Moyo wangu una majonzi, yako wapi mapenzi ya dhati?

Moyo wangu una majonzi, yako wapi mapenzi ya dhati?

Hahahhaahahahaahaa kuna namna ya kumpenda mwanamke ndugu kama hiyo huijui basi utapenda ambavyo upaswi kumpenda na mwishowe utaumizwa...umesema yupo busy busy nadhani ungekuwa wewe busy busy angalau ingekusaidia kdg..
Hahahaa nimejikuta nimecheka jinsi ulivyosema hiyo busy busy
 
Usiruhusu maishani mtu yeyote akakujua kwa 100% haijalishi huyo mtu ni nani kwako! Ukifanikiwa ktk hili utaishi maisha ya raha mustarehe sana boss
 
Pia usionyeshe mapenzi ya dhati kwa 100% mwanzoni mwa mahusiano, hii pia ni weaknesses na mwanamke akishajua atakuendesha sana. Ndio maana gari, treni, wakati zinaanza safari huanza na speed ndogo baada ya muda huchanganya mpaka kufikia maximum speed. So take love slowly
 
Kimbia mkuu,panapofuka moshi...lazima kuna moto,hizo dalili ndo huwa zao,as long as hamjafika mbali kaa umweleze ukweli kunja virago ondoka
 
Usiruhusu maishani mtu yeyote akakujua kwa 100% haijalishi huyo mtu ni nani kwako! Ukifanikiwa ktk hili utaishi maisha ya raha mustarehe sana boss
Sawa boss. Ushauri mzuri, nimeanza kufanyia kazi ushauri wa kila mmoja toka jana usiku. Ubarikiwe mkuu
 
Pia usionyeshe mapenzi ya dhati kwa 100% mwanzoni mwa mahusiano, hii pia ni weaknesses na mwanamke akishajua atakuendesha sana. Ndio maana gari, treni, wakati zinaanza safari huanza na speed ndogo baada ya muda huchanganya mpaka kufikia maximum speed. So take love slowly
Hahaha ahsante mkuu
 
Pole sana...
Hakuna mtu asiye na muda...
Ukiona mtu unamuhitaji na anasema yupo busy, ujue kuna sehemu mtu mwingine katengewa huo muda ambao wewe unaambiwa hana...

Follow your but but carry your brain...


Cc: mahondaw
 
Anarekebishika huyo mbona...kaa uongee nae...kuna wengine ni vichwa nazi hawaelewi kitu
Sasa huo muda wakukaa na kuongea nae anaupata wapi ili amrekebishe?

Na anaanzaje kumrekebisha mtu kama huyo mwenye kutokujali waziwazi?

Unajua wakati mwingine tunajilazimishia jela ya mapenzi wenyewe!

Mtoa mada wewe ndo unajua zaidi uwezo wa kuendelea kuvumilia unao? Coz kwa dalili hizo ni wazi atakusumbua zaidi huko mbeleni

Uzuri wake wa sura, apiarence yake ya kuvutia na ongea yake ya mashamsham vyote hivo sidhani kama vitakua na faida kwako ilihali mapenzi yake kwako hakuna... .

Jipime kama waweza endelea ama lah!
 
Ndu zangu wana jamvi....

Naomba nieleweke hivi, nimechoka, sijui tatizo langu ni kwamba napenda sana bila kiasi, nimepitia kwenye mahusiano kama matatu sasa toka nijue mapenzi ni nini, mwanamke wa kwanza aliniumiza sanaa, nililia mwanaume machozi ya kila aina, sikuwa tayari aniache, nilikuwa naona kam maisha yangu yatakuwa magumu sana nikiachana na huyo dada.
Niliteseka kwa zaidi ya mwaka mmoja nambembeleza turudiane, alinitesa mno, siwezi kuelezea. Siku moja nilijifungia chumbani kwangu saa 11 jioni hadi kesho yake, nilifunga simu, nikapiga magoti, nilisali sana, nilimlilia Mungu moyo wangu upate amani, nikamshi Mungu kama sio mapenzi yake amuweke mbali na mimi yule binti, kweli siku ya pili nilikuwa mwepesiii, sikuwa hata na hamu ya kumtafuta, nilimshukuru sana Mungu maisha yangu yanaanza kubadilika mwishowe nikafuta mpaka namba zake japo hata leo ninazo kichwani....

