Moyo wangu una majonzi, yako wapi mapenzi ya dhati?

Ahsante.hata kama ni mdogo anajua anachofanya.
Naomba nikupe pole na pongezi kwa kuwa unamhusisha Mungu ktk mahusiano yako hata kama kuna mahali unateleza kama mwandamu lkn unakumbuka kumrudia.Amini Mungu hatakuacha na kuna siku atakupa haja za moyo wako kwani anajishughulisha sana na maisha yetu.Kikubwa uwe mwaminifu kwa Mungu kuwa unamhitaji mke na si vingine kwani amesema mali na urithi mtu hupewa na babae bali mke mwema hutoka kwa Bwana.
- Tumia muda mwingi kwa maombi ukimkubusha Mungu haja yako kwani ampatae mke apata kitu chema.
-Kwa sababu saa zingine ni vigumu kumjua mkeo mtarajiwa ni yupi,tafuta kigezo kimojawapo utakacho mwambia Mungu,ukikiona kwa msichana utajua ndio wako(hutapoteza muda kwa mtu ambae sie)
-Jifunze kuwa na akiba ya penzi moyoni kwa ajili ya ulinzi pale mambo yakienda ndivyo sivyo.
- Ni muhimu kuwa na ukaribu wa kuonana mara kwa mara kwani utaimarisha mahusiano na kumgundua mtu mapema.
Kaka kuna mengi ila ni kukusaidia tu kutokana na uzoefu wa tulikotoka kwani maswala ya mahusiano hayana mwl kamili.Wengi unao waona kwenye ndoa kila mmoja ana uzoefu na mapito yake hata kama hayafanani.
Kaka sina maneno mengi , Mungu akubariki kwa ushauri mzuriii
 
Pole kaka umeniumiz san bt usikat tamaa katik mausian kila mtu upitia ivo kunakupenda na kutopendwa so kubsli yoot my dear kuchwa sio sabab yaww usindwe fny mengn ebu jarib kumpotzea taratbu
Tuko pamoja mkuu, ahsante sana na ubarikiwe
 
Kwanza nikupe pole kwa kuchoka, so Pole.
I know umechoka ndio maana the basic solution ya kupiga goti na kumuambia Mungu "Kama si mpango wako huyu dada aondoke na nimsahau" umeisahau kabisa.
Hakuna namna nyingine, go do that, and while you are at it - don't you forget to ask God to give you the right girl.
Vinginevyo utapambana sana mtaani ndugu yetu.
Ahsante sana kaka
 
Huyo si fungu lako. Maskini adi mekuhurumia Kama hutojal kuoa mtumishi, kuna mdada bikra safi mnene kiasi, maji ya kunde anayeelekea kuwa mweupe, mrefu, ni mdogo wangu. Tuna tabia Nzuri tu kwetu, hakuna aliyeoa kwetu akajuta. Ila sex kabla ya ndoa ni mwiko kwetu. Umri ni miaka 22. Kama utapenda tuwasiliane
 
Ndu zangu wana jamvi....

Naomba nieleweke hivi, nimechoka, sijui tatizo langu ni kwamba napenda sana bila kiasi, nimepitia kwenye mahusiano kama matatu sasa toka nijue mapenzi ni nini, mwanamke wa kwanza aliniumiza sanaa, nililia mwanaume machozi ya kila aina, sikuwa tayari aniache, nilikuwa naona kam maisha yangu yatakuwa magumu sana nikiachana na huyo dada.
Niliteseka kwa zaidi ya mwaka mmoja nambembeleza turudiane, alinitesa mno, siwezi kuelezea. Siku moja nilijifungia chumbani kwangu saa 11 jioni hadi kesho yake, nilifunga simu, nikapiga magoti, nilisali sana, nilimlilia Mungu moyo wangu upate amani, nikamshi Mungu kama sio mapenzi yake amuweke mbali na mimi yule binti, kweli siku ya pili nilikuwa mwepesiii, sikuwa hata na hamu ya kumtafuta, nilimshukuru sana Mungu maisha yangu yanaanza kubadilika mwishowe nikafuta mpaka namba zake japo hata leo ninazo kichwani....

Nikaanza mahusiano mengine, nikaona picha ni zile zile, nilikimbia mapema nilivoona tabia za mwanamke wangu wa kwanza zimeanza kujirudia kwa mwanamke huyo wa pili....nikamuomba Mungu nisiingie tena kwenye mahusiano kama vinginevyo iwe ni mwanamke wangu alieniandalia, nilikaa kwa karibu mwaka mmoja na nusu bila kuwa na mahusiano ya serious......

