Mogae wa Botswana ashinda tuzo

Wakuu pengine niseme tu kuwa kilichonyuma ya mo ibrahimu dhidi ya mkapa ni zanzibar 2001, hilo ndilo jambo ambalo wakubwa hawakutaka litokee kule kwa kisingizio cha demokrasia lakini mkapa alithibitisha kuwa yeye ni mkuu wa nchi na siyo genge kama wakubwa wanavyotaka sasa ionekane kuwa ni uvunjaji wa haki za binadamu, ninasisitiza kuwa bwm ktk issue ya zenj ilimpasa kuwajibika ktk stahili ile, pengine tumuulize dkt salim kama yeye angelikuwa rais zama zile angefanya nini kuzima uasi ule wa wapemba? Kama kuibiwa kura walishaibiwa tangu 95, ule ulikuwa ni ujeuri wa kumtishia mtu mzima nyau.

Kuhusiana na tuhuma za ufisadi hilo nalipinga kwani mo ibrahim org haiwezi kufanyia kazi tuhuma za mtaani ambazo hazijathibitika kisheria, na siyo mo ibrahimu tu bali mtu yeyote makini na mpenda na mtenda haki kamwe hawezi kujiingiza ktk maamuzi yanayotegemea media tena za tz.

Mogae ame score zaidi kt vita against aids jambo ambalo kwa kule wenzetu ni janga sawa na malaria tz, hivyo msije shangaa jk akiitwa tuzo hii endapo tu mambo yataenda kama yalivyo sasa hapa nchini.

All in all hii inathibitisha kuwa ndani ya mo ibrahim na panel ya majaji kuna mgawanyiko mkubwa juu ya kile kilichompatia chisano tuzo hiyo 2007, ni dhahiri kuna watu ndani yake hawakuridhika kukosa kwa mkapa.

Pengine nikubaliane na wakosoaji kuwa ilitosha kwa 2007 mkapa kuwa runner up, na haikuwa vema tena this year kum consider kwa tuzo hiyo maana jamaa kaiacha nchi 2005 hii 2008 na mbaya zaidi ni tuzo ya pili why considerring mkapa and not others hata kama si marais? Hapo wamethibitisha udhaifu wao wa vigezo kiutendaji.

Lakini ninaomba kufahamu pia kama ni kweli huyu comrade aliingizwa tena ktk kinyang'anyiro hicho ambacho si cha kuomba?
Maana nahisi media zetu kama kawaida bado siziamini.
 
hii award ina mapungufu makubwa sana... kama alikosa mwaka jana iweje awe tena kwenye kuiwania? hii award haitakiwi kuotolewa kila mwaka maana mwisho wa siku watakuwa wameisha marais bora naitaenda kwa ambae hafai. inatakiwa itolewe labda kila baada ya miaka mitatu ili tuwe tumepata wastaafu wapya.... na ikiwezekana mara nyingine mshindi akosekane
nakubaliana na wewe kabisa..... Maana marais wa ivyo ni wachache sana Africa na wengi wao hawataki kutoka madarakani. kama inatolewa kila mwaka wataishiwa majina soon.
 
pamoja na propaganda zote bado MZEE BEN ni kifaa katika historia ya utawala wenye mafanikio hapa nchini. kuingia kwake kwenye kinyanganyiro hicho na kutajwa kama mshindani makini kwa kirefu na vyombo mbali mbali ni historia na alama ya mafanikio kwake kama kiongozi na taifa aliloliongoza.

Mzee Ben rekodi yake ni ya kujivunia, ushahidi upo machoni mwa jamii makini. barabara, shule, huduma za serikali, economic reforms, revenue growth....

media zetu badooooooooo....au uchambuzi dhaifuuuuu.
chuki za kisiasa kwa huyu mzee zimebackfire mapemaaaaa,

Tukimlinganisha Mkapa na mtawala aliyemtangulia yaani Mzee Mwinyi na aliyemfuatia yaani JK ukweli ni kuwa Mkapa ataendelea kuwa best. Lakini hii hituzuii kusema kuwa Mkapa hafai kushinda tuzo ya Utawala Bora ya Mo Ibahim jamani.

Bila shaka tunakubaliana kuwa Mwenye Chongo ni bora mara elfu kuliko kipofu (siwakashifu walemavu ila natumia nahau kufikisha ujumbe) lakini akiwekwa na wenye macho bado ataonekana ana kasoro. Ukimweka Mkapa na Watawala wabovu ataonekana kung'ara lakini hana sifa ya kushindanishwa na Watawala makini!