Nikaanza mahusiano mengine, nikaona picha ni zile zile, nilikimbia mapema nilivoona tabia za mwanamke wangu wa kwanza zimeanza kujirudia kwa mwanamke huyo wa pili....nikamuomba Mungu nisiingie tena kwenye mahusiano kama vinginevyo iwe ni mwanamke wangu alieniandalia, nilikaa kwa karibu mwaka mmoja na nusu bila kuwa na mahusiano ya serious......

Mwaka huu mwezi wa Tano nilikutana na Binti mmoja mrembo kweli, ni mzuri kuanzia kutembea kwake, kuongea kwake, anapenda sana kanisa, kila Jumapili yuko kanisani ibada ya kwanza. Binti huyu kwa mara ya kwanza alikuja kwenye eneo langu la kazi, alikuja kumtembelea rafiki yake ambae pia staff mwenzangu, nilivyomuona kiukweli nilimpenda, nikajaribu kumuuliza yule rafiki yake, akanipa briefing kidgo kuhusu huyo binti, nilimuomba appointment ya kutoka nao wote wawili ili atleast nipate picha halisi na kujuana nae kidogo. Kwenye hiyo out tulibadilishana mawazo kidogo, tukabadilishana na mawasiliano pia, nikaanza kujenga nae urafiki, tukafahamiana vizuri then nikaona ni mtu ambae yuko smart kweli, siku moja nikamuomba appointment ya kutoka nae somewhere for lunch, hakukataa alikuja then tukaongea sana then nikamruhusu aende nyumbani mapema ili awahi mapishi ya jioni. Yote tisa, kumi huyo binti nilianza nae mahusiano baada ya kila mmoja kumfaham mwenzake,,,,ni takriban miezi 5 sasa toka tumeanza mahusiano rasmi, professionaly yeye ni mwalimu, mimi ni Muhasibu, tumekuwa tukiwasiliana vizuri sana, kinachonipa wakati mgumu kwake ni majibu yake, mara nyingi nikichat nae huwa ana majibu mkato sana (shortcuts), unaweza ukawa unamuuliza kitu sensitive yeye akakujibu majibu ambayo like she dont care. Kingine huyu binti amekuwa mgumu sana kushare nae muda, kama mpenzi wangu muda mwingine naweza muomba lunch tule sehem moja lakini akakataa bila sababu, nikimuliza sababu nini atakujibu niko busy ... hii statement ya niko busy imekuwa ikini disappoint sana, ukimuuliza busy na nini atakujibu sorry niko busy. Guys nisaidieni mtu kama huyu kweli bado anaweza kuwa na mapenzi ya dhati kwako? Katika chatting yake mara nyingi tumevutana sana, huwa ni mtu mwenye majibu ambayo yanaonyesha hajali kabisaa,,,

Tukiachana na hayo yote , wiki iliyopita wakati napiga nae story kwenye simu alichomekea agenda yake kuwa anataka kurudi chuo kwa miaka 3 kuanzia mwaka ujao kwa hiyo nikimhitaji maswala ya ndoa nisubiri mwaka 2020. Hili jambo limenikatisha sana tamaa guys, yaani nikae mtaani nimsubiri yeye anaenda chuo kwa miaka minne kuanzia sasa....moyo wangu uliumia sana kiukweli, bado naendelea kuumia, muda mwingine nawaza na kumwambia Mungu kwanini unanipitisha kwenye majaribu magumu kiasi hiki? Kweli ni binti niliempenda sana ila yeye kutokuwa na care inanikatisha tamaa, majibu yake mara nyingi ni " Poa, sawa, K, P n.k.
Guys wenye experience naombeni ushari, naumia kweli maana tayari nilishaingia kwake miguu yote, dalili ya kuumia tena naiona.

