Moshi: Mstaafu wa Polisi ajinyonga baada ya mke wake kuuza nyumba na mali nyingine

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Mstaafu wa jeshi la polisi wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro bwana Omary Msangi amejinyonga hadi kufa baada ya kwenda kutibiwa jijini Dares salaam na aliporudi akakuta mke wake ameuza kila kitu ikiwemo nyumba na mashamba hivyo kulazimika kwenda kuanza maisha ya kupanga nyumba.

----
Mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Omary Charema Msangi amejiua kwa kujinyonga bafuni kwake kwa kutumia waya wa pasi.

Tukio la kujinyonga mstaafu huyo limetokea usiku wa kuamkia jana akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi ambapo mwili wa mstaafu huyo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio leo Jumatano Januari 26, 2022 akisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kujinyonga kwa mstaafu huyo.

"Ni kweli hili tukio limetokea na tunafuatilia kujua hasa chanzo cha kujinyonga kwake," amesema Kamanda Maigwa

Taarifa za chanzo cha kijinyonga kwa askari huyo kutoka kwa mmoja wa ndugu wa familia hiyo zinadai kuwa wakati mwanaume huyo akiwa kwenye matibabu mkoani Dar es salaam, mke wake alitumia nafasi hiyo kuuza mali zake zote ikiwa ni nyumba, mashamba pamoja na mali nyingine.

Inadaiwa kuwa baada ya mstaafu huyo kurejea nyumbani kutoka kwenye matibabu alikuta nyumba yake imeuzwa na kulazimika kwenda kupanga.

Chanzo: Mwananchi
 
Mstaafu wa jeshi la polisi wilayani Mwanga mkoa wa Kilimanjaro bwana Omary Msangi amejinyonga hadi kufa baada ya kwenda kutibiwa jijini Dares salaam na aliporudi akakuta ameuza kila kitu ikiwemo nyumba na mashamba hivyo kulazimika kwenda kuanza maisha ya kupanga nyumba.

----
Mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Omary Charema Msangi amejiua kwa kujinyonga bafuni kwake kwa kutumia waya wa pasi.

Tukio la kujinyonga mstaafu huyo limetokea usiku wa kuamkia jana akiwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kiboriloni Manispaa ya Moshi ambapo mwili wa mstaafu huyo ulichukuliwa na kupelekwa kuhifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya KCMC.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa tukio leo Jumatano Januari 26, 2022 akisema bado wanaendelea na uchunguzi wa kubaini chanzo cha kujinyonga kwa mstaafu huyo.

"Ni kweli hili tukio limetokea na tunafuatilia kujua hasa chanzo cha kujinyonga kwake," amesema Kamanda Maigwa

Taarifa za chanzo cha kijinyonga kwa askari huyo kutoka kwa mmoja wa ndugu wa familia hiyo zinadai kuwa wakati mwanaume huyo akiwa kwenye matibabu mkoani Dar es salaam, mke wake alitumia nafasi hiyo kuuza mali zake zote ikiwa ni nyumba, mashamba pamoja na mali nyingine.

Inadaiwa kuwa baada ya mstaafu huyo kurejea nyumbani kutoka kwenye matibabu alikuta nyumba yake imeuzwa na kulazimika kwenda kupanga.

Chanzo: Mwananchi
Nyumba ya wanandoa yauzika kirahisi hivyo? There is more into this story!
 
Back
Top Bottom