Moshi: Mstaafu wa Polisi ajinyonga baada ya mke wake kuuza nyumba na mali nyingine

Mstaafu wa jeshi la polisi wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro bwana Omary Msangi amejinyonga hadi kufa baada ya kwenda kutibiwa jijini Dares salaam na aliporudi akakuta mke wake ameuza kila kitu ikiwemo nyumba na mashamba hivyo kulazimika kwenda kuanza maisha ya kupanga nyumba.

----
Mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Omary Charema Msangi amejiua kwa kujinyonga bafuni kwake kwa kutumia waya wa pasi.

Tukio la kujinyonga mstaafu huyo limetokea usiku wa kuamkia jana akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi ambapo mwili wa mstaafu huyo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio leo Jumatano Januari 26, 2022 akisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kujinyonga kwa mstaafu huyo.

"Ni kweli hili tukio limetokea na tunafuatilia kujua hasa chanzo cha kujinyonga kwake," amesema Kamanda Maigwa

Taarifa za chanzo cha kijinyonga kwa askari huyo kutoka kwa mmoja wa ndugu wa familia hiyo zinadai kuwa wakati mwanaume huyo akiwa kwenye matibabu mkoani Dar es salaam, mke wake alitumia nafasi hiyo kuuza mali zake zote ikiwa ni nyumba, mashamba pamoja na mali nyingine.

Inadaiwa kuwa baada ya mstaafu huyo kurejea nyumbani kutoka kwenye matibabu alikuta nyumba yake imeuzwa na kulazimika kwenda kupanga.

Chanzo: Mwananchi
Kuweni makini makini na hati zenu za nyumba.. wanawake huwa hawawazi kesho, wanawaza Leo tuu kama kuna solution ya kukopa au kuuza Mali kusolve tatizo la Mda mfupi kwao huwa ni rahisi kuuza kuliko kuvumilia..

Lakini pia labda aliuza kwaajili ya matibabu ya mzee..
 
Omba Mungu yasikukute.
Kuna mtu alioneshwa mpaka kaburi hewa akatoa hela kesho anapeleka tofali anaambiwa mbona hapa hapajauzwa.keshatapeliwa.
Mke anauzaje nyumba ya mume wake ama nyumba ya pamoja?

Nyumba sio nyanya iuzwe bila mashahidi wala majirani
 
Kama umesha conclude kwamba KAJINYONGA uchunguzi unaendelea wa nini ????

Aseme uchunguzi unaendelea kuthibitisha kweli kajinyonga. You have no freaking clue kwamba kajinyonga. Una waste government resources kuchunguza kwa nini kajinyonga, ili iweje, umkamate aliyemkera ????

Third world police, incompetent, untrained, unaccountable pinheads. Waziri Simbachamwene kasema polisi anafaa ambae hajaenda shule. Ili waweze kuwatumia kulinda tabaka tawala, kupora na kuua wafanyabiashara.
 
Vitu vyote hivyo vinauzwa mzee taarifa hata kutoka kwa watoto hana duh
Ila kama mzee alikua kauzu watoto wakawa upande wa mama yao balaa ndio hili sasa
Mauaji ss ni kila pembe nchi hii
 
Kama umesha conclude kwamba KAJINYONGA uchunguzi unaendelea wa nini ????

Angepaswa aseme uchunguzi unaendelea kuthibitisha kama kweli kajinyonga. You have no freaking clue kwamba kajinyonga. Una waste government resources kuchunguza kwa nini kajinyonga ili iweje, umkamate aliyemkasirisha ????

Third world police, incompetent, untrained, unaccountable pinheads.
Ha ha ha!
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom