Morocco ni mwenyeji wa ofisi kubwa za soka ila fainali inafanyika kwao halafu VAR haifanyi kazi

Morocco ni mwenyeji wa ofisi kubwa za soka ila fainali inafanyika kwao halafu VAR haifanyi kazi

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,470
Mpira wa Africa una figisu sana. Inashangaza sana kuna wenzetu wanaunga mkono figisu inazofanyiwa Simba au wanatoa vimaneno pale Simba inapofanya kila inachoweza kupata ushindi, hawajui kuna siku kwa unyonge wetu na timu zao zinaweza kuja kuwa wahanga na kuwa harakati za Simba zinafungua njia kwa mafanikio ya timu zetu nyingine wajue wapite wapi.

Kuhusu mechi ya jana, watu hawajaongelea kitendo cha screen ya VAR kutofanya kazi kuanzia mwanzoni tu wa mchezo hadi mchezo mzima. Mwamuzi aliwataarifu macaptain kuwa sceeen ina hitilafu kwa hiyo likitokea lolote inabidi awasikilize tu wasaidizi waliopo kwenye chumba cha VAR.

Morocco ni mwenyeji wa ofisi muhimu zisizopungua mbili za soka. Hata tuzo za CAF huwa zinafanyika Morocco. Inashangaza sehemu kama hii inaruhusu figisu za namna hii zinafanyika.

Mpira wa Africa ukiwa nyumbani kwako hautakiwi kumuangalia mtu usoni. Waarabu wanalijua hili ndiyo maana wamejimilikisha mafanikio ya mpira wa Africa katika ngazi ya vilabu.

Kesho katika mechi ya nyumbani ya Simba VAR ikiwa haifanyi kazi, utasikia midomo ya waswahili wenzetu.

Embu tujitambue tuache kuwaunga mkono na figisu zao kisa tuna utani wa jadi wa ndani, hivi hivi tutabaki wanyonge milele.

Katika mechi ya pili ya fainali wiki ijayo dhidi ya Berkane, Simba ifungulie booster zote za Ubaya Ubwela, isiache silaha katika stoo.
 
Kwahy berkane wamebebwa kuanzia mwanzo wa mashindano mpaka sasa?
Simba tulieni Acheni visingizio 😂
Jana kwa kweli hawajabebwa ndiyo maana hata baada ya mpira Kwisha waliendelea kudai penalty hewa.

Tarehe 25 watatujua na kututambua.
 
Sasa simba var mngeitumia kwenye tukio gani??
Matukio tata yalikua yanawafavour Belkane, hilo ni suala la kushukuru. Si ajabu figisu za var kutofanya kazi Mangungu anahusika.
 
Jana kwa kweli hawajabebwa ndiyo maana hata baada ya mpira Kwisha waliendelea kudai penalty hewa.

Tarehe 25 watatujua na kututambua.
Trh 25 mpigwe kimoja cha kijogoo mechi iishie hapo, na hv mtakuwa zanziberi Ndo maumivu mengine utadhani sio nyie mliosifia hicho kiwanja kwenye mechi iliyopita hapo 😂
 
Trh 25 mpigwe kimoja cha kijogoo mechi iishie hapo, na hv mtakuwa zanziberi Ndo maumivu mengine utadhani sio nyie mliosifia hicho kiwanja kwenye mechi iliyopita hapo 😂
Simba watashinda mabao matatu. Nimeshaliona hili kwa darubini kali mkuu.

Tusiposhinda nidai kiasi chochote cha pesa unachoona kitakutosha.
 
Jana kwa kweli hawajabebwa ndiyo maana hata baada ya mpira Kwisha waliendelea kudai penalty hewa.

Tarehe 25 watatujua na kututambua.
Kuna kazi za njano walikuwa wapewe ila refa akazimezea. Zile za kujiangusha ndani ya box zote ni kadi zile. Kuna mmoja alikuwa apate kadi na angeipata, mechi ya pili asingeweza kucheza.
 
Back
Top Bottom