Sio dhihaka , sio utani napitia kwenye wakati mgumu, ambao tayari mko kwenye ndoa naomba mtusaidie mlipitia katika wakati kama huu?
Muda mwingine huwa namwambia Mungu mapenzi ya kweli yale ya wazazi wetu yako wapi? Kiukweli vijana wa kiume tunapitia wakati mgumu sana pindi unapomtafuta binti wa kuwa nae kimaisha.

Naamin sipo mwenyewe, tusaidiane kwa ushauri na kufarijiana.
Hapo kwenye watoto wakiume tuna pitia wakato mgumu sana kwenye mahusiano ckubaliani naww kabisa mkii.

Ila huyo dem ni kwamba anamtu ampendae so ameona ngum kukwambia ila kama kweli unailuzoefu wakitosha kwenye mambo haya bac jiongeze.

Halafu jengine ni kwamba wanaume huwa hatupendi kama unavyopenda wewe na huwa hatuna muda wakulilia mapenzi bali tuna muda wakusaka mahela tu hayo mambo mengine yatakuja baadae sana.
 
Sasa huo muda wakukaa na kuongea nae anaupata wapi ili amrekebishe?

Na anaanzaje kumrekebisha mtu kama huyo mwenye kutokujali waziwazi?

Unajua wakati mwingine tunajilazimishia jela ya mapenzi wenyewe!

Mtoa mada wewe ndo unajua zaidi uwezo wa kuendelea kuvumilia unao? Coz kwa dalili hizo ni wazi atakusumbua zaidi huko mbeleni

Uzuri wake wa sure, apiarence yake ya kuvutia na ongea yake ya mashamsham vyote hivo sidhani kama vitakua na faida kwako ilihali mapenzi yake kwako hakuna... .

Jipime kama waweza endelea ama lah!
Yaani kama vile umesoma moyo wangu, tatizo ni huo muda wa kupoteza na mtu anaeendelea kujisikia na kujiona bado yupo yupo
 
She is 22 yrs mkuu
Ahsante.hata kama ni mdogo anajua anachofanya.
Naomba nikupe pole na pongezi kwa kuwa unamhusisha Mungu ktk mahusiano yako hata kama kuna mahali unateleza kama mwandamu lkn unakumbuka kumrudia.Amini Mungu hatakuacha na kuna siku atakupa haja za moyo wako kwani anajishughulisha sana na maisha yetu.Kikubwa uwe mwaminifu kwa Mungu kuwa unamhitaji mke na si vingine kwani amesema mali na urithi mtu hupewa na babae bali mke mwema hutoka kwa Bwana.
- Tumia muda mwingi kwa maombi ukimkubusha Mungu haja yako kwani ampatae mke apata kitu chema.
-Kwa sababu saa zingine ni vigumu kumjua mkeo mtarajiwa ni yupi,tafuta kigezo kimojawapo utakacho mwambia Mungu,ukikiona kwa msichana utajua ndio wako(hutapoteza muda kwa mtu ambae sie)
-Jifunze kuwa na akiba ya penzi moyoni kwa ajili ya ulinzi pale mambo yakienda ndivyo sivyo.
- Ni muhimu kuwa na ukaribu wa kuonana mara kwa mara kwani utaimarisha mahusiano na kumgundua mtu mapema.
Kaka kuna mengi ila ni kukusaidia tu kutokana na uzoefu wa tulikotoka kwani maswala ya mahusiano hayana mwl kamili.Wengi unao waona kwenye ndoa kila mmoja ana uzoefu na mapito yake hata kama hayafanani.
 
Pole kaka umeniumiz san bt usikat tamaa katik mausian kila mtu upitia ivo kunakupenda na kutopendwa so kubsli yoot my dear kuchwa sio sabab yaww usindwe fny mengn ebu jarib kumpotzea taratbu
 
Naamin sipo mwenyewe, tusaidiane kwa ushauri na kufarijiana.



Kwanza nikupe pole kwa kuchoka, so Pole.
I know umechoka ndio maana the basic solution ya kupiga goti na kumuambia Mungu "Kama si mpango wako huyu dada aondoke na nimsahau" umeisahau kabisa.
Hakuna namna nyingine, go do that, and while you are at it - don't you forget to ask God to give you the right girl.
Vinginevyo utapambana sana mtaani ndugu yetu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom