Sasa utaweza kueleweshwa na Kutafsiriwa video yoyote yenye lugha yoyote kupitia AI(Akili bandia)

KENGE 01

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
1,592
3,839
IQ>>AI

Na KENGE

Technology ya AI inazidi kukua siku hadi Siku,kupelekea makampuni makubwa kama Google na Microsoft kushindana ubunifu wa AI Technology.Kwasasa tumeona picha nyingi zikisambaa kila mtu anaweza kutengeneza picha yake kama tulivyoona hapa
Jinsi ya kutengeneza Picha kwa AI

Kwasasa makampuni makubwa yamewekeza nguvu nyingi kwenye AI ili kurahisishia watumiaji wake.

Lugha ndio Tatizo kubwa la dunia nzima,Kati ya matatizo makubwa ya dunia.Hasa nchi yetu ambayo lugha Mama ni Kiswahili hivyo wengi wamekutana na changamoto ya kujifunza zaidi ,Kupitia youtube kwani Video nyingi zemye content nzuri zinatumia Lugha tofauti kama Kingereza,Kihindi n.k

Sasa kupitia BARD AI ambayo ni ya google.Unaweza kutafsiri na kutafuta video yoyote youtube kwa njia ya kucopy na kuoaste link kama @KENGE01 navyokueleza:

1.Fungua browser yoyote kama Chrome,Opera mini n.k
Kisha Search kwa kuandika Bard AI.Kisha utaingia(Sign in) kwa account yako ya google
Picsart_23-12-06_20-32-26-307_1.jpg


2.Baada ya kuingia utaweza kuandika/Kuuliza chochote kwenye uwanja wa kuandika message(prompt)

Kama unataka kutafsiri au kutafuta video au Content ya kitu.hapo ndio mahala pakole.Lakini kama unataka kuelezewa video hakikisha unalink yake kutoka youtube
Picsart_23-12-06_19-52-46-084.jpg


KUTAFUTA VIDEO:
Kama unataka kutafuta video utafata hatua hizi:
Hapa chini mfano utaona KENGE alichukua mfano wa Trend ya sasa ni Miso Misondo.

Nikamuuliza AI hawa Miso Misondo ni kina nani,Na Nitafutie Video ikiwaonesha historia yao
Picsart_23-12-06_20-10-58-537.jpg


Kama unavyoona kwenye Picha,AI imetafuta Video inayohusu kina Miso Misondo na Kuuliza kama Nataka kuiangalia,Nami nikajibu ndio.Akanipa link.Link ambayo imeelezewa kila kitu kama mtunzi,muda n.k
Picsart_23-12-06_20-13-18-059.jpg


KUELEWESHWA VIDEO :

Unaweza kukutana na Video ukaangalia na hukuelewa chochote.Pia lugha inaweza kuwa sio Rafiki.Lakini kupitia AI sasa unaweza kupata muongozo na mwanga wa Video yoyote kama ifuatavyo.

Link ya Video,
Hakikisha unalink ya video husika.Mfano tutaangalia jinsi ya kupata Link ya video kutoka youtube

1.Ingia youtube kisha Search Video uitakayo:
Mfano hapa kwa haraka nimesearch jinsibya kupika PIZZA
Picsart_23-12-06_20-16-26-020.jpg


2.Bonyeza Share.
Picsart_23-12-06_20-19-38-690.jpg


3.Kisha copy Link

Picsart_23-12-06_20-22-35-818.jpg

Hapa link itajicopy kisha tutarudi kwenye Bard AI na kupaste kama ifuatavyo

Fungua Bard AI kisha Andika kwa mfumo huu:
(Nielezee kwa kifupi kuhusu video hii: weka link hapa )
Ai itakuelezea kwa kifupi video inahusu nini na Creator anachofanya
Picsart_23-12-06_20-25-22-429.jpg


Hivyo kwa wale wapenda tutorial za youtube,Ndio muda wa kuburudika.Kitu cha kuzingatia ni kwamba bado haiko stable sana kwahiyo baadhi ya Video inakua ngumu kutafsiriwa na AI.Lakini kwa siku,miezi,Miaka ijayo naamini itakua na uwezo wa kutafsiri video yoyote ile.

Kwa youtuber kama ulikua na wasiwasi wa kupoteza viewer,basi ondoa shaka kwakua mtu akishacopy na kupaste link yako tu kwenye Bard AI,kule youtube ataonekana na kuhesabika kama viewer hivyo haitaathiri viewer wako kabisaa.

Nimalizie kwa kusema AI wala sio Technolojia mpya ni tech ambayo ipo karne na karne,Licha ya kupewa kipaumbele miaka hii lakini toka karne Robotics,Machine learning na AI vipo,hivyo kumekuwa na Trend ya kutishana kwamba Miaka ijayo binadamu tutakosa kasi na kuachia AI ifanye kazi.Napinga kabisa

AI ni Tech nzuri lakini haitokaa kupindua mwanadamu kwakuwa akili ya mwanadamu ni masterclass haina mbadala.Hii ya kuOverrate AI ni uongo ndio maaana nimeanza kwa kuandika IQ(Kipimo cha akili ya Mwanadamu) >>(Ni Kubwa zaidi ya ) AI(Akili Bandia)

Nawasilisha
 

Attachments

  • Picsart_23-12-06_20-22-35-818.jpg
    Picsart_23-12-06_20-22-35-818.jpg
    78.4 KB · Views: 9
AI inaenda kumuwezesha binadamu kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja,ni vyema kila mtu akaangalia namna ya kuitumia teknojia hii kijiongezea maarifa na kipato(maokoto)
 
AI inaenda kumuwezesha binadamu kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja,ni vyema kila mtu akaangalia namna ya kuitumia teknojia hii kijiongezea maarifa na kipato(maokoto)
Hakika Lakini bado Nafasi ya mwanadamu haitaweza kuzibwa na AI
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Mi kila link nayoweka pale kwa BARD AI inagoma ku-process
 

Attachments

  • Screenshot_20231210_084248_Chrome.jpg
    Screenshot_20231210_084248_Chrome.jpg
    142.5 KB · Views: 10
Mi kila link nayoweka pale kwa BARD AI inagoma ku-process
Japo bado ipo kwenye matengenezo,ila baadhi ya content zinakataliwa mfano video ikiwa inajipromote sana au n.k..Pia badili prompt unaweza kuandika ivi "(Explain what the creator is doing in this video: http://link)" jaribu ivyo
 
Back
Top Bottom