Hueleweki, Kwanza Machame sio Moshi, Huko ni Hai! Labda unazungumzia mji wa Boma/kwasadala hapajakua, maana ndio town ya wamachame hiyo, kam ilivyo Himo/Njia panda kwa Wamarangu! Moshi mjini ya wa WAKIBOSHO, WAURU, OLDMOSHI... Hao ndio wamepakana na moshi mjini.
Huko kwenu Hai, tatizo ni Mbowe.....Anatorosha mabilioni nje badala ya kujenga huko.. Nasikia kuna viwanja alikuwa navyo moshi mjini hajaviendeleza, wanavichukua wenyewe......
Ebu mleta mada jisome hapa alafu tukuulize tena unaishi Nairobi au Mwanza??
Alafu mambo ya kutaja majina ya watu na kujisingizia una uhusiano nao sio sawa, watu tutafikiri watu wengine kabisa ambao tunawajua.. Mpwa wa Ment anayeishi Nairobi namfahamu na wala hana huu upuuzi, wewe labda utakuwa mkata majani wake pale kwao Nkuu..
https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/982284-wana-jamiiforums-mwanza-tukutane.html
Hawa wagogo wakishavuta bange za Dodoma wanajiona ni Wachagga ati..
Huu Mji haukui kabisa yani vilevile nilivyo Ondoka Miaka Mitano iliyopita inauma sana sijui nani kikwazo.Na huku Machame pia ndo vilevile jamani kunanukia ndizi tu.
Xmass iishe minirudi Nairobi.
Nilivyomuelewa mtoa mada ni kuwa Moshi ilipaswa kuwa imepiga hatua kubwa zaidi kimaendeleo ya kiuchumi,maendeleo ya upatikanaji wa huduma bora zaidi za kijamii na maendeleo ya walio wengi na sio wachache. Maendeleo sio barabara na mazingira yaliyo kijani au magari,watu wetu wanafanya nini kuwaingizia kipato chao? Huduma za kijamii zikoje na hapa sizungumzii uwepo wa Hospitali,ubora na aina ya huduma zinazopatikana zikoje? Binafsi hata shule tulizosoma tuliotoka huko tumeshindwa kuziboresha,lakini pia tuna vijana wengi tu ambao hawana ajira bado hatujazungumzia kiwango cha wanaume watu watu wazima ambao wamekuwa walevi wa kupindukia huko vijijini. Afya za watu zinadorora kila siku,sio wale wazee ulikuwa unaenda unakuta wako mashambani wanafanya kazi zao kwa bidii.
Mi nafikiri tujitafakari,je tunaweza kuwa sehemu ya kasi zaidi ya mabadiliko kwa mji wetu wa Moshi, tujiulize tu kwa nia ya kujenga na sio kujibu kwa kuwa mtoa mada ametoa maoni. Kwa nini tupo tulipo,nini tunaweza fanya kuwasaidia watu wetu kule Moshi na sio familia zetu tu? Wengi ni wakulima,ukifika Moshi utagundua climate change is real,joto sana na ile hali ya hewa imebadilika,tunafanya nini? Elimu na hospitali zetu,nini tunaweza fanya?
Nimetizama mchango wa mtoa mada kwa namna hii na naheshimu maoni ya kila mtu. Ninachowaza ni kuwa tunaweza kufanya zaidi na kuipeleka Moshi mbali zaidi. Nilikuwa hapo siku si nyingi kwa mapumziko,na kweli nilitamani kukutana na vijana na kuzungumza nao ila wakati na majukumu haukuruhusu.Nachoona kinabaki kilivyokuwa ni majengo na makanisa ila hali za watu sio kama huko nyuma. Siku njema.
Moshi Hakuna Mall kabisa nimekuja mjini kutafuta mahiyaji ya familia nimeteseka sana hadi wakenya wananishangaa mji ambao mlima mkubwa uko Africa dah nimepata aibu sana
Ebu mleta mada jisome hapa alafu tukuulize tena unaishi Nairobi au Mwanza??
Alafu mambo ya kutaja majina ya watu na kujisingizia una uhusiano nao sio sawa, watu tutafikiri watu wengine kabisa ambao tunawajua.. Mpwa wa Ment anayeishi Nairobi namfahamu na wala hana huu upuuzi, wewe labda utakuwa mkata majani wake pale kwao Nkuu..
https://www.jamiiforums.com/jf-chit-chat/982284-wana-jamiiforums-mwanza-tukutane.html
hawana tofauti na watu wa kibaha, kisarawe, mkuranga, wanaosema "nipo dar"!!
Nipo hapa kijijini sambarai naenjoy h+ kama nipo Kisumu vile.mwaka jana nilivyoondoka sikuacha nertwork nzuri hivi ila sasa naipata,AIKA RUWA MATENGERA👏👏👏👏👏👏👏👏👏👏
Karibu sana bossEnjoy life mkuu nyumbani hapo tarehe 24 ntakuwepo hapo.
Karibu sana boss