Ndio ndio......kuna watu kila wakiona sura za wahindi wanakasirika.........hii thread inaonekana ina elements vya chuki dhidi ya wahindi......Sisi hapa tunamzungumzia Mohammed Dewji kama mtu binafsi na haituizungumzii jamii yake. Maendeleo ya kweli ni yapi? huoni kuwa kwa kutumia soka tunaweza pia kuongeza pato la nchi kwenye utalii au hata kuboresha maisha ya vijana mbalimbali ambao wanaweza kuisaidia taifa lao kwa kuchangia kwenye pato la Taifa. Ukianza kujumuisha jamii yake utakuwa unakosea, sisi tunamzungumzia yeye kama mtu binafsi na michango yake mbalimbali. Je Mushi wewe ni Mzalendo? na umechangia nini kwenye Taifa lako?
Inaweza kuwa sio Wahindi-Watanzania wote wana mapenzi ya kweli na Tanzania. Lakini bila ya shaka kuna baadhi yao ni wazalendo kutushinda waasili wenyewe.
Kweli kuna sababu ya kuwa na wasiwasi na uzalendo wa Mohamed Dewj kama anavyoonekana kwenye picha hizi mbili (attached)? Aliacha shughuli zake muhimu na kujitokeza kushangilia ushindi wa Taifa stars. Ushindi ambao hauna faida wala maslahi yoyote kwa Mhindi ambaye hana mapenzi ya kweli na Tanzania.
Hakika huyu ni mmoja wa Wahindi wenye 'damu ya Kitanzania.'
Nasikia huyu kijana ni mafia. Bidhaa zake nyingi ni substandard.
Wewe unakijua kiswahili?......hoja mufilisi....nina ndugu zangu wanyantuzu hawajui hata salamu ya kiswahili nao je?Kaka!
MO Dewji hata kiswahili hajui....halafu hapa tunaongelea uzalendo.
Wewe unakijua kiswahili?......hoja mufilisi....nina ndugu zangu wanyantuzu hawajui hata salamu ya kiswahili nao je?
Kaka!
MO Dewji hata kiswahili hajui....halafu hapa tunaongelea uzalendo.
Kumbe huna uhakika.mi naona wanyantuzu wako unyantuzuni huko. MO tuko nae mitaani mijini. akina MO mara nyingi wanakuwa wamezaliwa mijini. tofauti na wanyantuzu au makabila mengine yaliyo mbali na mijini.
mtu akitoka usukumani au ufipani au popote pale kule kijijini akifika mjini akiongea kiswahili mostly kitakuwa na lafudhi ya huko alikotoka. baada ya muda hubadilika na inakuwa vigumu kujua katoka wapi akiongea kiswahili.
huenda MO au akina MO hawafagilii kiswahili. au pengine ukijua kiasia/kihindi inakuwa vigumu kuongea kiswahili vizuri.
Bora wewe uongee..........Mbona huwa namsikia akiongea Kiswahili(anapohojiwa na media),labda unifafanulie mkuu hajui Kiswahili kivipi???,je kampeni zake za Ubunge kwa wananchi wa Singida alizifanya kwa kutumia Lugha ipi??,alikuwa na mkalimani ama??,naomba unisaidie kwa hilo mkuu..Heshima mbele..Be blessed
...Ubunge una heshima yake. Unapovua shati kwenye kadamnasi na kuruka ruka tumbo wazi ndio tukujue kuwa wewe ni mzalendo sanaa, ama?? You must hand it to him, though. The guy knows how to hog some cheap publicity from unsuspecting Bongomites!!
....Unapovua shati kwenye kadamnasi na kuruka ruka tumbo wazi ndio tukujue kuwa wewe ni mzalendo sanaa, ama??.....
Msamehe Mnyaturu huyo..
Huu ni ukereketwa, uzalendo au mananii yalizidi!! Ni kweli kabisa kila Mtanzania mpenda maendeleo amefurahia ushindi wa Taifa Stars. Lakini nimeshangaa kuona hii picha hapo chini na kuona Mh. Dewji akionyesha BOXER yake. Kwa kiongozi wa jamii kuonyesha kitu kama hicho kwa mtazamo wangu haileti picha nzuri. Tusianze tukajikuta tunaanza hata ku-promote vitu ambavyo havina maana kwa jamii, mfano mitepesho n.k
Haya ni maoni yangu, wewe mwenzangu unasemaje? Angalia hiyo picha hapo chini. Bonyeza palipoandikwa Dewji hapo chini...