Moshi: International School of UWCEA yasitisha masomo Baada ya Wanafunzi 2 kupatwa na Corona

Hayo masuala ya huko hospitalini mkuu ngoja na mie kwamba pale muhimbili kuna kipindi ilikuwa walinzi hawaruhusu mtu kuingia pale getini bila barakoa ila sasa unapita tu uvae au usivae,na kule ndani kuna baadhi ya sehemu ikuwa hauingii bila barakoa ila sasa unaingia bila barakoa. Je hiyo ina maana gani kwako?

Ndio maana nakwambia humu kila mtu anaongea lake,wewe unasema hawapimi corona huko hospitali kwamba mtu akifa na kushindwa kujua sababu ya kifo wanasema ni matatizo ya kupumua ila wengine wanasema huko hospitali corona wanapima wagonjwa.
Kwahiyo unaamini kabisa hakuna mtu aliyekufa kwa Corona tokea tutangaziwe Corona imeisha?
Unadhani wizara kweli haina Takwimu za wanaopimwa?
 
Eti uwoga ni ugonjwa mkubwa kuliko ugonjwa wenyewe, hata takwimu toeni tu, mbona matangazo ya HIV yalikuwa yanasisitizwa kuwafanya watu wahabarike na wachukue hatua leo matangazo ni ugonjwa, ni kwatia watu hofu, inatakiwa tufikiri upya, hasira ni kali ukihisi mpedwa wako kaondoka kwa sababu ya Covid-19 na mtu anatangaza kuwa hatuna tatizo hilo, duniani Nchi usifiwa kwa mambo yake mazuri lakini hadi sasa sijaona sifa nzuri tuliopata kwa kuficha takwimu, kuacha kuvaa masks, wala kutochokua juhudi za kupata kinga, ni hatari siasa kuchanganya na utaalam, au kutafuta sifa baadhi wakiangamia, binadamu wote ukosea ila uharibu unapochanganya na kiburi, dharau, kujiona!
Hofu ni tatizo kweli,kuna watu walikimbia dar na familia zao wakaenda mikoani kisa kuogopa corona. Nina rafiki yangu alikuwa hataki kurudi Dar kwa kuogopa corona et hospitali zimejaa wagonjwa wa corona. Kuna kipindi hadi huko hospitali unaweza kukosa kuhudumiwa wauguzi walikuwa wanaogopa waoga,huko karantini watu wananyanyapaliwa.
 
Na hata hivyo, bila kupepesa macho, ni lazima tuseme Asante Mungu, maana kipindi kile cha wimbi la maambukizi ya awali, Tumekuwa salama Sana nchini tofauti na wenzetu, na hata sasa, Ishini Kwa Imani hiyohiyo inawezekana tena Mungu kutuvusha, ondoeni hofu huku tukichukua tahadhari zote za kujikinga maana serikali haijazuia watu kuchukua hatua za kujikinga na korona
Kinacho kufanya kuwa na uhakika kuwa tuliishi salama zaidi ni takwimu tu za kweli, sio maneno ya jukwaani huku watu wanaangamia, kama hauna takwimu hauwezi jigamba dhidi ya wenzako tena wenye takwimu!
 
Kwahiyo unaamini kabisa hakuna mtu aliyekufa kwa Corona tokea tutangaziwe Corona imeisha?
Unadhani wizara kweli haina Takwimu za wanaopimwa?
Mie nina mtazamo wangu tofauti,sipo kwenye kundi la watu wanaoamini corona imeisha Tz wala wale wanaoamini ipo na inauwa sana watu,kwa upande wangu naona kuna vitu havijaeleweka kwenye hili janga la corona hata kipindi kile serikali inatoa takwimu bado nilikuwa naona kuna vitu haviko sawa.
Watu hawatafakari zaidi kwanini kipindi ambacho ilikuwa inaonekana corona inazidi ndio kipindi akaanza kuacha kutoa takwimu na kuacha kupima na hadi mwishoni akafikia kuthubutu kabisa kusema corona imeisha.

Kwahiyo kama corona ilikuwepo toka mwanzo siwezi kusema haipo wakati hakuna kilichofanyaki kuiondoa,tatizo ni uhalisia wa huu ugonjwa wenyewe na ndio sababu ya kubishana hapa kuwa upo mara haupo.
 
Mie nina mtazamo wangu tofauti,sipo kwenye kundi la watu wanaoamini corona imeisha Tz wala wale wanaoamini ipo na inauwa sana watu,kwa upande wangu naona kuna vitu havijaeleweka kwenye hili janga la corona hata kipindi kile serikali inatoa takwimu bado nilikuwa naona kuna vitu haviko sawa.
Watu hawatafakari zaidi kwanini kipindi ambacho ilikuwa inaonekana corona inazidi ndio kipindi akaanza kuacha kutoa takwimu na kuacha kupima na hadi mwishoni akafikia kuthubutu kabisa kusema corona imeisha.

Kwahiyo kama corona ilikuwepo toka mwanzo siwezi kusema haipo wakati hakuna kilichofanyaki kuiondoa,tatizo ni uhalisia wa huu ugonjwa wenyewe na ndio sababu ya kubishana hapa kuwa upo mara haupo.
Nifafanulie hapo unaposema tatizo ni uhalisia wa huu ugonjwa!
 
Mkuu jinsi watu wanavyoichukulia corona unadhani ni sawa uhalisia wa corona yenyewe?
Dunia nzima inazungumzia corona na kusema ni ugonjwa na mambo mengi yamevurugika kwa sababu ya corona,lakini wakati huo huo tunaambiwa wanaopata huu ugonjwa na kupona ni wengi kuliko wanaokufa kwa maana vifo vya corona ni vichache tofauti na ugonjwa kama Ebola. Na pengine ndio sababu insyofanya watanzania kuamini hakuna corona Tz kwa sababu laiti corona ingekuwa inapukutisha watu basi kusingekuwa na huku kuamini kwamba hakuna corona.

Je, unafikiri kwanini sasa corona imekuwa ikionekana ni ugonjwa hatari sana?
Hayo mataifa ya Ulaya, Asia na Marekani wanavyoichukulia Corona ni sawa kwa maana husumbuliwa sana na magonjwa ya aina hiyo kama influenza, inawezekana ni biolojia ya miili yao na hali ya hewa.

Corona imeonekana ni ugonjwa hatari kwa sababu

1. Kutokana na nchi ulizoanzia, kwa kua wao ndio wenye vyombo vya habari vikubwa na kuendesha uchumi wa dunia, kama ungeanzia Afrika ungetangazwa kwenye habari zao mara moja moja tena kwa habari fupi tu na ingewezekana wangetutenga kabisa, hamna mtu kwenda kwao wala wao kuingia huku hovyo hovyo.

2. Corona haiui kila mtu anayeupata ila inasamabazwa kiurahisi kwa watu wengi ndani ya muda mfupi kuliko magonjwa kama Ebola na hata yale mafua ya ndege (H5N1), hii ni kwa sababu hata mtu asiyekuwa na dalili anaweza kuueneza kwa njia ya hewa bila kujia wakati hayo magonjwa mengine huenezwa pale ambapo virusi vinakuwa vimeushambulia sana mwili na mara nyingi mgonjwa huwa mahututi na hawezi kuzunguka na kuusambaza kwa urahisi.

Afrika ni nchi chache zinazoweza kukabiliana na Corona kwa uhakika kutokana na hali duni ya kiuchumi, kwa mfano Kenya tangu wanapambana na Corona wameripoti vifo 1736 , hiyo ni karibu mwaka sasa, na ndani ya mwaka huo huo wana wastani ya vifo
10,700 vinavyotokana na Maralia, jiulize bado magonjwa mengine kama TB, homa ya ini. Inawezekana nguvu kubwa ingewekwa kwenye haya magonjwa yetu ingeokoa uhai wa watu wengi zaidi kuliko tu kuhangaika na ugonjwa mmoja.

Jiulize kwa nini ukienda kukaa huko Ulaya watakuambia uonyeshe kama una chanjo mara ya Yellow Fever, upimwe TB na mengineyo lakini kamwe hawakuambii uonyeshe ama upewe chanjo ya Influenza zinazowasumbua, wakati wao kila mwaka wanapeana chanjo za influenza ili kujilinda na wala hawajali kama tutazibeba hizo influenza na kuzileta kwetu ila hawataki haya magonjwa yetu makali yawafikie kwa namna yoyote maana walishayadhibiti siku nyingi.

Ni ngumu kuamini kwamba corona haipo kabisa Tanzania kutokana na muingiliano tulionao na mataifa yenye maambukizi makubwa ya Corona, hakuna haja ya kuanza kuweka watu lockdown ama quarantine na kufanya mass testing, hiyo muda wake umeshapita na gharama ni kubwa ila ni bora tu tungeambiwa ukweli ugonjwa upo na kukumbushana kuchukua tahadhari, ikiwapo hata mtu ukijiona hali si nzuri ni bora ajitenge mwenyewe kwa muda, apige dawa zetu asili ili usiusambaze kwa wengine. Sasa hivi kuna watu wanaona aibu hata kuvaa barakoa na wanazo ndani huku wana matatizo lukuki ya presha, sukari n.k. ambayo yanaweza kuwa hatarishi endapo watapata maambukizi.
 
Ukiondoa Ujinga naotaka kukupanda! Kwako wewe unataka nini juu ya Corona?

Kwamba uwekwe lockdown au uje unawishwe mikono na kuvalishwa barakoa siyo?

Nataka kuwepo na taarifa ya ugonjwa huo ili watu wajikinge zaidi. Kunawa na kuvaa barakoa ni hatua t dhidi ya huo ugonjwa.
 
si ndicho mnachokitaka.
Maana wenzenu wanaoishi maisha ya kukaa ndani mnaona wanafaidi mnataka na nyie mjionee.
Mmeambiwa Corona hamnaa
Lakini mnazidi kuyatafuta na mtayapata muda si mrefu
Lockdown ni moja ya hatua dhidi ya Corona, na kuwepo kwa corona ni jambo jingine.
 
Serikali isiigie kwenye mtego wa kuchukua chanjo ya korona, bado ipo kwenye majaribio maana ni teknolojia mpya ya uzalishaji wa chanjo inayohusisha kuingiza vinasaba vinavyotokana na virus kwenye vinasaba vilivyo ndani ya seli hai za binadamu. Imeshaleta madhara ya allergy na vifo kwa baadhi ya watu waliochanjwa.
Umewaona waliokufa au na wewe unamaabara yako,, chanjo zingine mnazikubali ila zingine mnakataa,,, hamna chochote mnachoweza nyinyi zaidi ya kumwomba Mungu tu,, geographical yetu ya mazingira machafu inatubeba, manakula chakula kinyesi kipo karibu,, mimoshi tunayovuta tutafikiri wote tunavuta sigara,,
 
si ndicho mnachokitaka.
Maana wenzenu wanaoishi maisha ya kukaa ndani mnaona wanafaidi mnataka na nyie mjionee.
Mmeambiwa Corona hamnaa
Lakini mnazidi kuyatafuta na mtayapata muda si mrefu

Huna unaloongea zaidi ya kupiga Siasa mfu hapa jukwaani. Kukaa lockdown ni maamuzi, na kutangaza kuwa ugonjwa upo ni jambo jingine. Hata sasa ugonjwa upo lakini tunaendelea na shughuli zetu huku kukiwa na tahadhari kidogo sana. Unamtishia nani kwamba tunachokitafuta tutakipata? Nahisi umeishiwa na hoja ndio maana unaokoteza vitisho vya kipuuzi.
 
Back
Top Bottom