Morogoro Enzi Hizo: Hii ndio Morogoro bwana!

Mimi ni Mananga (RIP) Product! Msaidizi Mama SUMARI na Mwl. selemani! Ngakuka yupo na FRENCH, pale MATHS alisimama MKAMI, huku BIOS alicheza KUNAMBI, Michezo Mwl. SUKA bila kumsahau Mama NJAMA ktk ENGLISH
Msalimie Kasongo K, under Mananga, au ......
Enzi hizo MORO SEC haijazungushiwa ukuta, pale uwanjani JAMAICA ndio ulikuwa uwanja wao!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waluguru Shule yenu hiyo hapo!
images.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe akili fupi SUA ni chuo cha kilimo eneo inabidi liendelee kuwa kubwa kutokana na future expansion itakapohitajika
Mji huu umejaa wahindi naa waarabu ndo maana hauendelei! watu wanapiga hela kwenye barabara za mjini zinajengwa kila siku hazidumu, kila kona ni ma ccm tu yamejaa. Uchafu umezagaa labda siku hizi kidogo, barabara nyingi zimejaa mashimo kila mwaka mto kikundi unapumua maji yake mtaani hakuna suluhisho.
Japokuwa mji ukipangwa na kujengwa vizuri unaweza kuwa kama New York kutokana na mandhari yake lakini kutokana na wenyeji wake wa kikuguru na ushamba wao wakiuita ujanja huu mji hauwezi kuendelea. Tujifunze hata kamji ka Iringa kalivyo pazuri.
Serikali ipanue mji wa Morogoro kwa kuwanyang'anya SUA na Mzinga na Mzumbe ili watu wajenge majumba tena wapime viwanja vipya wakiwanyang'anya au kuwapunguzia taasisi hizo maeneo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MOROGORO HAPO ZAMANI.

Leo 23:25pm 17/04/2020

Watoto wa Morogoro enzi hizo akina John Dilinga,Duncun Butinini,Mbui Yondani na wengine wengi waliokuwa maarufu pale Mji kasoro Bahari.

Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma kidogo ya miaka ya 1980 hadi 2000 mwanzoni... Hii town ya wajanja , vijana wanaojua kuvaa,wenye exposure, wapenda burudani na utafutaji...

Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa... Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill na Kigurunyembe ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa kishua na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto wa kihuni...

Mitaa maarufu ilikuwa ya kishua ni Forest, Liti, Sua na Rock garden... Mitaa maarufu ya ushenzini kulikuwa na Mji mpya, Kichangani, Mafiga.

Kwa sasa kichangani ni kama Kinondoni,kwa sasa Kichangani kumekuwa ushuani,Lami kila sehemu na mataa ya Magufuli,Enzi hizo Kichangani kwa watukutu kulikuwepo jamaa mmoja alikuwa anajiita mjepu, alikuwa anaingiza shilingi begani inazama yote,

Shule bora wakati huo Bungo Primary school watoto wa kichangani,walikuwa hawaruhusiwi kwenda kusoma pale,kukataliwa kulikuwa kwa sababu ya utukutu wa watoto wa kichangani,lakini niwajuze tu kichangani ndipo kulikuwa na studio bora ya muziki,

Studio ya Mbaraka Mwishehe ambapo bendi kama Cuban Malimba na Moro Jazz zilipata kurekodi hapo,utakumbuka nyimbo kadhaa za mkali wa muziki Tanzania,mkali ambaye miaka ya sabini tayari alipanda ndege kwenda kupiga Muziki pale Tokyo,Japan

Baadhi ya nyimbo zake kama ile ya heri ya Sikukuu ya Iddi "Nakutakia mkono wa Iddi" na "shemeji shemeji huku wazima taa" na nyingine nyingi kama "Jogoo la Shamba haliwiki mjini" Kichangani ni sehemu ya kihistoria,

Watoto watukutu wa kichangani enzi hizo walikuwa jumamosi wanaenda nanenane, kulikuwa na dampo linaitwa mchafu koge, watoto wa kichangani walikuwa wanaenda kuokota mavitu ya wazungu, hatari sana,umenikumbusha mbali sana mwanangu.

Tuachane na kichangani,Wakazi wa Moro ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka vitu hivi viwili vilikuwa kwenye damu yao sababu ya mastaa wa muziki kama Mbaraka Mwishehe na Staa wa soka Charles Boniface Mkwasa,Peter Tino na wengine wengi...

Morogoro kulikuwa na timu maarufu Reli kiboko ya vigogo,Reli ni kizazi cha pili cha timu bora ya timu za miaka ya sabini kama mseto,Sasa Reli kiboko ya vigogo ilikuwa daraja la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki..

Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa akiitwa "Ya mungu" ambae ndio shabiki wa kwanza mtanzania kujichora mwilini rangi nini na kubakisha macho na bukta yake tu

Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica,Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari,

Timu ambazo ziliacha umaarufu pale Morogoro ni Uruguay na Paraguayi timu hizi zikicheza refa alikuwa anaingia na panga sasa goli likifungwa mara nyingi ndio ilikuwa mwisho wa mchezo vurugu zake watu wataenda kung'oa misalaba katika uwanja ule wa kilakala makaburini,ilikuwa balaa kubwa.

Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel mziki mkubwa wa JDs Entertainment nazungumzia muziki wa John Dilinga,burudani ya beach ilikuwa Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill..

Sasa kwenye burudani ya muziki kulikuwa na mtu anaitwa Dj Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga ndio alomfundisha Udijei John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu..

Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja Dj Joseph Kusaga akimfundisha kazi Dj Peter Moe.

Watoto wa Moro enzi hizo najua mpo wengi,Mwisho Mwampamba,O-Ten na Mfalme Sele awa ni kizazi cha tatu cha burudani Mjini Morogoro,Aya watoto wa Moro naomba tukumbashane mawili matatu matukio, maujanja na mazuri ya Moro Town.

Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe.. Kulikuwa na watemi wa mji kina Slim mtoto wa sheikh mkuu, Matata, Gamba mcheza judo, vijana wa siafu toka mji mpya nk

Unaikumbuka Miss Morogoro? Lilikuwa tukio kubwa mjini,Unawakumbuka wadau Alex Nictas, Unamkumbuka Kalalambe, unamkumbuka Ghikas,

Unawakumbuka mabingwa wa kudansi kitaifa? Kina Askofu, Bob Tigger, Super Ngedere nk

Unakumbuka mashindano ya magari? Unawakumbuka wakimbiza magari maarufu waliopata kutwaa medali za dhahabu Afrika Mashariki na kati akina Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos wengi wao walikuwa ni mainjia pale kwenye karakana ya treni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,

Unakumbuka watoto wa kigiriki na bata zao na mademu zao kwa Mama Perina na Acropol? Achana na akina Sushi na Periminda Rajj awa ni uzao wa tatu kwa watoto wazuri enzi hizo mjini Morogoro,Unakumbuka masista duu na mabraza meni wa mitaa ya Forest?

Unakumbuka enzi za Mnet inaingia mjini? Moro mji wote ulikuwa na access ya kuona dstv bure toka mwaka 1990 hii ilikuwa ni favor ya Wasouth hasa baada ya kuachiwa Nelson Mandela, ambao ndugu zao walikuwa pale Mazimbu,Morogoro wameoa Waluguru na tayari wamelowea Morogoro.

Unakumbuka heka heka za ligi za mbuzi uwanja wa shujaa, makaburini kilakala,Jabal hira na kikundi,achana na Jamhuri Stadium ulikuwa uwanja wa kishua.

Unakumbuka Fete Fete? Unakumbuka Shan Cnema? Unakumbuka swimming pool ya rock garden? Ha ha ha nitakuwa nimekukumbusha mbali sana mtoto wa Moro,

Unamkumbuka Mzee Mkwidu na Patel wakuu wa shule maarufu Kigurunyembe & Forest Hill? Awa walikuwa na Wazima kama miungu miwili wa Shule kubwa za Sekondari mjini Moro,

Unamkumbuka Maneno Big G rip? Unamkumbuka Mnambo wauza ngada maarufu? Hatari sana.

Unamkumbuka Ndanje jambazi aliyetikisa mji? Unakumbuka ishu yake ya silaha na February Ma rope?

Unamkumbuka toz wa kipindi hicho Puzzo na kundi lake la kurap Watukutu akiwa na Sallam meneja wa Diamond sasa hivi?

Unawakumbuka Gangster Family? Unawakumbuka Ze domp?

Unamkumbuka Mwalimu Achimpota,Unaikumbuka bus la Chambo kutoka kihonda, unakumbuka tuisheni za Shule ya Mwele na Sabasaba.

Unakumbuka ule upepo uliokuja wa watu kuzamia Sauz na ulaya? Akina Master Bros kule CCT mizambarauni na nyimbo yake ya "Dear Mama" akiomba msamaha kwa Mama yake baada ya Safari yake ya kwenda Zambia kuishia mpakani Afrika ya kusini.