Watanzania tutamkumbuka Mkapa!

Ni kweli tutamkumbuka Mkapa, sababu kubwa ya kumkumbuka ni kuwa hatujapata kiongozi bora kuliko yeye kwa miongo miwili sasa lakini bado huwezi kumwingiza Mkapa kutafuta kiongozi mwenye vigezo vya utawala bora Africa.

Wakuu pengine niseme tu kuwa kilichonyuma ya mo ibrahimu dhidi ya mkapa ni zanzibar 2001, hilo ndilo jambo ambalo wakubwa hawakutaka litokee kule kwa kisingizio cha demokrasia lakini mkapa alithibitisha kuwa yeye ni mkuu wa nchi na siyo genge kama wakubwa wanavyotaka sasa ionekane kuwa ni uvunjaji wa haki za binadamu, ninasisitiza kuwa bwm ktk issue ya zenj ilimpasa kuwajibika ktk stahili ile, pengine tumuulize dkt salim kama yeye angelikuwa rais zama zile angefanya nini kuzima uasi ule wa wapemba? Kama kuibiwa kura walishaibiwa tangu 95, ule ulikuwa ni ujeuri wa kumtishia mtu mzima nyau.

Kuhusiana na tuhuma za ufisadi hilo nalipinga kwani Mo ibrahim org haiwezi kufanyia kazi tuhuma za mtaani ambazo hazijathibitika kisheria, na siyo mo ibrahimu tu bali mtu yeyote makini na mpenda na mtenda haki kamwe hawezi kujiingiza ktk maamuzi yanayotegemea media tena za tz.

Mogae ame score zaidi kt vita against aids jambo ambalo kwa kule wenzetu ni janga sawa na malaria tz, hivyo msije shangaa jk akiitwa tuzo hii endapo tu mambo yataenda kama yalivyo sasa hapa nchini.

All in all hii inathibitisha kuwa ndani ya mo ibrahim na panel ya majaji kuna mgawanyiko mkubwa juu ya kile kilichompatia chisano tuzo hiyo 2007, ni dhahiri kuna watu ndani yake hawakuridhika kukosa kwa mkapa.

Pengine nikubaliane na wakosoaji kuwa ilitosha kwa 2007 mkapa kuwa runner up, na haikuwa vema tena this year kum consider kwa tuzo hiyo maana jamaa kaiacha nchi 2005 hii 2008 na mbaya zaidi ni tuzo ya pili why considerring mkapa and not others hata kama si marais? Hapo wamethibitisha udhaifu wao wa vigezo kiutendaji.

Lakini ninaomba kufahamu pia kama ni kweli huyu comrade aliingizwa tena ktk kinyang'anyiro hicho ambacho si cha kuomba?
Maana nahisi media zetu kama kawaida bado siziamini.
Swadakta, hilo naungana nawe.

Nimalizie kwa kusema kuwa Mkapa atakuja kuipata tuzo ya Mo iwapo tu Africa tutakuwa tunarudi nyuma; lakini kama tunasonga mbele hatakuja kuipata!
 
..nakubaliana na mchangiaji aliyependekeza tuzo hii isiwe inatolewa kila mwaka.

..wajaribu kuitoa kila baada ya miaka 5 ili tuwe na washindani wengi zaidi.

NB:

..Salim Salim ni mmoja kati ya majaji wanaochagua mshindi.

..nategemea atatumia ushawishi wake kuwezesha tuzo hiyo kwenda kwa Mkapa au Kikwete.
 
Dude, you can't be serious......
 
Nyani McCain,

..kuna watu[ndani na nje] wanaamini Kikwete is good for the country. i am not one of them though.

..sasa huenda Salim Salim ni miongoni mwa wa-Tanzania hao. kwa msingi huo basi nategemea anaweza kuwashawishi huko Mo Foundation ili Kikwete apewe tuzo hiyo.

NB:
 
Masatu, najua wewe ni mpiga debe mzuri tu wa Serikali za CCM lakini inapofika suala la uzalendo/utaifa ningekuomba uweke mbali mapenzi yako kwa Vyama na kutanguliza utaifa. Kwa yote mabaya Mkapa aliyofanya yaweza kuwa mapungufu ya kibinadamu maana hakuna aliye mkamilifu, lakini inapofika kuwa implicated kwenye hujuma ya kujiuzia Kiwira Coal Mine (wizi) kwa bei chee hapo inakuwa ngumu kusema kuwa huo ni upungufu wa kibanadamu maana hiyo ni hujuma kwa Uchumi wa Taifa na Watanzania.

Nikuulize swali; Je, Mkapa amekanusha hiyo tuhuma ya kujiuzia KCL na kama amekanusha hivi ni kweli kuwa KWL si mali yake? Kama angejiuzia kwa bei ya soko (kitu ambacho ni kinyume cha maadali ya uongozi) tungeweza kusema kuwa bado alikuwa kiongozi mzuri. Tena unakumbuka mauaji ya Pemba Zanzibar baada ya Uchaguzi wa 2000? Unajua kuhusu uchaguzi wa Zanzibar ulivyoendeshwa na hata kupigiwa kelele na Waangalizi wa Kimataifa na wa ndani kuwa haukukidhi matakwa ya kuwa Uchaguzi huru na wa Haki? Uongozi bora wa Mkapa uko wapi hapo? Kwenye kuruhusu kuchotwa kwa mabilioni ya EPA kugharamia kampeni za CCM?

Pili, hata hivyo sitashangaa siku akija kupata hiyo tuzo maana kwa kawaida wanaotoa hiyo tuzo si Watanzania na uzoefu unaonyesha kuwa ni Wafadhili na Watu wa nje ndiyo huwasifia viongozi wetu (hawawajui sana) nao viongozi wetu hulenga kujionyesha kwa watu wa nje kuwa wao ni viongozi bora ili kuwapendeza hao Wafadhili wao.

Ibrah,

Shukran kwa mchango wako kwenye thread hii.

Labda tu nianze kwa kuweka rekodi sawa mimi ni mpiga debe wa serikali za CCM. Im open minded person nakosoa na kusifia pale ninapoona sahihi. Kama kwa kufanya hivyo ndio ninaakuwa mpiga debe wa CCM so be it.

Kuhusu habari za Kiwira mimi nisingependa kuingia kiundani kwani kinachoendelea ni shutuma za vyombo vya habari ambavyo hazija thibitishwa na chombo chochote huru (kisheria) Labda tu niharakishe kusema sikanushi kama Mkapa anamiliki Kiwira au laa lakini kubwa zaidi hata kama anamiliki hizo habari za "kujiuzia" hazina mashiko na ni pure speculations.

Swali kuwa mbona hajakanusha, my frriend vyombo vya habari kazi yao ni habari pasipo na habari kimsingi hawana kazi hivyo lazima wawe na habari ili wa survive na infact hiyo ndio carrier yao. Lakini Mkapa ni Rasi mstaafu kwa sasa anaishi kwa pensheni ( kwa alivyosema mwenyewe ) Sasa ikiwa atajiingiza katika shughuli za kukanusha kila kinachoandikwa na vyombo vya habari ni sawa na ku dance according to their tune atakanusha mangapi?

Ama kuhusu mauaji ya Pemba hapa hoja yako ina nguvu na pengine hilo linaangukia katika awajibikaji wa uongozi. Ikumbukwe Mkapa alikuwa nje ya nchi na aliekuwa anakaimu Urais alikuwa marehemu Omari Juma. Hata hivyo Mkapa anawajike kwa makosa ya waliofanya watu wa chini yake na pengine hilo ni miongoni mwa mapungufu ya kibinadamu ya Mkapa.

All said and done Mkapa rekodi nzuri ya Mkapa kwenye ujenzi wa miundo mbinu imara, mipango kamambe ya ya maendeleo ya shule za msingi na sekondari, makusanyo ya kodi, utawala bora, vitendea kazi kwenye ofisi za serikali nk itabaki kuwa ni tunu kwa watanzania na vizazi vijavyo.

Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni....
 
..nakubaliana na mchangiaji aliyependekeza tuzo hii isiwe inatolewa kila mwaka.

..wajaribu kuitoa kila baada ya miaka 5 ili tuwe na washindani wengi zaidi.

NB:

..Salim Salim ni mmoja kati ya majaji wanaochagua mshindi.

..nategemea atatumia ushawishi wake kuwezesha tuzo hiyo kwenda kwa Mkapa au Kikwete.
....Mh! Hata kama hawana vigezo vya kupewa hiyo tuzo wapewe tu kwa kuwa Salim yumo kwenye jopo la majaji???? No man!!!!haijatulia hiyo....
 
