Mother tongue and first language whats the difference

Mtazamaji

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
5,937
1,437
Wanajamvi
Nina swali la kutaka kupata ufafanunuzi wa mipaka, tofauti na sifa kati Mother tangue( lugha ya mama) na 1st language ( lugha ya kwanza)

Mfano mitatu tofauti ni mimi ni Mgogo:-

  • Nimezaliwa dar nikajua kiswahili na kujifunza kigogo.
  • N nimezaliwa dodoma nika aqcuire kigogo na kiswahili nikakijua kwa kujifunza
  • Nimezaliwa dar nikajua kiswahili baada ya muda nikaenda majuu na sijui kigogo najua kiswahili na kingereza
Sasa ni lugha ya mama na ipi ni lugha ya kwanza ipi katika hayo mazingira tofauti.

Karibuni tuelimishane
 
Ulivyonza kujua kuongea (wakati huo una miaka 2 hivi), ulianza kuongea lugha gani? kwangu mimi nadhani hiyo ndio 'monther tongue' (kwa maana kuwa ndio lugha wazazi/walezi wako walikuwa wakikuongelesha) na pia ndio lugha yako ya kwanza kujua kuiongea. Hivyo, lugha ya kwanza na 'mother tongue' ni kitu kimoja tu.
 
Ni jibu sahihi, no comments
 
Aksante sana
kwa hiyo mgogo aliyezaliwa dodoma na kuongeleshwa kigogo kajifunza kiswahili shuleni kiswahili kwake itakuwa second language Na kingereza baadaye third language?
 
A lugha ya kwanza (lugha ya asili, lugha ya mama (mother tongue) ) ni lugha ya mtu aliyo jifunza tokaea kuzaliwa kwake.

Ila wapo baadhi ya wataalam wa Lugha wanatufahamisha kuwa Lugha ya kwanza au Mother Tongue ni ile lugha ambayo mtu anafikiria kwayo au Lugha ambayo wewe unaijuwa zaidi ya lugha zingine kwa maana ya kuitumia zaidi na hata kwenye kufikiri unaitumia hiyo lugha.

Kwa upande mwingine, lugha ya pili ni lugha yoyote ambayo mtu anaongea zaidi ya lugha ya kwanza. Yaani lugha ambayo umejifunza baada ya kujua lugha ya kwanza au Mother Tongue.
 
Ulivyonza kujua kuongea (wakati huo una miaka 2 hivi), ulianza kuongea lugha gani? kwangu mimi nadhani hiyo ndio 'monther tongue' (kwa maana kuwa ndio lugha wazazi/walezi wako walikuwa wakikuongelesha) na pia ndio lugha yako ya kwanza kujua kuiongea. Hivyo, lugha ya kwanza na 'mother tongue' ni kitu kimoja tu.

Mother tongue ni lugha ya wazazi wako. Si lazima iwe lugha ya kwanza, japo mara nyingi ni hivyo. Wakati mwingine lugha ya kwanza siyo mother tongue, bali ni lugha ya kujifunza, tukichukulia mfano wa jamaa kwamba Mgogo (kwa kabila la wazazi wake) aliyezaliwa akajifunza kiswahili kama lugha ya kwanza kwa sababu ya urahisi huo unaotokana na mazingira, na baadaye akajifunza kigogo. Kiswahili haiwi mother tongue kwa sababu amekijua kama lugha ya kwanza, bali itabaki kuwa lugha ya kwanza. Mother tongue ambayo amejifunza baadaye itabaki kuwa kigogo kwani ndiyo lugha ya wazazi wake, lugha ya asili yake (kabila lake).
 
1. Mother tongue ndiyo hiyo hiyo 1st Language (L 1), Native Language au Arterial Language!! Hii ni ile lugha mtu najifunza mar atu anapozaliwa/aliyojifunza na ndiyo anajitambulisha nayo kimawasiliano na jamii kubwa kwenye nchi yake
2. Inaweza pia kuwa lugha ya mama au inarepresent ethnic group yako
Defining mother tongue

  • Based on origin: the language(s) one learned first (the language(s) in which one has established the first long-lasting verbal contacts).
  • Based on internal identification: the language(s) one identifies with/as a speaker of;
  • Based on external identification: the language(s) one is identified with/as a speaker of, by others.
  • Based on competence: the language(s) one knows best.
  • Based on function: the language(s) one uses most.
 
Kitu gani kinacho kuchanganya?
Mkuu malezo yak nimeyapata hasa lile kuseam lugha ya mma ni ile mtu unayotumia hata ukiwa unafikiria nahisi linaweza kuwa sahihi. Kuwa naweza kuwa mgongo lakini memory yangu inadecode na kurecall info kwa kiswahili then kuzitafsiri kama inabidi

Sasa kuna maelezo ya wadau wengine naona yanachanganyana ila maelezo ya wadau wote yamenipa mwanga zaidi.
 
Mkuu nashukuru kwa kunielewa, kuhusu hao wachangiaji wengine kuna msemo siku hizi unasema hivi "Akili za kuambiwa changanya na za kwako". Basi ushauri wangu ni kuwa chukuwa kile ambacho wewe unakiona kuwa kinafaa.
 
Kwani hakuna mtaalam wa lugha kabisa ambaye anaweza kutupa msimamo juu ya hili? Ningependa kujua hitimisho hapa ni lipi.
 
mf.wazazi wangu ni wahehe na nikazaliwa,na lugha niliyofunwa kuaza kuongea ni kiswahili nilipoenda shule kiingereza na kihehe kidogo nimejifunzia ukubwani
nijuavo:mother tongue ni kihehe, ila first language ni kiswahili,kiingereza second language,kikorea third language nk
 
mother tongue is your venecular language, thelanguage u speak but it must be from where u originate......first language is the language u acquire firstly........its possible for ya mother tongue to be your first language........
 
