Zack Abdul
JF-Expert Member
- Mar 9, 2026
- 1,176
- 900
Ndugu zangu Watanzania Wazalendo kuna wakati tunapaswa kusema ukweli kuhusu mwenendo wa baadhi ya siasa zinazofanywa na Ufipa kwa sababu Taifa letu lina thamani kubwa kuliko maslahi ya kisiasa ya watu wachache.
Tanzania imejengwa katika msingi wa amani mshikamano utu na kuheshimiana HII NI SHERIA MAMA. Huo ndio utamaduni wetu wa Kitanzania uliotufanya tubaki imara kwa miaka mingi tofauti na mataifa mengi yaliyotikiswa na migogoro ya kisiasa.
Lakini kwa sasa tunaona baadhi ya viongozi wa CHADEMA wakijenga siasa za taharuki na uchochezi kila siku kana kwamba maendeleo ya kisiasa lazima yaambatane na hasira migawanyiko na kuaminisha wananchi kuwa hakuna tumaini ndani ya nchi yao.
Badala ya kuzungumzia sera, uchumi, ajira, elimu na maendeleo ya wananchi mara nyingi nguvu kubwa inawekwa katika kuhamasisha taharuki na kuwagawa Watanzania kwa misimamo ya kisiasa.
Hii siyo siasa tulizozirithi kutoka kwa waasisi wetu. Tanzania ilisimama kwenye msingi wa majadiliano uvumilivu na heshima hata pale watu walipokuwa na tofauti kubwa za kiitikadi.
Leo hii tunaona baadhi ya wanasiasa wakiamini kuwa ukali wa maneno matusi na uchochezi ndiyo njia ya kupata umaarufu wa kisiasa.
Hilo ni jambo la hatari kwa mustakabali wa Taifa letu.
Kinachoumiza zaidi ni kuona baadhi ya viongozi wanaotafuta kuaminiwa na
Watanzania wakionekana mara kwa mara kwenye mabaa😆 starehe za usiku na maisha ambayo hayatoi picha ya uongozi wa mfano kwa vijana.
Jamii yetu bado inaamini kuwa kiongozi anatakiwa kuwa na maadili nidhamu na kujiheshimu kwa sababu yeye ndiye kioo cha jamii.
Vijana wetu wanaiga wanachokiona kutoka kwa viongozi wao.
Kiongozi anapokuwa mstari wa mbele kwenye vurugu za kisiasa au maisha ya anasa yasiyoendana na maadili ya uongozi anaharibu taswira ya kizazi kizima.
Tatizo jingine kubwa ni uchu wa madaraka na ubinafsi unaoonekana wazi ndani ya siasa hizi.
Badala ya siasa kuwa chombo cha kuwatumikia wananchi zimeanza kuonekana kama njia ya kutafuta umaarufu fedha na nafasi binafsi.
Wengine wako tayari kutumia hasira za wananchi kama mtaji wa kisiasa ilimradi wapate nguvu ya kisiasa.
Lakini mzalendo wa kweli hawezi kuchezea amani ya nchi yake kwa sababu ya tamaa ya madaraka.
Tunapaswa kujifunza kupitia mataifa mengine yaliyopoteza utulivu kwa sababu ya siasa za uchochezi.
Mara nyingi migogoro huanza taratibu kupitia maneno ya kuwagawa wananchi kueneza chuki na kuwafanya vijana waamini kuwa vurugu ndiyo suluhisho la matatizo yao. Tanzania haipaswi kufika huko.
Taifa letu lina heshima kubwa Afrika kwa sababu ya utulivu wake na jukumu la kila mzalendo ni kuulinda.
Siasa za taharuki hazijawahi kujenga nchi yoyote Maendeleo huja kupitia utulivu, kazi, uwekezaji, umoja na wananchi kuwa na matumaini na nchi yao.
Tunahitaji siasa za hoja siasa za sera na siasa za ushindani wa maendeleo.
Kama kuna changamoto ndani ya nchi zipingwe kwa ustaarabu na kwa hoja si kwa kuwasha moto wa hasira kwa wananchi kila siku.
Ni muhimu pia vijana wakaelewa kuwa siasa si uadui.
Unaweza kuwa na tofauti za kisiasa lakini ukaendelea kuwa mzalendo wa nchi yako.
Hatupaswi kufikia hatua ya kuwafanya Watanzania wachukiane kwa sababu ya vyama vya siasa.
Taifa ni kubwa kuliko chama chochote na amani ni muhimu kuliko ushindi wa kisiasa.
Msimamo wa wazalendo wa kweli unabaki kuwa mmoja kulinda amani ya Tanzania kuheshimu utamaduni wetu wa mshikamano na kuhakikisha viongozi wanaotafuta ridhaa ya wananchi wanaonyesha maadili busara na uzalendo wa kweli.
Tanzania yetu isiwe sehemu ya siasa za vurugu bali ibaki kuwa mfano wa utulivu heshima na maendeleo kwa vizazi vya sasa na vijavyo. #TanzaniaYetu