Mwaka huu mwezi wa Tano nilikutana na Binti mmoja mrembo kweli, ni mzuri kuanzia kutembea kwake, kuongea kwake, anapenda sana kanisa, kila Jumapili yuko kanisani ibada ya kwanza. Binti huyu kwa mara ya kwanza alikuja kwenye eneo langu la kazi, alikuja kumtembelea rafiki yake ambae pia staff mwenzangu, nilivyomuona kiukweli nilimpenda, nikajaribu kumuuliza yule rafiki yake, akanipa briefing kidgo kuhusu huyo binti, nilimuomba appointment ya kutoka nao wote wawili ili atleast nipate picha halisi na kujuana nae kidogo. Kwenye hiyo out tulibadilishana mawazo kidogo, tukabadilishana na mawasiliano pia, nikaanza kujenga nae urafiki, tukafahamiana vizuri then nikaona ni mtu ambae yuko smart kweli, siku moja nikamuomba appointment ya kutoka nae somewhere for lunch, hakukataa alikuja then tukaongea sana then nikamruhusu aende nyumbani mapema ili awahi mapishi ya jioni. Yote tisa, kumi huyo binti nilianza nae mahusiano baada ya kila mmoja kumfaham mwenzake,,,,ni takriban miezi 5 sasa toka tumeanza mahusiano rasmi, professionaly yeye ni mwalimu, mimi ni Muhasibu, tumekuwa tukiwasiliana vizuri sana, kinachonipa wakati mgumu kwake ni majibu yake, mara nyingi nikichat nae huwa ana majibu mkato sana (shortcuts), unaweza ukawa unamuuliza kitu sensitive yeye akakujibu majibu ambayo like she dont care. Kingine huyu binti amekuwa mgumu sana kushare nae muda, kama mpenzi wangu muda mwingine naweza muomba lunch tule sehem moja lakini akakataa bila sababu, nikimuliza sababu nini atakujibu niko busy ... hii statement ya niko busy imekuwa ikini disappoint sana, ukimuuliza busy na nini atakujibu sorry niko busy. Guys nisaidieni mtu kama huyu kweli bado anaweza kuwa na mapenzi ya dhati kwako? Katika chatting yake mara nyingi tumevutana sana, huwa ni mtu mwenye majibu ambayo yanaonyesha hajali kabisaa,,,

Tukiachana na hayo yote , wiki iliyopita wakati napiga nae story kwenye simu alichomekea agenda yake kuwa anataka kurudi chuo kwa miaka 3 kuanzia mwaka ujao kwa hiyo nikimhitaji maswala ya ndoa nisubiri mwaka 2020. Hili jambo limenikatisha sana tamaa guys, yaani nikae mtaani nimsubiri yeye anaenda chuo kwa miaka minne kuanzia sasa....moyo wangu uliumia sana kiukweli, bado naendelea kuumia, muda mwingine nawaza na kumwambia Mungu kwanini unanipitisha kwenye majaribu magumu kiasi hiki? Kweli ni binti niliempenda sana ila yeye kutokuwa na care inanikatisha tamaa, majibu yake mara nyingi ni " Poa, sawa, K, P n.k.
Guys wenye experience naombeni ushari, naumia kweli maana tayari nilishaingia kwake miguu yote, dalili ya kuumia tena naiona.

Sio dhihaka , sio utani napitia kwenye wakati mgumu, ambao tayari mko kwenye ndoa naomba mtusaidie mlipitia katika wakati kama huu?
Muda mwingine huwa namwambia Mungu mapenzi ya kweli yale ya wazazi wetu yako wapi? Kiukweli vijana wa kiume tunapitia wakati mgumu sana pindi unapomtafuta binti wa kuwa nae kimaisha.

Naamin sipo mwenyewe, tusaidiane kwa ushauri na kufarijiana.
Katika kipindi hicho cha miezi mitano, je tayari umeshamgegeda??

Kimsingi, huyo hakutaki, anae bwana mwingine anaempenda kwa dhati. Wewe kwako amejiegesha tu apate hizo lunch na vijisent vya saluni

Achana nae!!!
 
Pole sna bro,maneno yako yananiumiza sna ,najua umr wako utakuwa tyr kwa ajir ya kuishi na mwenza wako,lkn kuwa na subira huenda Mungu anakuepusha na mabaya zaid ya hayo pole ana
 
8374d1a5b3ca16f31ff36a0d29ca894d.jpg
 
Pole sna bro,maneno yako yananiumiza sna ,najua umr wako utakuwa tyr kwa ajir ya kuishi na mwenza wako,lkn kuwa na subira huenda Mungu anakuepusha na mabaya zaid ya hayo pole ana
Ahsante sana ndugu yangu
 
Huyo si fungu lako. Maskini adi mekuhurumia Kama hutojal kuoa mtumishi, kuna mdada bikra safi mnene kiasi, maji ya kunde anayeelekea kuwa mweupe, mrefu, ni mdogo wangu. Tuna tabia Nzuri tu kwetu, hakuna aliyeoa kwetu akajuta. Ila sex kabla ya ndoa ni mwiko kwetu. Umri ni miaka 22. Kama utapenda tuwasiliane
Hahahahaa mkuu nimejikuta kucheka, yaani umenifanya nifurahi tu. Ahsante sana
 
Inaonekena hata wewe hujatulia,kama unaharaka sana vile,sijui umri wako but try kurelax mapenzi ukiyakamia sana unahalibu,majaribu yako ni madogo sana lakini unapanick sana,relax,Mwanamke ni Kitabu ukikubwa sana huwezi kukimaliza kwa siku moja,ninachoweza kukushauri Relax,endelea kumwomba Mungu,Mwanamke anayejitambua mwenye njozi za mafanikio hutampata kwa njia rahisi lazima atakupima kwa mengi tumia akili zako vizuri kupima mambo na kuchukua hatua,stering hafi.
 
Pole duniani hapa hamna mapenzi ya kweli mi najua mapenzi ya dhati yalikuwapo enzi za kina Yesu na huwa naamini ukivalue mapenzi utapata partiner ambae ni pasua kichwa hasa ila siwezi semea watu wote naambiwa bado wenye mapenzi ya kweli wapo endelea kuomba maana kwa MUNGU yote yawezekana
Sio kweli..hapo ndio usaliti ulianza..Yuda Escariote mwanafunzi wa Yesu .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom