Most dependable, reliable and honest Clearing & Forwarding Agents in Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Most dependable, reliable and honest Clearing & Forwarding Agents in Dar es Salaam

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Bucktooth Maftaha, Feb 8, 2013.

 1. Bucktooth Maftaha

  Bucktooth Maftaha JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2013
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 373
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nimewahi kutuma magari mengi kutoka Japan pamoja na makontena kutoka Marekani, lakini experiences zangu zinatofautiana sana kuhusiana na uwezo, uaminifu na gharama za kutoa mzigo wako kutoka bandarini baada ya kumwachia kazi Clearing & Forwarding Company and/or Agent.

  Kwa maada hii, ningependa kufahamu maoni ya Wahusika kuhusu companies au independent Clearing & Forwarding Agencies zenye sifa tofauti ili wadau tupate picha kamili kuhusu uwezo na mapungufu ya kampuni au agents waliyo kwenye biashara hii ili Wadau tuwe na picha kamili ya nani anafaa na nani wa kumkimbia.

  Tumechoka kulipia mamilioni ya shilingi kwa storage charges na gharama nyinginezo ilhali shipping documents na exemptions zimekamilika hata kabla ya mzigo bado kuwasili bandarini, na gharama za mwanzo zinalipwa, lakini kwa makusudi, Clearing and Forwarding Agents fulani wana tabia ya kuchelewesha kutoa mzigo wako bandarini kwa sababu lukuki zisizo na maana, hadi grace period ya siku 21 inapita na hatimaye unaishia kulipa mamilioni in storage charges na upuuzi mwingine kwa wawekezaji binafsi wenye container yards kama Azam na wengineo.

  Napenda kuwakilisha!
   
 2. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 60
  Umeleta mada moja bomba sana, ninahasira na agent kishoka mmoja nitakuja kumwaga A to Z, stay tuned!! Jamani tuelezeni tusiendelee kuibiwa! Tukimbilie makampuni au agents binafsi, au wote hawaaminiki?
   
 3. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2013
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,900
  Likes Received: 612
  Trophy Points: 280
  katika mambo yanayoleta usumbufu kwenye importation ni clearing agent .... kupata aliyemwaminifu ni kazi ... na ukimpata usimuachie

  ngoja tupate maoni zaidi
   
 4. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2013
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,357
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Clearing agents wengine wanakula na watu wasio wahaminifu TRA. Kwa kweli nchi yetu kuna mambo mengi yanatia kinyaa hasa kama umewahi kwenda nchi zingine na kuona jinsi watu wanavyofanya mambo. Professionalism kwetu ni zero. Kila mtu anaangalia jinsi ya kupata viela vya 5ok, 100k za kunywa tu bila kujali mteja anavyoumia. Kuna clearing agent nilishamtupia hela baada ya kuona ananjaa kali kwa kusema uongo wa kijinga.
  Nilimpata mwingine ambaye ni mzuri kwa magari kama documents ziko sawa ni mzuri lkn ni wachache wazuri kuwapata bongo
   
 5. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2013
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 0
  Mtaje kaka na sisi tunufaike na ufanisi wake
   
 6. Bucktooth Maftaha

  Bucktooth Maftaha JF-Expert Member

  #6
  Feb 9, 2013
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 373
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu tuambie sababu zako zinazokufanya useme ni bora, na kama vipi umtaje ili tumpelekee biashara.
   
 7. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #7
  Feb 12, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 60
  Kagalala mkuu wangu hebu tudokeze nasi tukapate huduma yake, yaani mkijigundulia chimbo zuri inakuwa siri tena jamani ?! Funguka mkubwa watu tumeumizwa sana, tunapaswa kumpromoti huyo agent wako mzuri tusipeleke kazi kwa VISHOKA!!
   
 8. Kubota

  Kubota JF-Expert Member

  #8
  Feb 12, 2013
  Joined: Oct 21, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 60
  Ninawapa number ya simu ya Ajenti mmoja kichaa bandarini Dar! Ogopa hiki kichwa!! 0713412152 anasauti ya mtu mzima kutoka bara lafudhi ya Sumbawanga. Mtu mwenye nafasi naomba ampigie na akamuone aweze kujionea sura ya wagangaji bandarini Dar es Salaam ilivyo! Hawa ndiyo aibu ya Tanzania! Kumbe pale bandarini hakuna utaratibu kiasi kwamba watu kama huyu wanaruhusiwa kufanya huduma hii! Huyu KISHOKA wa bandarini ni mtu mwenye umri wa wastaafu!

  Huyu KISHOKA alipokea malipo na ilipofika kutoa mzigo akasema iongezwe pesa kubwa tu tofauti na mapatano, nilipompa uthibitisho wa bei tuliyopatana akaweka kinyongo, mzigo alichelewesha saaana kutoka! Mzigo ulipotoka ulikuwa haujakamilika! Aliamua kujifidia kwa kupunguza vitu.

  Sababu ya kuchelewa sana kutoa mzigo kumbe hapo bandarini Dar hawa maajenti VISHOKA huwa wavizia kutoa mizigo kiujanja ili wasilipie baadhi ya charges, wapate faida kubwa zaidi, sasa safari hiyo huyo KISHOKA alikwama kuutoa mzigo kwa vichochoro vyao wanavyovijua na ndiyo ikawa chanzo cha kuchelewesha mzigo. Yaani nadhani tunapaswa kutambua watu na makampuni mazuri, wana JF tusaidiane kwa hili.
   
 9. lucky sabasaba

  lucky sabasaba JF-Expert Member

  #9
  Feb 12, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 1,673
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Kubota umenikumbusha mbali sana kuna jamaa mmoja kishoka anaitwa NATHAN ni agent pale Bandarini ,nilisoma naye MKWAWA iringa,niliagiza mark 2 akanipa makisio ya 3.5ml Kabda kodi hazijapanda,nilimpatia pesa sikumwona wiki 2 simu pia haipatikani!!!!!nilimtafuta bosi wake akaniambia anatafutwa na watu wengi sana,sio mwaminifu,ata pale central police wanamjua vizuri,nilipeleka malalamiko yangu wakasema mambo ya huyo bwana ni magumu!!!!husijaribu kukutana na mtu huyo,gari lilikaa zaidi ya wiki 3 Bandarini likaibiwa vifaa vingi sana na storage chaji ikaja Juu sana,husijaribu kumtafuta Huyu kishoka,sitaki tena maagent wenye ofisi za briefcase
   
 10. lucky sabasaba

  lucky sabasaba JF-Expert Member

  #10
  Feb 12, 2013
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 1,673
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Uongo wao unafanana eti Leo SYSTEM IPO DOWN sasa tungoje kesho!!!!!!!!!!!
   
 11. M

  Mfikilwa JF-Expert Member

  #11
  Feb 12, 2013
  Joined: Mar 11, 2008
  Messages: 356
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mie nawish turuhusiwe wenyewe wenye mizigo tuwe tunatoa mizigo yetu, magent wote hawafai, mie nimeshabadilisha maagent mpaka basi tena, hawafai, yani hawafai hawafai hawafai
   
 12. MKATA KIU

  MKATA KIU JF-Expert Member

  #12
  Feb 12, 2013
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,171
  Likes Received: 953
  Trophy Points: 280
  Tatizo wabongo tunapenda Bei rahisi,,,

  Nendeni kampuni za logistics za kueleweka dunian muwape kazi,,,, wakizingua mnawacharge wao..

  1. KUHNE + NAGEL ipo dunia nzima na inafanya shughuli zote za logistics so hata bongo wapo

  2. DHL nao wanafanya mambo yote na Bongo wapo

  3. BOLLORE AFRICA LOGISTICS wale wanaoimiliki AMI ICD na SDV nao wanafanya shughuli zote hadi clearance...

  Ukitaka uhakika nendeni kampuni za kueleweka wakufanyie kazi japokuwa gharama zao ni kubwa na hawataki longo longo hakikisha documents zote unapeleka wakati sahihi uone kama watashindwa kufanya...

  Through my Experience Kuhne + Nagel na SDV ni wazuri sana tatizo lao wanafanya clearance za makampuni tu yaani mizigo mingi,, kama una kagari chako kamoja sijui kontena la moja au mawili Sizani kama wanakubali,,,, ila jamaa hawana longo longo

  Hizi kampuni kubwa hazitaki usumbufu na wewe mteja we unapeleka document na una confirm tu wakati wa Declarations kama kodi ipo hivi... Then wanakulipia kila kitu Wao baada ya Kazi yako kuisha umeshapata hadi mzigo wako Ndo unaletewa Invoice ufanye malipo yote hadi waliyokulipia wenyewe...

  Na kutokana na style hii hawafanyi kazi na wateja wadogo wasioeleweka,,, lakini Ni wazuri vibaya mno,,, kama unataka uhakika nenda kampuni zenye reputation kwenye logistics industry duniani
   
 13. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #13
  Feb 19, 2013
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,216
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Sio kila Mtanzania anaweza kumudu hizo gharama za hayo makampuni uliyoyataja.
  Na ukizingatia makampuni mengi makubwa huwa wana idadi za Containers au magari ili kukupokea Kama mteja.
  wafanyabiashara wengi wakubwa Kariakoo na hapa mjini kwa ujumla huwa wanatumia hizi kampuni za wazawa zenye ufanisi na weledi katika kazi husika.

  Mimi binafsi huwa huwa natumia Logistic Co. moja hapa mjini katika Import and Export,kwa kweli huwa wananifanyia kazi zangu vizuri na kwa muda unaotakiwa. Ni kweli wapo VISHOKA wa kuwaogopa Kama ukoma. Ila kuna makampuni machache ya wazawa yanayofanya vizuri kwenye sekta husika.

  Kama kuna mtu yuko serious anahitaji msaada kuhusu masuala ya Logistics nijulishe ili nikupatie njia ya mawasiliano ya hiyo kampuni.
   
Loading...