Mimi ninavyoielewa MOTHER TONGUE si lazima ufahamu kuizungumza ile lugha yenyewe ya mother tongue. Ila ni namna unavyozungumza lugha zingine kwa kutumia matamshi na sauti za lugha ya kwenu. Mother tongue ni lafudhi.Kama unapozungumza kiingereza, kiswahili, au lugha nyingine ya kigeni, kama lafudhi yako ni ya kisukuma basi your mother tongue is sukuma. Kuna jirani yetu mchagga ana watoto watatu. Wale wakubwa wawili waliwahi kuishi kwa bibi yao Moshi lakini hawana lafudhi ya kichagga.Yule mdogo hajawahi kukaa Moshi zaidi ya wiki 1, lakini kiswahili chake ni kichagga kitupu. Thats why nikasema mother tongue si lazima ufahamu kuzungumza ile lugha bali ni "LAFUDHI"
 
mf.wazazi wangu ni wahehe na nikazaliwa,na lugha niliyofunwa kuaza kuongea ni kiswahili nilipoenda shule kiingereza na kihehe kidogo nimejifunzia ukubwani
nijuavo:mother tongue ni kihehe, ila first language ni kiswahili,kiingereza second language,kikorea third language nk
Hii ninaikubali zaidi kwa sababu unaweza kuwa na "mother tongue" kwa maana ya lugha ya mama kuliko lugha mama. Katika hali hii, hata lugha ya mama ikiwa huitumii kila mara, ulijifunza ukiwa na umri mdogo baadaye ukawacha kuitumia mara kwa mara, inaweza kuwa na athari ndogo kwako kuliko lugha ya kwanza, L1, ambayo unaitumia kila siku. Ama iwapo unatumia lugha mbili, ya mama na ya kwanza kwa uwezo ule ule hii inajulikana kama "bilingualism".
 
Mother tongue is the first language that a child acquire just directly from a mother and this is to those who have raised by their mother while first language is the first language to be acquired by a child from guardians, it can be a house girl, sister neighbors this is to children raised by guardians and not his or her mother. All are first languages but mother tongue a teacher is a mother. I am linguist so take it from me.
 
Ulivyonza kujua kuongea (wakati huo una miaka 2 hivi), ulianza kuongea lugha gani? kwangu mimi nadhani hiyo ndio 'monther tongue' (kwa maana kuwa ndio lugha wazazi/walezi wako walikuwa wakikuongelesha) na pia ndio lugha yako ya kwanza kujua kuiongea. Hivyo, lugha ya kwanza na 'mother tongue' ni kitu kimoja tu.

Mother tongue ni lugha ya mama ambayo unapaswa kujifunza mara unapozaliwa ikiwa na maana kuwa baba na mama yako wanaongea lugha moja kwa maana ya kabila. Lugha ya kwanza kwetu sisi ni kiswahili na lugha ya pili ni nyingine yeyote iwe ya kigeni au ya kabila lingine la nchini mwako kwa wale wenye wazazi wa kutoka kabila tofauti lugha ya baba ndio mother tongue kwani mother tongue ina maana lugha ya asili yenu na si lugha ya mama.
 
kwa mujibu wa wataalamu wa lugha haya majina'mother tongue, first language, second language and foreign language' hayatokani na series (mfuatano) bali kiwango cha umahili (compitence) katika lugha husika. Nikweli pia kuwa fitrst language ndo mother tangue maana mtoto ataanza kuongea lugha ya mama (kwa kudhani kuwa kila mtoto analelewa na mama yake na wale jamaa wakaribu so ataanza kutumia lugha ya mama ( wana ita 'to acquire' sio 'to learn' yaani kujifunza.Inaaminika kuwa mtu atakuwa mahili sana katika lugha ya kwanza/mother tongue. Kwa upande wa second language ni lugha ambayo mtu anajifunza baada ya lugha ya kwanza/mother tongue. Umahili katika second language ni ni mdogo kulinganisha na mother tongue. So kama lugha ni ya kwanza lakini sio ya mama inakuwa first language ila umahili unakuwa sawasawa. Na lugha yoyote itakuwa second language kwa mtu iwapo tu sio mother tongue/first language na iwapo anaonyesha umahili mkubwa. Hata kama ni lugha ya kigeni kama mtu anaimudu kiasi cha kukaribia native speaker lugha hiyo ina kuwa second language kwake sio foreign. So mtu anaweza kuwa na lugha tatu au nying zikiwa second languages kwake ilimradi tu ni mahili. maanake nikuwa anazimudu kwa kiwango cha lugha ya pili. So hakuna kitu kama third language and so forth.
 
First language sio lugha ulianza kuongea ya kwanza. Ni lugha ambayo unaifahamu kuliko zingine zote. Mother tongue ni lugha ya "kwenu".
Kwa hali ya kawaida english haiwezi kua mother tongue ya mtanzania. Ila mother tongue inaweza kutokea kua your first language. na first language inaweza badilika kadiri mtu anajizoweza kuzungumza lugha mpya.
Kwa mifano hapo juu:
1. Mother tongue Kigogo, first language Kiswahili sababu ndicho unakielewa zaidi
2. Mother tongue and first language Kigogo sababu ndio kina dominate na ndio lugha ya "Nyumbani"
3. Mother tongue Kiswahili na kama english imepanda kuliko kiswahili basi inakua ndio first language.
 
Back
Top Bottom