Morogoro: Kakakuona atabiri neema. DC awataka wakulima wafuate sheria za kilimo

Prisonerx

JF-Expert Member
Jun 30, 2020
540
1,000
Wangemuwekea chupa ya COVIDOL or NIMCAF na hakika angezikimbilia na hiyo ingekuwa ni tafasiri ya kukubwa na janga la corona
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
55,462
2,000
Katika dunia hii ya sayansi bado kuna misukule inaamini hawa wadudu eti wanaleta neema .DC mzima na kadegree kake ametoka ofisini anakimbilia kumuona mdudu eti atabiri na kuacha wanasayansi wenye utafiti


USSR
Huyu ana amini
Etwege

Ova
 

Krav Maga

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
4,625
2,000
KAKAKUONA AONEKANA MVOMERO ATABIRI NEEMA

Mnyama Kakakuona ameonekana Wami Sokoine, Wilaya ya Mvomero ambapo Viongozi wa Kimila na Kidini walimtumia ili aweze kutabiri hali ya mwaka huu.

Walimuwekea zana za kimila, zana za umeme na vifaa vingine ambapo alipita kati ya unga na maziwa hali iliyoonekana kuwa ishara ya neema kwa mwaka 2021.

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Albinus Mgonya amesema, mbali na imani kuwa msimu utakuwa mzuri, amewataka Wananchi wazingatie kilimo bora kwa kuzingatia Sheria za Kilimo.

Nami All - Rounder nawakumbusheni hata mwaka juzi alionekana Mikoa ya Nyanda za Kati tukaambiwa kuna neema ila kukawa na Msoto tupu tu.

Taarifa: aboodmediatz
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom