenzi yake amuweke mbali na mimi yule binti, kweli siku ya pili nilikuwa mwepesiii, sikuwa hata na hamu ya kumtafuta, nilimshukuru sana Mungu maisha yangu yanaanza kubadilika mwishowe nikafuta mpaka namba zake japo hata leo ninazo kichwani....

Nikaanza mahusiano mengine, nikaona picha ni zile zile, nilikimbia mapema nilivoona tabia za mwanamke wangu wa kwanza zimeanza kujirudia kwa mwanamke huyo wa pili....nikamuomba Mungu nisiingie tena kwenye mahusiano kama vinginevyo iwe ni mwanamke wangu alieniandalia, nilikaa kwa karibu mwaka mmoja na nusu bila kuwa na mahusiano ya serious......

Mwaka huu mwezi wa Tano nilikutana na Binti mmoja mrembo kweli, ni mzuri kuanzia kutembea kwake, kuongea kwake, anapenda sana kanisa, kila Jumapili yuko kanisani ibada ya kwanza. Binti huyu kwa mara ya kwanza alikuja kwenye eneo langu la kazi, alikuja kumtembelea rafiki yake ambae pia staff mwenzangu, nilivyomuona kiukweli nilimpenda, nikajaribu kumuuliza yule rafiki yake, akanipa briefing kidgo kuhusu huyo binti, nilimuomba appointment ya kutoka nao wote wawili ili atleast nipate picha halisi na kujuana nae kidogo. Kwenye hiyo out tulibadilishana mawazo kidogo, tukabadilishana na mawasiliano pia, nikaanza kujenga nae urafiki, tukafahamiana vizuri then nikaona ni mtu ambae yuko smart kweli, siku moja nikamuomba appointment ya kutoka nae somewhere for lunch, hakukataa alikuja then tukaongea sana then nikamruhusu aende nyumbani mapema ili awahi mapishi ya jioni. Yote tisa, kumi huyo binti nilianza nae mahusiano baada ya kila mmoja kumfaham mwenzake,,,,ni takriban miezi 5 sasa toka tumeanza mahusiano rasmi, professionaly yeye ni mwalimu, mimi ni Muhasibu, tumekuwa tukiwasiliana vizuri sana, kinachonipa wakati mgumu kwake ni majibu yake, mara nyingi nikichat nae huwa ana majibu mkato sana (shortcuts), unaweza ukawa unamuuliza kitu sensitive yeye akakujibu majibu ambayo like she dont care. Kingine huyu binti amekuwa mgumu sana kushare nae muda, kama mpenzi wangu muda mwingine naweza muomba lunch tule sehem moja lakini akakataa bila sababu, nikimuliza sababu nini atakujibu niko busy ... hii statement ya niko busy imekuwa ikini disappoint sana, ukimuuliza busy na nini atakujibu sorry niko busy. Guys nisaidieni mtu kama huyu kweli bado anaweza kuwa na mapenzi ya dhati kwako? Katika chatting yake mara nyingi tumevutana sana, huwa ni mtu mwenye majibu ambayo yanaonyesha hajali kabisaa,,,

Tukiachana na hayo yote , wiki iliyopita wakati napiga nae story kwenye simu alichomekea agenda yake kuwa anataka kurudi chuo kwa miaka 3 kuanzia mwaka ujao kwa hiyo nikimhitaji maswala ya ndoa nisubiri mwaka 2020. Hili jambo limenikatisha sana tamaa guys, yaani nikae mtaani nimsubiri yeye anaenda chuo kwa miaka minne kuanzia sasa....moyo wangu uliumia sana kiukweli, bado naendelea kuumia, muda mwingine nawaza na kumwambia Mungu kwanini unanipitisha kwenye majaribu magumu kiasi hiki? Kweli ni binti niliempenda sana ila yeye kutokuwa na care inanikatisha tamaa, majibu yake mara nyingi ni " Poa, sawa, K, P n.k.
Guys wenye experience naombeni ushari, naumia kweli maana tayari nilishaingia kwake miguu yote, dalili ya kuumia tena naiona.

Sio dhihaka , sio utani napitia kwenye wakati mgumu, ambao tayari mko kwenye ndoa naomba mtusaidie mlipitia katika wakati kama huu?
Muda mwingine huwa namwambia Mungu mapenzi ya kweli yale ya wazazi wetu yako wapi? Kiukweli vijana wa kiume tunapitia wakati mgumu sana pindi unapomtafuta binti wa kuwa nae kimaisha.