Umeishi mtaa gani Mafisa, Misufini kwa Afande Sele, Kilakala, Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma road, Sua, Vibandani, Relwe magorofani, Kigurunyembe, Madizini? Au wapi Umeishi?

Kuna watu maarufu wengi sana Dar ambao maujanja yao wamejifunzia Moro Town... Hakika Morogoro ni Jiji kasoro bahari.

WATOTO WA MOROGORO MIKONO JUU!!!

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Nipo Dar hivi sasa,
0755078854
John delinga nlijuana naye wakati huo anaishi manzese..... Dj jd alifundishwa na dj John Peter pantalakis...... Chotara wa kihaya na kigiriki

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni Mananga (RIP) Product! Msaidizi Mama SUMARI na Mwl. selemani! Ngakuka yupo na FRENCH, pale MATHS alisimama MKAMI, huku BIOS alicheza KUNAMBI, Michezo Mwl. SUKA bila kumsahau Mama NJAMA ktk ENGLISH Enzi hizo MORO SEC haijazungushiwa ukuta, pale uwanjani JAMAICA ndio ulikuwa uwanja wao!

Sent using Jamii Forums mobile app
Maths Siyo Ole yule mmasai for DEF, na ABC mwishee. Wengine wooote tuko sawa. Vipi zile Pipi kule Mochuari, natamani niowaone wale wauzaji niwake buku 10 nifidie nilizoiba na kununua na kuokota.
HP wako nani, HZ, HM,MN,JA hao walikuwa Ma HP bora kwangu.
Mr Musoma RIP
 
Unapakumbuka Kaumba?
Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma kidogo ya miaka ya 90 hadi 2000 mwanzoni. Hii town ya wajanja, vijana wanaojua kuvaa, wenye exposure, wapenda burudani na utafutaji. Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa. Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill na Kigurunyembe ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa kishua na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto wa kihuni. Mitaa maarufu ilikuwa ya kishua ni Forest, Liti, Sua na Rock Garden. Mitaa maarufu ya ushenzini kulikuwa na Mji mpya, Kichangani, Mafiga.

Watu wa Moro ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka. Kulikuwa na timu ya mji maarufu Reli kiboko ya vigogo hii ilikuwa daraja la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki. Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa kuitwa ya Mungu ambae ndio shabiki wa kwanza Mtanzania kujichora mwilini. Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica, kulikuwa na Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari.

Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel na Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill. Hapa kuna mtu anaitwa DJ Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga ndio alomfundisha Udijei John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu. Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja DJ Joseph Kusaga akimfundisha kazi DJ Peter Moe.

Watu wa Moro najua mpo wengi umu Jf naomba tukumbashane mawili matatu matukio, maujanja na mazuri ya Moro Town.

Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe. Kulikuwa na watemi wa mji kina Slim mtoto wa sheikh mkuu, Matata, Gamba mcheza judo, vijana wa siafu toka mji mpya nk

Unaikumbuka Miss Morogoro? Unamkumbuka Alex Nictas?

Unawakumbuka mabingwa wa kudansi kitaifa? Kina Askofu, Bob Tigger, Super Ngedere nk

Unakumbuka mashindano ya magari? Unawakumbuka wakimbiza magari maarufu kina Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos nk

Unakumbuka Wagiriki na bata zao kwa Mama Perina na Acropol? Unakumbuka masista duu na mabraza meni wa mitaa ya Forest?

Unakumbuka enzi za Mnet inaingia mjini? Moro mji wote ulikuwa na access ya kuona dstv bure.

Unakumbuka heka heka za ligi za mbuzi uwanja wa shujaa, makaburini kilakara na kikundi?

Unakumbuka Fete Fete? Unakumbuka Shan cinema? Unakumbuka swimming pool ya rock garden?

Unamkumbuka Mzee Mkwidu na Patel wakuu wa shule maarufu KG & Forest?

Unamkumbuka Maneno Big G rip? Unamkumbuka Mnambo wauza ngada maarufu?

Unamkumbuka Ndanje, jambazi aliyetikisa mji? Unakumbuka ishu yake ya silaha na February Ma rope?

Unamkumbuka toz wa kipindi hicho Puzzo na kundi lake la kurap Watukutu akiwa na Sallam meneja wa Diamond sasa hivi? Unawakumbuka Gangster Family? Unawakumbuka Ze Domp?

Unamkumbuka Achimpota? Unaikumbuka bus la Chambo?

Unakumbuka ule upepo uliokuja wa watu kuzamia Sauz na ulaya?

