Morogoro Enzi Hizo: Hii ndio Morogoro bwana!

Morogoro Enzi Hizo: Hii ndio Morogoro bwana!

Ila sikunyingi sana nilitoka kuja kurudi ajajajajajajajajajajaj magorofa ni hatari tofauti na miaka hiyo nilishangaa sana kumenoga mno Moro


Cc Smart911
Moro ilikua ndogo san kipindi kile sasa hivi pamebadilika sana mm mwenyewe nilienda Mwere pale nikakuta vigae wametoa wamepiga bati ambapo zaman madirisha yalikua ya vioo na vigae juu
 
Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma kidogo ya miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni... Hii town ya wajanja , vijana wanaojua kuvaa,wenye exposure, wapenda burudani na utafutaji... Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa... Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill na Kigurunyembe ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa kishua na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto wa kihuni... Mitaa maarufu ilikuwa ya kishua ni Forest, Liti, Sua na Rock garden... Mitaa maarufu ya ushenzini kulikuwa na Mji mpya, Kichangani, Mafiga.

Watu wa Moro ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka.... Kulikuwa na timu ya mji maarufu Reli kiboko ya vigogo hii ilikuwa daraja la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki.. Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa kuitwa Ya mungu ambae ndio shabiki wa kwanza mtanzania kujichora mwilini... Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica, kulikuwa na Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari.

Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel na Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill... Hapa kuna mtu anaitwa Dj Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga ndio alomfundisha Udijei John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu.. Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja Dj Joseph Kusaga akimfundisha kazi Dj Peter Moe.

Watu wa Moro najua mpo wengi umu Jf naomba tukumbashane mawili matatu matukio, maujanja na mazuri ya Moro Town.

Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe.. Kulikuwa na watemi wa mji kina Slim mtoto wa sheikh mkuu, Matata, Gamba mcheza judo, vijana wa siafu toka mji mpya nk

Unaikumbuka Miss Morogoro? Unamkumbuka Alex Nictas?

Unawakumbuka mabingwa wa kudansi kitaifa? Kina Askofu, Bob Tigger, Super Ngedere nk

Unakumbuka mashindano ya magari? Unawakumbuka wakimbiza magari maarufu kina Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos nk

Unakumbuka wagiriki na bata zao kwa Mama Perina na Acropol? Unakumbuka masista duu na mabraza meni wa mitaa ya Forest?

Unakumbuka enzi za Mnet inaingia mjini? Moro mji wote ulikuwa na access ya kuona dstv bure.

Unakumbuka heka heka za ligi za mbuzi uwanja wa shujaa, makaburini kilakara na kikundi?

Unakumbuka Fete Fete? Unakumbuka Shan cinema? Unakumbuka swimming pool ya rock garden?

Unamkumbuka Mzee Mkwidu na Patel wakuu wa shule maarufu KG & Forest?

Unamkumbuka Maneno Big G rip? Unamkumbuka Mnambo wauza ngada maarufu?

Unamkumbuka Ndanje jambazi aliyetikisa mji? Unakumbuka ishu yake ya silaha na February Ma rope?

Unamkumbuka toz wa kipindi hicho Puzzo na kundi lake la kurap Watukutu akiwa na Sallam meneja wa Diamond sasa hivi? Unawakumbuka Gangster Family? Unawakumbuka Ze domp?

Unamkumbuka Achimpota? Unaikumbuka bus la Chambo?

Unakumbuka ule upepo uliokuja wa watu kuzamia Sauz na ulaya?

Umeishi mtaa gani Mafisa, Msufini, Kilakara, Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma road, Sua, Vibandani, Relwe magorofani, Kigurunyembe, Madizini? Au wapi Umeishi?

Kuna watu maarufu wengi sana DSM ambao maujanja yao wamejifunzia Moro Town... Hakika Morogoro ni jiji kasoro bahari.

WATOTO WA MOROGORO MIKONO JUU.
Ukiiongelea moro moyo wangu huwa wafarijika sana ni mji mtamu sana kimaisha.umeelezea fresh kbs hiyo timu ya reli ilikuwa krb na hom xo mechi zote ni free.mbali na hiyo mapopo wa wazee wa disko wacha kbsaa.
 
Namjua huyo mwalimu, itakuwa ile karibu na ule mti uliosimama miaka ile kwa Mzee maarufu sheik .........
hahaaa mkuu wapazungumzia michumvini daaahh mti ulisimama baada yakuanguka watu walijazna kbao nakumbuka nilikuwa Mdogo aisee ..halima kihemba alikuja kufuatilia ile habari
nikweli mwalimu alikuwa anaishi area zile Zile ...daaahh sasa hvi pame badilika kbisaaaa
 
hahaaa mkuu wapazungumzia michumvini daaahh mti ulisimama baada yakuanguka watu walijazna kbao nakumbuka nilikuwa Mdogo aisee ..halima kihemba alikuja kufuatilia ile habari
nikweli mwalimu alikuwa anaishi area zile Zile
...daaahh sasa hvi pame badilika kbisaaaa

Hiyo wahenga tuuu ndiyo tunajua hiyo hbr, nilikwenda kuona ule mti aiseee.Miaka ile daladala moja tuu.
 
Masika mtaa wa wajanja ndo nlikozaliwa shule ya msingi mwere, sikukuu fete fete na mango garden ndo maeneo yakujidai. Mnambo alikuwa bonge la brother men enzi hiyo. Kiukweli Moro imebadilika lakini bado panavutia
 
Moro wote vibwengo tu japo nimepatiako mke aliyemrithi mke wangu wa ndoa.
 
Masika mtaa wa wajanja ndo nlikozaliwa shule ya msingi mwere, sikukuu fete fete na mango garden ndo maeneo yakujidai. Mnambo alikuwa bonge la brother men enzi hiyo. Kiukweli Moro imebadilika lakini bado panavutia
ww mwere mwaka gani ulimaliza maana naona wengi kumbe tumesoma mwere humu
 
Umemtaja hapo huyo Mshambuliaji hatari sana wa zamani wa Reli ya Morogoro na Simba Sports Club David Mihambo ambaye kwa sasa yupo zake Mbezi Beach Makonde na hataki hata kusikia suala la Mpira wa Kibongo ( Kitanzania ) kwani anasema hakuna jambo ambalo lilimuuma kama yule ' Baniani ' mmoja alivyowaahidi kuwapa kila Mchezaji Gari aina ya KIA halafu hapo hapo tena usiku akaenda kuwahujumu Wachezaji akina Hussein Marsha, Mohamed Mwameja, George Lucas Gazza na George Magere Masatu na wakafungwa ' Kizembe ' sana Shamba la Bibi Taifa na kukosa Kombe na Zawadi hizo.
 
Kwa father kanuti kulikuwa na mtu anaitwa Chai bado.alikuwa mbabe balaa.
 
Aisee umenikumbusha mbali sana....me nimemaliza A level pale Forest Hill..08'...enzi zile Moro ilikia Moro kweli...
 
Back
Top Bottom