Moshi: Afungua kesi kuzuia kadi na michango ya harusi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,372
8,108
Mfanyabiashara maarufu wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, James Mushi amefungua maombi madogo akiiomba Mahakama ya Wilaya hiyo itoe zuio la kusitisha usambazaji wa kadi na michango ya harusi ya mtu anayedaiwa kutumia jila lake na familia yake kuchangisha michango hiyo.

Akiwasilisha maombi hayo jana Jumatano Septemba 28, 2022, wakili wa mfanyabiashara huyo, Elia Kiwia, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo, Julieth Mawole alidai mteja wake huyo ameingia kwenye mgogoro mkubwa na familia yake na kutishia ndoa yake kuvunjika baada ya mke wake kumtuhumu mumewe kuwa ni mzinifu.

"Kati ya tarehe 16 na 20, mwaka 2022 mteja wangu alipata taarifa kuwa katika eneo la Boma ng'ombe, Machame na Arusha kuna mtu alitengeneza kadi kwa ajili ya michango ya harusi na kusambaza kadi hizo za mchango wa harusi kwa kutumia jina lake yeye na mke wake bila yeye kushirikishwa," alisema

"Mheshimiwa kitendo hicho cha mtu huyo kutumia jina la mlalamikaji yeye na familia yake imesababisha mgogoro mkubwa kwenye ndoa na kuhatarisha ndoa yake kuvunjika.

“Ambapo mke wake mlalamikaji amemchukulia mume wake kama mtu mzinifu mwenye watoto nje ya ndoa kwa kumuingiza kwenye michango bila ridhaa yake" alieleza wakili Kiwia

"Fedha hizo mlalamikaji hajui kama zinatumika kwa njia gani na kwamba hana uhakika kama fedha hizo zinazokusanywa kwa kutapeli au anadanganya kwa njia ya kujipatia fedha jambo ambalo aliona na yeye linaweza kumletea shida na familia yake".

"Huyu bwana James na familia yake wanashindwa kuelewa hizo fedha ni za nini na kwamba ni uwezekano wa matapeli wanakusanya fedha kwa kutumia jina lake ambao mwisho wa siku wanaweza kukamatwa yeye na mke wake kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na wanaweza kufungwa."

"Kwa hiyo tumekuja hapa kuomba kadi hizi zisiendelee kusambazwa na huyu anayelalamikiwa pamoja na watu wengine wanne ambao majina yao yako ndani ya kadi hii".

Hata hivyo, hakimu Mawole alitoa zuio usambazwaji wa kadi hizo pamoja na michango hiyo mpaka hapo kesi itakapotajwa Oktoba 19.

Akizungumza nje ya mahakama, mfanyabiashara huyo, Mushi alisema baada ya kupata taarifa zimechapishwa na kusambazwa mtaani alifanya jitihada za kupata kadi hizo katika meneo mbalimbali na kukuta zimeandikwa jina lake.

"Wakati kadi hizi zikiwa zinaendela kusambazwa maeneo mbalimbali iliniletea shida na familia yangu ambapo mke wangu aliniuliza inakuwaje natengeneza kadi za michango ya harusi bila kumshirikisha yeye ndipo akaanza kunituhumu nina watoto nje ya ndoa na hii imeleta shida kwenye ndoa yangu na jamii kwa watu ambao wananifahamu".

"Kwenye ile kadi kulikuwa na majina ya watu watano ambao mimi siwafahamu na wala sikuwahi kukaa kikao chochote na wao kupanga mchango au kitu chochote, kwa kuwa kitendo hiki niliona kinaniletea madhara katika familia ikabidi nimtafute wakili wangu ili tujue ni kwanini hawa watu wanafanya hivi."

MWANANCHI
 
Ndoa ndoano, Ila bado Ushamba mwingi michango ya harusi.
 
Mimi nilidhani hilo shauri la hiyo kesi ya kusitisha michango ya harusi linahusu harusi zote nchini ili nipate unafuu. Maana hapa nilipo nina vimeo vya kutosha tu. Yaani kwa mtu mwingine ni mtaji kabisa wa biashara!

Mbaya zaidi kwenye hivyo vimeo vinavyofikia sita mpaka sasa; viwili nipo kwenye kamati!!
 
Back
Top Bottom