Namimi hii hapa, niliishi Moro mwaka 1993/4, Eneo la Mazimbo, kipindi hicho ni Poli tu kuanzia Mazimbu Kanisa Katoliki hadi Daraja la treni Tinge tinge karibu na Kambi ya Wakimbizi ya Mazimbu. Asubuhi Lukobe Shamba, kulima mpunga, jioni kumwagilia bustani za babu pembezoni mwa mto Ngerengere. Nilijifunza kulima miwa, choroko na kuvua Dagaa uduvi. Tukiamka mimi na dada zangu ni kwenda Kupanga foleni ndani ya Kambi za wakimbizi wa South Africa kuchukua mbao za kuni za kupikia nyumbani. Wakati mwingine wasimamizi wa Wakimbizi (UNHR), utufungulia Makontena tuchukue nguo na viatu, tukifika nyumbani tunauza. Mjini kati Moro kwenda mpaka sikukuu, Sisi tulikua wapori pori tu uko Mazimbu.