Umeishi mtaa gani Mafisa, Msufini, Kilakara, Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma road, Sua, Vibandani, Relwe magorofani, Kigurunyembe, Madizini? Au wapi Umeishi?

Kuna watu maarufu wengi sana DSM ambao maujanja yao wamejifunzia Moro Town. Hakika Morogoro ni jiji kasoro bahari.

WATOTO WA MOROGORO MIKONO JUU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MOROGORO HAPO ZAMANI.

Leo 23:25pm 17/04/2020

Watoto wa Morogoro enzi hizo akina John Dilinga,Duncun Butinini,Mbui Yondani na wengine wengi waliokuwa maarufu pale Mji kasoro Bahari.

Naizungumzia zaidi Moro ya kipindi cha nyuma kidogo ya miaka ya 1980 hadi 2000 mwanzoni... Hii town ya wajanja , vijana wanaojua kuvaa,wenye exposure, wapenda burudani na utafutaji...

Ni mji uliofikia kuitwa jiji kasoro bahari kutokana na upatikanaji wa kila kitu kinachotakiwa... Kulikuwa na shule kubwa mbili Forest Hill na Kigurunyembe ambapo Forest ilikuwa ya watoto wa kishua na Kigurunyembe ilikuwa ya watoto wa kihuni...

Mitaa maarufu ilikuwa ya kishua ni Forest, Liti, Sua na Rock garden... Mitaa maarufu ya ushenzini kulikuwa na Mji mpya, Kichangani, Mafiga.

Kwa sasa kichangani ni kama Kinondoni,kwa sasa Kichangani kumekuwa ushuani,Lami kila sehemu na mataa ya Magufuli,Enzi hizo Kichangani kwa watukutu kulikuwepo jamaa mmoja alikuwa anajiita mjepu, alikuwa anaingiza shilingi begani inazama yote,

Shule bora wakati huo Bungo Primary school watoto wa kichangani,walikuwa hawaruhusiwi kwenda kusoma pale,kukataliwa kulikuwa kwa sababu ya utukutu wa watoto wa kichangani,lakini niwajuze tu kichangani ndipo kulikuwa na studio bora ya muziki,

Studio ya Mbaraka Mwishehe ambapo bendi kama Cuban Malimba na Moro Jazz zilipata kurekodi hapo,utakumbuka nyimbo kadhaa za mkali wa muziki Tanzania,mkali ambaye miaka ya sabini tayari alipanda ndege kwenda kupiga Muziki pale Tokyo,Japan

Baadhi ya nyimbo zake kama ile ya heri ya Sikukuu ya Iddi "Nakutakia mkono wa Iddi" na "shemeji shemeji huku wazima taa" na nyingine nyingi kama "Jogoo la Shamba haliwiki mjini" Kichangani ni sehemu ya kihistoria,

Watoto watukutu wa kichangani enzi hizo walikuwa jumamosi wanaenda nanenane, kulikuwa na dampo linaitwa mchafu koge, watoto wa kichangani walikuwa wanaenda kuokota mavitu ya wazungu, hatari sana,umenikumbusha mbali sana mwanangu.

Tuachane na kichangani,Wakazi wa Moro ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka vitu hivi viwili vilikuwa kwenye damu yao sababu ya mastaa wa muziki kama Mbaraka Mwishehe na Staa wa soka Charles Boniface Mkwasa,Peter Tino na wengine wengi...

Morogoro kulikuwa na timu maarufu Reli kiboko ya vigogo,Reli ni kizazi cha pili cha timu bora ya timu za miaka ya sabini kama mseto,Sasa Reli kiboko ya vigogo ilikuwa daraja la kwanza alikuwa akija Simba au Yanga atoki..

Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana wa akiitwa "Ya mungu" ambae ndio shabiki wa kwanza mtanzania kujichora mwilini rangi nini na kubakisha macho na bukta yake tu

Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica,Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari,

Timu ambazo ziliacha umaarufu pale Morogoro ni Uruguay na Paraguayi timu hizi zikicheza refa alikuwa anaingia na panga sasa goli likifungwa mara nyingi ndio ilikuwa mwisho wa mchezo vurugu zake watu wataenda kung'oa misalaba katika uwanja ule wa kilakala makaburini,ilikuwa balaa kubwa.

Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel mziki mkubwa wa JDs Entertainment nazungumzia muziki wa John Dilinga,burudani ya beach ilikuwa Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill..

Sasa kwenye burudani ya muziki kulikuwa na mtu anaitwa Dj Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga ndio alomfundisha Udijei John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu..

Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja Dj Joseph Kusaga akimfundisha kazi Dj Peter Moe.

Watoto wa Moro enzi hizo najua mpo wengi,Mwisho Mwampamba,O-Ten na Mfalme Sele awa ni kizazi cha tatu cha burudani Mjini Morogoro,Aya watoto wa Moro naomba tukumbashane mawili matatu matukio, maujanja na mazuri ya Moro Town.

Moro Town ulikuwa pia mji wa kibabe.. Kulikuwa na watemi wa mji kina Slim mtoto wa sheikh mkuu, Matata, Gamba mcheza judo, vijana wa siafu toka mji mpya nk

Unaikumbuka Miss Morogoro? Lilikuwa tukio kubwa mjini,Unawakumbuka wadau Alex Nictas, Unamkumbuka Kalalambe, unamkumbuka Ghikas,

Unawakumbuka mabingwa wa kudansi kitaifa? Kina Askofu, Bob Tigger, Super Ngedere nk

Unakumbuka mashindano ya magari? Unawakumbuka wakimbiza magari maarufu waliopata kutwaa medali za dhahabu Afrika Mashariki na kati akina Collen, Steve, Pat, Kararambe, Shanto, De Santos wengi wao walikuwa ni mainjia pale kwenye karakana ya treni ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,

Unakumbuka watoto wa kigiriki na bata zao na mademu zao kwa Mama Perina na Acropol? Achana na akina Sushi na Periminda Rajj awa ni uzao wa tatu kwa watoto wazuri enzi hizo mjini Morogoro,Unakumbuka masista duu na mabraza meni wa mitaa ya Forest?

Unakumbuka enzi za Mnet inaingia mjini? Moro mji wote ulikuwa na access ya kuona dstv bure toka mwaka 1990 hii ilikuwa ni favor ya Wasouth hasa baada ya kuachiwa Nelson Mandela, ambao ndugu zao walikuwa pale Mazimbu,Morogoro wameoa Waluguru na tayari wamelowea Morogoro.

Unakumbuka heka heka za ligi za mbuzi uwanja wa shujaa, makaburini kilakala,Jabal hira na kikundi,achana na Jamhuri Stadium ulikuwa uwanja wa kishua.

Unakumbuka Fete Fete? Unakumbuka Shan Cnema? Unakumbuka swimming pool ya rock garden? Ha ha ha nitakuwa nimekukumbusha mbali sana mtoto wa Moro,

Unamkumbuka Mzee Mkwidu na Patel wakuu wa shule maarufu Kigurunyembe & Forest Hill? Awa walikuwa na Wazima kama miungu miwili wa Shule kubwa za Sekondari mjini Moro,

Unamkumbuka Maneno Big G rip? Unamkumbuka Mnambo wauza ngada maarufu? Hatari sana.

Unamkumbuka Ndanje jambazi aliyetikisa mji? Unakumbuka ishu yake ya silaha na February Ma rope?

Unamkumbuka toz wa kipindi hicho Puzzo na kundi lake la kurap Watukutu akiwa na Sallam meneja wa Diamond sasa hivi?

Unawakumbuka Gangster Family? Unawakumbuka Ze domp?

Unamkumbuka Mwalimu Achimpota,Unaikumbuka bus la Chambo kutoka kihonda, unakumbuka tuisheni za Shule ya Mwele na Sabasaba.

Unakumbuka ule upepo uliokuja wa watu kuzamia Sauz na ulaya? Akina Master Bros kule CCT mizambarauni na nyimbo yake ya "Dear Mama" akiomba msamaha kwa Mama yake baada ya Safari yake ya kwenda Zambia kuishia mpakani Afrika ya kusini.

Umeishi mtaa gani Mafisa, Misufini kwa Afande Sele, Kilakala, Ngoto, Kingo, Mlapakoro, Boma road, Sua, Vibandani, Relwe magorofani, Kigurunyembe, Madizini? Au wapi Umeishi?

Kuna watu maarufu wengi sana Dar ambao maujanja yao wamejifunzia Moro Town... Hakika Morogoro ni Jiji kasoro bahari.

WATOTO WA MOROGORO MIKONO JUU!!!

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Nipo Dar hivi sasa,
0755078854
Mwalimu jesca achimopota

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forest Hills watoto wa pateli au sio nawewe ni mwarabu nini make ndo wamejaa pale!

Lol maeneo ya forest huko kichangani kilakala kote tulikua tunaenda kuchota maji pindi hostel morosec yakikatika hapo ndo tunapata muda wa kuzuruzaaa

Cc Smart911
[emoji23][emoji23][emoji23] na vile hakuna uzio

Enzi za mkangwa au?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom