GE2025 Moja ya impacts za CHADEMA kutoshiriki Uchaguzi zaanza kuonekana sasa

GE2025 Moja ya impacts za CHADEMA kutoshiriki Uchaguzi zaanza kuonekana sasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
11,163
Reaction score
22,739
Chadema ndo ilikuwa inatia wagombea hofu wa vyama vingine.kwa kutokushiriki sasa imefungulia kila mtu ambaye anajua atagombea kupitia CCM atashinda bila wasiwasi.

Na wakati huo huo vyama vingine vya upinzani vinaona hii ni nafasi ya wao kuweza pata wabunge kwa kuwa ni wazi kuna majimbo ambayo wataachiwa ili kuweza balance kidogo shughuli za kibunge.

Sasa every Tom , Dick and Harry wants to be a MP. Na watu wa CCM na vyama rafiki wanafurahia kuwa hili libaki kama lilivyo kusiwe na mabadiliko kutoka NRNE ibaki vivyo hivyo.
 
Kwa nyongeza kushiriki cha CDM kungeleta faida zifuatazo kwa CCM
1. Watu wengi kujitokeza kupiga kura, hivyo, kuwa rahisi kwa CCM kuiba kura kutokana na justification ya wingi wa watu-Ifahamike huendi mwaka huu ukawa na watu wachache sana kwenda kupiga kura wakiamini wagombea wa CCM wameshapita automatically hata kama kutakuwa kura ya Ndiyo au Hapana
2. Kwa baadhi wa wagombea wa CCM ambao kwa namna moja au nyingine watanyimwa fursa ya kugombea/kupitishwa na wajumbe kupitia chama chao, walikuwa wanaweza kuhama chama na kuhamia upinzani na kuweza kugombea kutokana na popularity ya mgombea. Baadhi ya wagombea watakosa fursa hiyo kutokana na kutoshiriki kwa CDM-Ifahamike uwezekano wa kushinda unategemea na nguvu ya chama husika ambacho mgombea amehamia​
 
Haya ndio wengine tulikuwa tunahofia. Chadema walikurupuka na NRNE na hawakutaka kusikia ushauri. G55 waliwaambia CCM ukiwaachia mpunga wanaondoka na sinia.

Sasa hivi kila mtu anajua kuwa serikali na bunge lijalo ni la CCM. Bunge la wakina Shilole na Mwijaku.

Safari hii CCM hawatafanya kosa la kuharibu uchaguzi mpaka ikabidi walazimishe upinzani feki wa Covid-19.

Sasa hivi ACT-WAZALENDO na Chaumma wataachiwa washinde viti kadhaa ili kuwe na kambi rasmi ya upinzani isiyo na meno. Watajitahidi kuwasemea wananchi lakini watapuuzwa. Na Katiba Mpya italetwa na hilo bunge.

Chadema wangeunganisha kambi na kuwasikiliza G55 Sasa hivi pangekuwa na msisimko zaidi na wangewasumbua sana CCM. Tumaini lililobaki ni baadhi ya watu makini waliobaki kuhama CDM na kuhamia CHAUMMA au ACT-WAZALENDO.

Na hapa bado. Tutaona watakavyoendesha chama chao bila ruzuku. Kwa miaka mitano.

Kama hali itakuwa hivyo, lawama zote itabidi zibebwe na Chadema na sio mwengine.

Amandla..
 
Wapo bize kwa kalumanzila tangu jana wakati hawana mpinzani
 

Attachments

  • e60cf688-223b-473e-8594-3406b1e11014.jpeg
    e60cf688-223b-473e-8594-3406b1e11014.jpeg
    106.4 KB · Views: 16
  • 49601334-f0e8-44a2-bd50-2c448200b869.mov
    1.5 MB
Back
Top Bottom