Movie ya Man on a ledge

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Image may contain: 7 people, people standing, text that says 'Tanweer WORTHINGTON ELIZABETH JAMIE ANTHONY GENESIS BANKS BANKS BELL MACKIE RODRIGUEZ HARRIS MAN ON A LEDGE DVD VIDEO RELIANCE'



...Taarifa ya kuwa baba yake kabakiza muda mfupi wa kuishi duniani ilimkuta akiwa nyuma ya nondo..

..Wakati hajajua aipokee vipi habari hiyo ni siku mbili mbele..akafungwa pingu akahudhurie mazishi..

..Nick Cassidy alilia akiwa jela..akalia tena alipokuwa mbele ya kaburi la baba yake..

...Kesi ya kuiba almasi yenye thamani ya dola milioni arobaini,ndiyo iliyomfanya ahukumiwe miaka 25 ndani ya gereza la Sing Sing Correctional Facility..

...Ye ni askari mstaafu..na wala hakuiba mali ile..na njia pekee iliyomjia akilini ya kulisafisha jina lake..ni kutoroka jela..

..Ndio..Nick Cassidy alihudhuria msiba wa babaake..lakini hakurudi tena jela..aliondokea pale pale makaburini..

..mbele ya macho ya maaskari..akawaonesha kuwa hata yeye alikuwa askari kabla..kurasa ikafungwa hapo..

..Roosevelt Hotel,ndani ya Manhattan, New York City akiwa na jina la bandia..Nick alichukua chumba,akalipia na chakula akaletewa..lakini hakula..

..Alikuwa na jambo lake..

..Ni jambo hilo ndilo lililofunga mitaa..ni kwa jambo hilo ndipo maaskari walipouona uchizi wa mtu anaedai haki..

..Ilianza kama utani..watu wakajua haiwezekani,wengine wakaamini ni maigizo..polisi walipokuja kulitilia maanani jambo lile..

..Walikuwa wameshachelewa..

..Umbali mrefu kutoka chumba cha ghorofa ya 21..mwanaume huyu alifungua dirisha akasimama kwenye ukingo uliobakiza sehemu ndogo tu ya kiatu chake...

..Wananchi waliporipoti taarifa ya kuwepo kwa mtu anaetaka kujiua kwa kujirusha ghorofani..polisi walifika hotelini na kuanza uchunguzi..

..Nyuma ya tukio la Nick kuna uhalifu uliotakiwa kudhibitiwa..

...Nick cassidy hataki kuongea na mtu yoyote..anachohitaji ni mwanamke tu..what a mess..

..Yaani mwanamke ndo kamsimamisha pale na kufanya mji mzima usimame kwa masaa..yaani ni mwanamke ndo anafanya nchi itangaze live habari yake!..

..Ni big plan..asipoletewa anachokitaka anajirusha..kutaka kujiua ni kosa kisheria..na ye analijua hilo ndo maana yupo pale kwa makusudi..

..Anavunja sheria anayoijua..

..Polisi hawawezi kusogea alipo..ni sehemu hatari sana..njia pekee ni kumtimizia mahitaji yake..akaulizwa mwanamke anaemtaka,akawajibu..

..Lydia Mercer..mwanamke mwenye kazi moja tu kwenye jeshi la polisi..kila anapohitajika mtu wa kushawishiwa jambo..basi aliitwa mwanamke huyu...ni detective negotiator..

..Nick cassidy anawatuma polisi wamuitie mtu anaeweza kumshawishi yeye ashuke pale..polisi wanashangaa..mbona hajirushi kama kweli ni mtu wa kujirusha!...anawasumbua..

...Mwanamke yule alifika na alifanya kila uwezo wake kuongea na nick atoke pale juu..akamuhakikishia mpaka usalama wake baada ya tukio lile..

..Asichokijua mama yule na jeshi lake la polisi ni kitu kimoja tu..

..Nick Cassidy hayupo pale kwa bahati mbaya..ni plan ya akili iliyopangwa mwaka mmoja nyuma..

..Nick aliuhitaji muda wa polisi..alitaka attention ya marekani yote iwe kwake..na ndicho kilichotokea..na lengo ni moja tu..

..Ile almasi aliyoambiwa kaiiba mpaka akaenda jela..alikuwa anataka kuiiba kweli..

..Bado hujanielewa..(kwa sababu unajiuliza ataibaje na ye yupo ghorofani anataka kujiua)

..Maaskari wakiwa na heka heka za kufunga mitaa na zimamoto za mji mzima kurundikana pale hotelini..kaka wa cassidy alikuwa kwenye vault ndani ya jengo iliyopo ile almasi..

..Kwa kutumia maelekezo ya cassidy pale alipo..alikuwa akiwasiliana na kakaake na kakaake alikuwa akimwambia aendelee kuwapumbaza maaskari kuwa anataka kujirusha..

..Ni suala la kuununua muda wa jeshi la polisi kwa gharama ya kuwapigisha stori...

..Polisi wana deal na nick asijirushe ghorofani..kumbe wahuni wanafanya tukio kubwa kuliko wao walivokusanyika na kufunga mji..

..Nick ni genius alietaka kuionesha dunia matumizi ya akili..

..Muda polisi walipokuja kugundua wameibiwa akili...

...walijiona hawakuwa nazo hata hizo akili zenyewe..

..#MAN ON A LEDGE
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom