Morogoro Enzi Hizo: Hii ndio Morogoro bwana!

Morogoro Enzi Hizo: Hii ndio Morogoro bwana!

Umemtaja hapo huyo Mshambuliaji hatari sana wa zamani wa Reli ya Morogoro na Simba Sports Club David Mihambo ambaye kwa sasa yupo zake Mbezi Beach Makonde na hataki hata kusikia suala la Mpira wa Kibongo ( Kitanzania ) kwani anasema hakuna jambo ambalo lilimuuma kama yule ' Baniani ' mmoja alivyowaahidi kuwapa kila Mchezaji Gari aina ya KIA halafu hapo hapo tena usiku akaenda kuwahujumu Wachezaji akina Hussein Marsha, Mohamed Mwameja, George Lucas Gazza na George Magere Masatu na wakafungwa ' Kizembe ' sana Shamba la Bibi Taifa na kukosa Kombe na Zawadi hizo.
Asilimia kubwa mpira wa kibongo umejaa fitina
 
Mz
Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma kidogo ya miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni. Hii town ya wajanja, vijana wanaojua kuvaa, wenye exposure, wapenda burudani na utafutaji. Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa. Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill na Kigurunyembe ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa kishua na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto wa kihuni. Mitaa maarufu ilikuwa ya kishua ni Forest, Liti, Sua na Rock Garden. Mitaa maarufu ya ushenzini kulikuwa na Mji mpya, Kichangani, Mafiga.

Watu wa Moro ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka. Kulikuwa na timu ya mji maarufu Reli kiboko ya vigogo hii ilikuwa daraja la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki. Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa kuitwa ya Mungu ambae ndio shabiki wa kwanza Mtanzania kujichora mwilini. Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica, kulikuwa na Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari.

Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel na Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill. Hapa kuna mtu anaitwa DJ Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga ndio alomfundisha Udijei John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu. Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja DJ Joseph Kusaga akimfundisha kazi DJ Peter Moe.

Watu wa Moro najua mpo wengi umu Jf naomba tukumbashane mawili matatu matukio, maujanja na mazuri ya Moro Town.

Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe. Kulikuwa na watemi wa mji kina Slim mtoto wa sheikh mkuu, Matata, Gamba mcheza judo, vijana wa siafu toka mji mpya nk

Unaikumbuka Miss Morogoro? Unamkumbuka Alex Nictas?

Unawakumbuka mabingwa wa kudansi kitaifa? Kina Askofu, Bob Tigger, Super Ngedere nk

Unakumbuka mashindano ya magari? Unawakumbuka wakimbiza magari maarufu kina Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos nk

Unakumbuka Wagiriki na bata zao kwa Mama Perina na Acropol? Unakumbuka masista duu na mabraza meni wa mitaa ya Forest?

Unakumbuka enzi za Mnet inaingia mjini? Moro mji wote ulikuwa na access ya kuona dstv bure.

Unakumbuka heka heka za ligi za mbuzi uwanja wa shujaa, makaburini kilakara na kikundi?

Unakumbuka Fete Fete? Unakumbuka Shan cinema? Unakumbuka swimming pool ya rock garden?

Unamkumbuka Mzee Mkwidu na Patel wakuu wa shule maarufu KG & Forest?

Unamkumbuka Maneno Big G rip? Unamkumbuka Mnambo wauza ngada maarufu?

Unamkumbuka Ndanje, jambazi aliyetikisa mji? Unakumbuka ishu yake ya silaha na February Ma rope?

Unamkumbuka toz wa kipindi hicho Puzzo na kundi lake la kurap Watukutu akiwa na Sallam meneja wa Diamond sasa hivi? Unawakumbuka Gangster Family? Unawakumbuka Ze Domp?

Unamkumbuka Achimpota? Unaikumbuka bus la Chambo?

Unakumbuka ule upepo uliokuja wa watu kuzamia Sauz na ulaya?

Umeishi mtaa gani Mafisa, Msufini, Kilakara, Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma road, Sua, Vibandani, Relwe magorofani, Kigurunyembe, Madizini? Au wapi Umeishi?

Kuna watu maarufu wengi sana DSM ambao maujanja yao wamejifunzia Moro Town. Hakika Morogoro ni jiji kasoro bahari.

WATOTO WA MOROGORO MIKONO JUU.
Mzee mkwidu amefariki mwezi huu
 
Mji wa kipumbavu ikifika sana 1 na nusu usiku watu waahalala mjini kweupeee
 
Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa akiitwa "Ya mungu" ambae ndio shabiki wa kwanza mtanzania kujichora mwilini rangi nini na kubakisha macho na bukta yake tu.... hiyo RELI ilikuwa na watu kweli.... golini.... DUNCAN MWAMBA - Kipa wa Machejo... ATHUMANI MSOMALI kipa mrefuuuu... Bakari Tutu, James Charles, Madundo Mtambo... Juma Salum kati kati.... Boniface Njohole, Mwanamtwa Kihwelo, Ramadhani Chilambo, Peter Mjata... daaah... gone those days
 
Yes Salute Morogoro, nakumbuka Kigurunyembe CNE kilikua mfano bora wa usafi wa hali ya juu, inasemekana hata president wa awamu ya kwanza alipenda sana kulala pale, kweli crocodile 🐊 ni tofauti kabisa na lizard 🦎, Leo ni uchafu mkubwa pale, hooooo Tungi kule na mmmm na 602 pale weee, good memories za mji na mkoa kwa ujumla, kwa sasa mmmmm, ile T1 ilitakiwa ichepushwe kuanzia Kingirowira hadi pacha ya kwenda sangasanga
 
Acheni utoto. Yaani kabisa nanyi mnakuja zungumzia Morogoro kama ni kitu cha maana katika matukio? Morogoro tuleteeni ndizi, nazi, mchele na matunda tu. Hayo mambo mengine yaachieni Dar, Mbeya, Arusha ndo wanayajua.
 
KITENGA alikuwa sio wa mchezo, nasikia alikamatwa na wamasai baada ya kuiba ng'ombe Melela. Walipiga sana mapanga lakini hakufa, hadi walipotoa hirizi mwilini mwake, pia nasikia polisi walimburuza gari.
Alitokea mzee mmoja akawaambia pigeni kivuli tu,ndio mpaka kifo chake.
 
Nani anamkumbuka Rolling stone? Jamaa mwizi anayejua kingereza cha hatari msafiii, vitu kwake being cheee, soski, mafuta na nk. Na kifo chake je? Ilikiwa gumzo mjini.
Jina lake Marka Kisanga..
Jamaa alikuwa na duka Jirani yetu,alikuwa Bonge la bishoo. Miwani tinted mpaka usiku wa manane. Kama Shwaznigga.

Dukani kwake ikishafika saa mbili usiku hauzi bidhaa za kawaida Kama chumvi,sukari,unga mafuta no, hata Kama zipo, labda upewe bure.Ni pombe kwenda mbele.
Nilikuwa napenda Kila akikaribia kufunga duka Kuna nyimbo "Lala Salama" sio wa "Diamond" itapigwa inajirudia mpaka anafunga duka..

Baada ya kuzinguana na baba mwenye nyumba ikabidi ajenge kiosk kingine upande wa pili wa barabara kikitizamana na duka alilotoka, unaambiwa kimejengwa usiku toka msingi Hadi bati utafikiri kimeota Kama mmea.
Siku taarifa zimekuja Kama jamaa kafa kwenye ambush nilikuwa nasoma Morogoro Sec,istoshe ipo karibu mortuary ya mkoa.
Nyepesi nyepesi, ndugu zake Hadi mama ake mzazi walishindwa kumtambua jinsi alivyokuwa ameanza kuharibika, cha kushangaza mwanamke wake ndio alimtambua, kweli dam sio nzito kuliko Maji.

Watu wakashangaa.
Ikabidi Dada atoe Siri kwamba jamaa akiendaga kwenye ambush kuwa anavaa chupi yake, (ya mwanamke). Na ndicho kilichomfanya amtambue. (Masharti ya mganga sijui).

Mazishi yake Sasa, wahuni ndio ikabidi waongoze ibada, Mana hakuzikwa kikanisa..
Ila jamaa mtaani alikuwa POA SANA..
 
Jina lake Marka Kisanga..
Jamaa alikuwa na duka Jirani yetu,alikuwa Bonge la bishoo. Miwani tinted mpaka usiku wa manane. Kama Shwaznigga.

Dukani kwake ikishafika saa mbili usiku hauzi bidhaa za kawaida Kama chumvi,sukari,unga mafuta no, hata Kama zipo, labda upewe bure.Ni pombe kwenda mbele.
Nilikuwa napenda Kila akikaribia kufunga duka Kuna nyimbo "Lala Salama" sio wa "Diamond" itapigwa inajirudia mpaka anafunga duka..

Baada ya kuzinguana na baba mwenye nyumba ikabidi ajenge kiosk kingine upande wa pili wa barabara kikitizamana na duka alilotoka, unaambiwa kimejengwa usiku toka msingi Hadi bati utafikiri kimeota Kama mmea.
Siku taarifa zimekuja Kama jamaa kafa kwenye ambush nilikuwa nasoma Morogoro Sec,istoshe ipo karibu mortuary ya mkoa.
Nyepesi nyepesi, ndugu zake Hadi mama ake mzazi walishindwa kumtambua jinsi alivyokuwa ameanza kuharibika, cha kushangaza mwanamke wake ndio alimtambua, kweli dam sio nzito kuliko Maji.

Watu wakashangaa.
Ikabidi Dada atoe Siri kwamba jamaa akiendaga kwenye ambush kuwa anavaa chupi yake, (ya mwanamke). Na ndicho kilichomfanya amtambue. (Masharti ya mganga sijui).

Mazishi yake Sasa, wahuni ndio ikabidi waongoze ibada, Mana hakuzikwa kikanisa..
Ila jamaa mtaani alikuwa POA SANA..
Weee kweli unamjua hadi yule mdogo wake V, si eti, mkewe alikuwa mtoto wa mama N yule ticha wa Moro.sec kule F. Nilinunua sana soksi wakati anaduka pale hospital ya mkoa. Si unajua watoto wa hostel mafuta,lotion,zoote kwake.
 
Standard 7 Bungo primary 1995
1996-99 Kigurunyembe Secondary O-level
A-level 2000-2002 Forest Hill Secondary

Sent from my SM-J100H using JamiiForums mobile app
Basi miye kuna siku sikuja na jembe wala kwanja, nikakamatwa na makusi na Dogo nikawekwa airport. Wenyewe wakatimka tulikamatwa km 4 hv tuko form6. Miye nikapewa sweta nikampa jamaa nae akanipa lake nikaenda kule uwanjani bize nalima. Duuh Dogo na makusi walinitafuta siku ile shule nzima walikalili sweta duuh maisha haya acha watoto watudanganye tuu siku hizi nawachora tuu.
 
Back
Top Bottom