Naamin sipo mwenyewe, tusaidiane kwa ushauri na kufarijiana.
Pole mkuu,nakushauri unapoanzisha mahusiano usilenge ndoa kamwe,wala usionyeahe kujali kupita kiasi,ukisha kula Mara ya kwanza mkaushie hadi yy akutafute,kamwe usijionyeshe unajali sana Ila ingia nusu nusu,usimtext kuwa unampenda sana cjui ma vitu gani gani km umeshatafuna,Ila subir yy akikuambia I love u bby bac nawe jibu I'll you too hny,...usijiweke kimbelembele cha kuonyesha unajali au unapenda sana,....watakuumiza wtt Wa cku hiz Hawa mjomba.km unampenda kweli bac mpende kisiri siri yy asijue how much u love her.baadae utaona reaction yake kwako na hapo ndo utachagua kuweka ndani au kupotezea....Ila kumbuka wakati unaendelea kuchagua make sure unatumia condom ucje ukala chuya mangi,....ikibidi tumia kauli ya TID alomwambia Prezoo atumie DUME,tena akaongeza atumie condom ya bei ghali ili walau awe na amani kua haitapasuka.....
 
Mtumishi wa Mungu kama utapata nafasi njoo mpaka PM umalizie kunipa ushauri unaosimama kwa miguu yake. Maneno haya yamenifanya moyo wangu upoe kwa muda, hakika nimefarijika mno kuona hata huku kuna watu kama wewe mnaoweza kugusa maisha ya mtu direct. Ubarikiwe mno
ISAYA 34:16 NENO LINASEMA HAKUNA ATAKAYEMKOSA MWENZAKE YAANI KM UMEONA DALILI HIZO TAMBUA FIKA KUNA MTU ANAYETEGEMEWA NA C WW JITAHIDI RUDI MAGOTINI MWA MUNGU KWA UPYA MAANA LILILO KUSUDI LA MUNGU BABA HALITAKUSABABISHA UJE UJUTE BALI KUSUDI LA MUNGU BABA LITAKUFANYA WEWE NA NYUMBA YAKO MUMFURAHIE MUNGU BABA MILELE
 
Pole mkuu,nakushauri unapoanzisha mahusiano usilenge ndoa kamwe,wala usionyeahe kujali kupita kiasi,ukisha kula Mara ya kwanza mkaushie hadi yy akutafute,kamwe usijionyeshe unajali sana Ila ingia nusu nusu,usimtext kuwa unampenda sana cjui ma vitu gani gani km umeshatafuna,Ila subir yy akikuambia I love u bby bac nawe jibu I'll you too hny,...usijiweke kimbelembele cha kuonyesha unajali au unapenda sana,....watakuumiza wtt Wa cku hiz Hawa mjomba.km unampenda kweli bac mpende kisiri siri yy asijue how much u love her.baadae utaona reaction yake kwako na hapo ndo utachagua kuweka ndani au kupotezea....Ila kumbuka wakati unaendelea kuchagua make sure unatumia condom ucje ukala chuya mangi,....ikibidi tumia kauli ya TID alomwambia Prezoo atumie DUME,tena akaongeza atumie condom ya bei ghali ili walau awe na amani kua haitapasuka.....
Niseme tu ahsante mkuu
 
ISAYA 34:16 NENO LINASEMA HAKUNA ATAKAYEMKOSA MWENZAKE YAANI KM UMEONA DALILI HIZO TAMBUA FIKA KUNA MTU ANAYETEGEMEWA NA C WW JITAHIDI RUDI MAGOTINI MWA MUNGU KWA UPYA MAANA LILILO KUSUDI LA MUNGU BABA HALITAKUSABABISHA UJE UJUTE BALI KUSUDI LA MUNGU BABA LITAKUFANYA WEWE NA NYUMBA YAKO MUMFURAHIE MUNGU BABA MILELE
Amen. Hakika Nitamtegemea Mungu mpaka anipatie aliyenipangia yeye
 
Ndu zangu wana jamvi....

Naomba nieleweke hivi, nimechoka, sijui tatizo langu ni kwamba napenda sana bila kiasi, nimepitia kwenye mahusiano kama matatu sasa toka nijue mapenzi ni nini, mwanamke wa kwanza aliniumiza sanaa, nililia mwanaume machozi ya kila aina, sikuwa tayari aniache, nilikuwa naona kam maisha yangu yatakuwa magumu sana nikiachana na huyo dada.
Niliteseka kwa zaidi ya mwaka mmoja nambembeleza turudiane, alinitesa mno, siwezi kuelezea. Siku moja nilijifungia chumbani kwangu saa 11 jioni hadi kesho yake, nilifunga simu, nikapiga magoti, nilisali sana, nilimlilia Mungu moyo wangu upate amani, nikamshi Mungu kama sio mapenzi yake amuweke mbali na mimi yule binti, kweli siku ya pili nilikuwa mwepesiii, sikuwa hata na hamu ya kumtafuta, nilimshukuru sana Mungu maisha yangu yanaanza kubadilika mwishowe nikafuta mpaka namba zake japo hata leo ninazo kichwani....