Zawadi pekee anayostahili Jambazi Benjamin William Fisadi Mkapa ni kusekwa jela yeye na mke wake na kunyang'anywa mali zao zote. Nashangaa hiyo taasisi ya Mo Ibrahim inapoteza muda wake kufanya uchambuzi wa jina la Fisadi Mkapa.
 
Ukisoma hii thread unagundua uelewa wetu sisi watanzania/Waafrika.

Hivi kweli kwa nchi maskini za kiafrika, kuna mtu anaweza kusema kwamba kuna utawala wa sheria na haki? Kuna wanaotaka tuamini kwamba Mkapa anaweza kuonekana mwenye hatia endapo mahakama itasema hivyo? Jamani tusizidhulumu nafsi zetu. Kama serikali imeshindwa kuwashtaki wezi wa EPA, waliosaini mikataba mibovu, waliotulaza gizani na wengine lukuki waliohujumu uchumi wetu na maisha ya watanzania...tunaweza kuiamini kwamba inaweza kumchukulia hatua RAIS MSTAAFU? Lets be realy!

Ni kiongozi gani Africa ameshawahi kuwajibishwa kwa makosa ndani ya nchi yake? THANK God WAZUNGU wameamua kutuasaidia katika hili (Taylor and maybe Bashir!). So far mimi natamani kwenye review Conference ya mkataba wa Roma mwakani (mkataba unaoanzisha mahakama ya ICC) waweke corruption as a crime against humanity!

Kama alivyosema jamaa hapo juu, Mkapa ni kiongozi bora kama ukimlinganisha na viongozi mafisadi ambao ndo wamejaa Africa. Definetely..ukimlinganisha na Kibaki, Kabila, Mseveni nk..Mkapa will emerge as a winner. Ni kama mtu yeyote akijilinganisha na mgonjwa aliye hospitali..lazima utaonekana mwenye afya!

Watu wanasema Mkapa aliweka miundo mbinu na brah brah kibao..kwani aliomba uraisi afanye nini? after all si ni kodi zetu tunalipa? I say it Mkapa let us down. Aliiba na ushahidi upo..kuanzia na umaskini unaowatafuna watanzania. Kila siku hapa JF tunachambua mikataba ya madini..tumeona tulivyouzwa kama taifa...kwani Mkapa hakujua? Guys Mkapa has done more damage to our country than our collective imagination can ever comprehend!

Wakuu nadhani mnapoandika humu, muwe conscience na uwezo wetu wa kufikiri! Kuna watu humu wana akili zao. kama unaona unataka kuchezea akili za watu kwa kumsifia Mkapa nk..ni vema ukaenda kwenye blog za Michuzi nk..hapa watu tunajadili msatakabali wa taifa.!

Iam really dissapointed kuona kwamba na uwezo wetu wa kufikiri bado tunapima viongozi wetu kwa standards zile zile za kifisadi!

Huwezi linganisha utawala wa Mogae au Chisano na wa fisadi Mkapa! Chisano kapokea nchi ikiwa zero kabisa! nenda kaone mzee alivyojitahidi.

Tanzania viongozi wetu wanakuwa na nafasi na mandate ya kuwasaidia wananchi wao..lakini ndo hivyo wanapokezana vijiti kuiba!

Yes, Mkapa ana mazuri yake, lakini by far..ni rais ambaye alishindwa kutumia nafasi yake kuiweka nchi yetu kwenye dira stahiki! na JK so far ndo amekuwa worse! Tunamkumbuka Mkapa (kama wapo wanaomkumbuka) kwa sababu his alternative is worse!
 
hii award ina mapungufu makubwa sana... kama alikosa mwaka jana iweje awe tena kwenye kuiwania? hii award haitakiwi kuotolewa kila mwaka maana mwisho wa siku watakuwa wameisha marais bora naitaenda kwa ambae hafai. inatakiwa itolewe labda kila baada ya miaka mitatu ili tuwe tumepata wastaafu wapya.... na ikiwezekana mara nyingine mshindi akosekane

Hii njemba ina pesa za mchezo nyingi tu, hivyo kila mwaka lazima mshindi apatikane hata kama wananchi wa nchi anakotoka Rais huyo hawakubaliani na Rais wao kupewa zawadi hiyo. Mimi naona huyu Mo Ibrahim hiyo pesa yake angeelekeza kwingine kwa mfano kusaidia maskini katika nchi mbali mbali za Afrika, kupunguza magonjwa yanayowaua Waafrika wengi n.k.badala ya kutafuta umaarufu ambao tayari anao.
 
Back
Top Bottom