Ladslaus Modest
JF-Expert Member
- Jun 27, 2008
- 635
- 20
Aliyekuwa rais wa Botswana, Festus Mogae, ameshinda tuzo yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 5 itakayohamasisha utawala bora barani Afrika.
Bw Mogae aliachia madaraka mwezi Aprili baada ya kutumikia urais kwa vipindi viwili nchini humo.
Botswana ni moja ya nchi zenye utulivu mno kutoka bara la Afrika, haijawahi kuwa na mapinduzi na imekuwa na uchaguzi wa vyama vingi mara kwa mara tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 1966.
Wakati wa kutangazwa zawadi hiyo, aliyekuwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annan, amemsifia Bw Mogae kwa hatua yake ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi uliokithiri nchini humo.
Tuzo ya Mo Ibrahim, ambayo ni tuzo yenye thamani ya juu kabisa duniani ilianzishwa na mjasiriamali wa masuala ya mawasiliano aliye raia wa Sudan, Mo Ibrahim.
Mbali na tuzo hiyo ya milioni 5, Bw Mogae pia atapokea dola za kimarekani 200,000 kwa mwaka mpaka maisha yake yatakapofikia hatima.
Botswana imejaaliwa na madini ya almasi, lakini ukilinganisha na nchi nyingine zenye utajiri wa aina hiyo barani Afrika madini hayo haikuwa chanzo cha mgogoro nchini humo.
Chanzo BBC
Ninatumaini kipindi kijacho zawadi hii itakuja Tanzania.