Nikaanza mahusiano mengine, nikaona picha ni zile zile, nilikimbia mapema nilivoona tabia za mwanamke wangu wa kwanza zimeanza kujirudia kwa mwanamke huyo wa pili....nikamuomba Mungu nisiingie tena kwenye mahusiano kama vinginevyo iwe ni mwanamke wangu alieniandalia, nilikaa kwa karibu mwaka mmoja na nusu bila kuwa na mahusiano ya serious......

Mwaka huu mwezi wa Tano nilikutana na Binti mmoja mrembo kweli, ni mzuri kuanzia kutembea kwake, kuongea kwake, anapenda sana kanisa, kila Jumapili yuko kanisani ibada ya kwanza. Binti huyu kwa mara ya kwanza alikuja kwenye eneo langu la kazi, alikuja kumtembelea rafiki yake ambae pia staff mwenzangu, nilivyomuona kiukweli nilimpenda, nikajaribu kumuuliza yule rafiki yake, akanipa briefing kidgo kuhusu huyo binti, nilimuomba appointment ya kutoka nao wote wawili ili atleast nipate picha halisi na kujuana nae kidogo. Kwenye hiyo out tulibadilishana mawazo kidogo, tukabadilishana na mawasiliano pia, nikaanza kujenga nae urafiki, tukafahamiana vizuri then nikaona ni mtu ambae yuko smart kweli, siku moja nikamuomba appointment ya kutoka nae somewhere for lunch, hakukataa alikuja then tukaongea sana then nikamruhusu aende nyumbani mapema ili awahi mapishi ya jioni. Yote tisa, kumi huyo binti nilianza nae mahusiano baada ya kila mmoja kumfaham mwenzake,,,,ni takriban miezi 5 sasa toka tumeanza mahusiano rasmi, professionaly yeye ni mwalimu, mimi ni Muhasibu, tumekuwa tukiwasiliana vizuri sana, kinachonipa wakati mgumu kwake ni majibu yake, mara nyingi nikichat nae huwa ana majibu mkato sana (shortcuts), unaweza ukawa unamuuliza kitu sensitive yeye akakujibu majibu ambayo like she dont care. Kingine huyu binti amekuwa mgumu sana kushare nae muda, kama mpenzi wangu muda mwingine naweza muomba lunch tule sehem moja lakini akakataa bila sababu, nikimuliza sababu nini atakujibu niko busy ... hii statement ya niko busy imekuwa ikini disappoint sana, ukimuuliza busy na nini atakujibu sorry niko busy. Guys nisaidieni mtu kama huyu kweli bado anaweza kuwa na mapenzi ya dhati kwako? Katika chatting yake mara nyingi tumevutana sana, huwa ni mtu mwenye majibu ambayo yanaonyesha hajali kabisaa,,,

Tukiachana na hayo yote , wiki iliyopita wakati napiga nae story kwenye simu alichomekea agenda yake kuwa anataka kurudi chuo kwa miaka 3 kuanzia mwaka ujao kwa hiyo nikimhitaji maswala ya ndoa nisubiri mwaka 2020. Hili jambo limenikatisha sana tamaa guys, yaani nikae mtaani nimsubiri yeye anaenda chuo kwa miaka minne kuanzia sasa....moyo wangu uliumia sana kiukweli, bado naendelea kuumia, muda mwingine nawaza na kumwambia Mungu kwanini unanipitisha kwenye majaribu magumu kiasi hiki? Kweli ni binti niliempenda sana ila yeye kutokuwa na care inanikatisha tamaa, majibu yake mara nyingi ni " Poa, sawa, K, P n.k.
Guys wenye experience naombeni ushari, naumia kweli maana tayari nilishaingia kwake miguu yote, dalili ya kuumia tena naiona.

Sio dhihaka , sio utani napitia kwenye wakati mgumu, ambao tayari mko kwenye ndoa naomba mtusaidie mlipitia katika wakati kama huu?
Muda mwingine huwa namwambia Mungu mapenzi ya kweli yale ya wazazi wetu yako wapi? Kiukweli vijana wa kiume tunapitia wakati mgumu sana pindi unapomtafuta binti wa kuwa nae kimaisha.

Naamin sipo mwenyewe, tusaidiane kwa ushauri na kufarijiana.
Em fanya kumsahau huyo dem alaf mteme na fanya kuyasahau mapenzi ji keep busy na shughul zako ipo cku.
 
Do one thing. Kama amekuona Wa nini na wewe kwa moyo Wa kujikaza ndani ya maumivu piga moyo konde na mwone Wa kazi gani na b happy na wadada wengine kwa story, sure utasahau na atakukumbuka tu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom