Moshi: Mstaafu wa Polisi ajinyonga baada ya mke wake kuuza nyumba na mali nyingine

Mwaka mbaya huu kila mkoa siyo Kilimanjaro Tu. Mengine hata hatuna taarifa nayo. Yaani kujiua, kuawa, ndiyo imeshika Kasi. Laana hii.
Mbona unawahi kusema kuwa sio Kilimanjaro tu. So unaona hapo dada zenu wamefanya Yao na huku wanaolewa Sana na wanaongoza kuolewa.

Sasa subiria ustaafu ama uzeeke ndo utajua kuwa maji ni chakula kuliko vyakula vyote
 
Dah, tuanze kuficha hati sasa.....ni kusurrender tu mahala na kusign wa kuichukua ni wewe, mwingine anaweza tu kuchukua ukifa tena watoto wote wawe above 25yrs na waridhie ndio mama apewe...

Hawa wenzetu wanaweza hata kushawishiwa na kitoto cha 25yrs kikiwa kinampiga pipe akauza nyumba au kusurrender hati... (sorry kwa lugha ya kihuni)
 
Mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Omary Charema Msangi amejiua kwa kujinyonga bafuni kwake kwa kutumia waya wa pasi.

Tukio la kujinyonga mstaafu huyo limetokea usiku wa kuamkia jana akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi ambapo mwili wa mstaafu huyo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio leo Jumatano Januari 26, 2022 akisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kujinyonga kwa mstaafu huyo.

"Ni kweli hili tukio limetokea na tunafuatilia kujua hasa chanzo cha kujinyonga kwake," amesema Kamanda Maigwa

Taarifa za chanzo cha kijinyonga kwa askari huyo kutoka kwa mmoja wa ndugu wa familia hiyo zinadai kuwa wakati mwanaume huyo akiwa kwenye matibabu mkoani Dar es salaam, mke wake alitumia nafasi hiyo kuuza mali zake zote ikiwa ni nyumba, mashamba pamoja na mali nyingine.

Inadaiwa kuwa baada ya mtaafu huyo kurejea nyumbani kutoka kwenye matibabu alikuta nyumba yake imeuzwa na kulazimika kwenda kupanga.


Mwili wa mwanaume huyo unatarajiwa kuzikwa leo Usangi Wilaya ya Mwanga.

Mwananchi
 
Kama ana hati inauzwa tu
Si kuuza tu hata ikiwa ni kuichukulia mkopo lazima maridhiano ya wawili yathibitishwe! Sheri mbona ipo wazi kwa hili? Na kama alifia nyumbani kwake iweje iuzwe na marehemu asiende popote kudai haki yake? Kuna la zaidi hapa.
 
Mke anauzaje nyumba ya mume wake ama nyumba ya pamoja?

Nyumba sio nyanya iuzwe bila mashahidi wala majirani
Anaweza kusingizia mumewe yuko Dar mahututi, hivyo anatafuta pesa za kumtibia. Kweli mume yuko Dar Kwa matibabu, Nani hataamini, ikizingatiwa ni mkewe?
 
Myebusi wala usishangae alipangiwa atakufa hivyo. Wangapi wanakumbana na mishtuko ya hatarii lakini hawajinyongi? Kwasabab hawakupangiwa watakufa hivyo.
Mkaldayo Tz huku huu mwaka vifo vya kuuwawa,kujiuwa vimekuwa vingi sana..
 
Back
Top Bottom