MO,MANJI,BAKHRESA MSIBA HAMJAUSIKIA

MO,MANJI,BAKHRESA MSIBA HAMJAUSIKIA

Kuna watu wanadhani kuwa MO alirudi uraiani kwa sababu ya kelele zao

Hawajui kuwa Bank zilivunjwa kurudisha uraiani mtoto wao

Mbona kelele hizo hazijawarudisha wengi uraiani?
 
sijwasikia social media TV media Wala karimjee kumuaga mpendwa wetu mbona wengine tunajitoa mkipata matatizo .sio poa

SUBASHI PATEL: KIFO CHA MENGI NIPIGO KWA ... - YouTube
 
Hakuna cha ajabu hapo,Dewj muhindi Baharesa mwarabu {siyo kwamba sijui kama ni mpemba hasha ila wapemba wengi wakipata cent nao hujikuta waarabu} so maybe wamembagua kwa ngozi yake.

Ni maoni yangu,yanaweza kuwa sahihi au yasiwe sahihi.
 
Hawa ni Watanzania tu wa kuzaliwa sina maana ya kuwa mbaguzi ila ndio ukweli mchungu
 
Watanzania tuache upumbavu wa kifikra. Hujasikia wewe lakini sio lazima kila kitu kiwe public, watu wengine hawapendi kiki hasa kwenye mambo kama misiba.

Salamu zao za rambirambi utajuaje kuwa wamezifikisha kwa familia ya marehemu privately?

Acheni ujinga fanyeni mambo ya msingi.
Sio ujinga mbona wakienda kula bata na watoto wao wanatuonyesha ??? Watuonyeshe UTU pia tuujue
 
Mtoa mada acha kuwa na fikra za kitumwa hizo, kwani wasipohudhuria hao (mo, bakhresa na Manji) maiti haitozikwa? Au wamekwamisha utaratibu mzima wa mazishi ya MENGI? uwepo wao au kutokuwepo hakuna athari yoyote katika msiba wa MENGI
 
watu wanaishi kwa Code ... we tulia waachie mambo yao .. hao na wewe mnaishi dunia mbili tofauti ... na fasiri yako ya matukio kama haya ni tofauti sana na hao jamaa wanavyoya tafsiri
Great comment!
 
Kwenye Islam,kuaga mwili hakupo aslan. Hivyo unaweza kukuta sababu ni hizo. Kuzika sawa,ila kwenda kuaga mwili kwa sheria za Uislam,haipo. Sasa kwa mtu kama mzee Bakhresa,sidhan kama anaweza kwenda kuaga mwili,japo anaweza kwenda kuzika. Kuaga mwili na kuzika ni vitu tofauti.
Kikwete ,Mwinyi,Gharib Bilal ,Othman Chande ,Juma Mwapachu ,Samia Suluhu ...Hawa ni Wapentekoste ?
 
Mkuu mtu anapofariki unatakiwa umuombee kwa mungu/allah kwa moyo wako wote amsamehe makosa yake apumzike kwa amani tu ndo msaada mkubwa wa kuufanya kwa marehemu..hizi za social media na kuonyesha ulifanyaje msibani ni zetu binadamu tu,allah hazijui anajua juu ya moyo wako msiba ulivyokugusa
 
Mimi mbona sikuudhuria na siulizwi...!!

Au nini maana ya Luninga na kurusha maombolezo mubashara..!

Kila mmoja ange hudhuria unadhani pangetosha hapo.

Acheni kasumba..
 
sijwasikia social media TV media Wala karimjee kumuaga mpendwa wetu mbona wengine tunajitoa mkipata matatizo .sio poa
Tanganyika ya sasa sio ile ya 2000 sasa hivi watu hawaend katika mikusanyiko hovyo,
Sasa hivi watu hivi watu bila taarifa za kina juu ya usalama wao inakuwa vigumu kutokea so wanatuma wawakilishi,Kuna mtoto wa Bakhresa alionekana pale kwa mengi nadhani ni kawakilisha familia na kampuni.
Yawezekana usiwaone hao watu katika msiba lakini wakawa wamehusika kwa kiasi kikubwa sana,kumbuka hata katika msiba wa Bosa Ruge kuna watu walikuwa busy sana na ule msiba yan kila jambo pale msibani walionekana wao ila mwishowe katika zile shukran za pekee za watu watano hawakutajwa, baadhi ya waliotajwa hawakuonekana msibani wala popote/walihusika katika msiba kwa 99% bila kujionesha,Mtu anaweza asiwepo pahala ila msaada wake ukawa mkubwa sana kuliko mimi na wewe uliepo eneo la tukio husika.
 
sijwasikia social media TV media Wala karimjee kumuaga mpendwa wetu mbona wengine tunajitoa mkipata matatizo .sio poa
sijui kwa hao matajiri wengine, ila familia ya bakhresa siku ya kwanza tu ilituma muwakilishi nyumba kwa mzee mengi pale mikocheni kwenda kutoa mkono wa pole kwa wafiwa.

na muwakilishi huyo ni abubakar bakhresa ambaye ni mtoto wa mzee said bakhresa mmiliki wa bakhresa group.

kuhusu bakhresa family, hawa jamaa mambo yao ni kimyakimya sana, hawapo friendly na camera za media japo wao wenyewe wanamiliki tv station kubwa hapa east africa.

nina hakika pale karimjee abubakar bakhresa alikuwepo ila hakutaka attention ya media. na hata huko machame watakuwa wametuma mtu wao, ila watu wa media sio rahisi kujua.
 
Watanzania tuache upumbavu wa kifikra. Hujasikia wewe lakini sio lazima kila kitu kiwe public, watu wengine hawapendi kiki hasa kwenye mambo kama misiba.

Salamu zao za rambirambi utajuaje kuwa wamezifikisha kwa familia ya marehemu privately?

Acheni ujinga fanyeni mambo ya msingi.
kwahiyoo msiba nao ni private mkuu.........

hard stone heart......
 
Watu tunafuatilia sana maisha ya watu..., hujui kwanini hawakwenda au kama kweli hawakwenda, hata kama hawakwenda kila mtu ana haki ya kujua la rohoni mwake hata kama wewe unamuona fulani ni mzuri mwingine anaweza asimuone kama wewe unavyomuona.., pia vile vita vya Rostam na Mengi sidhani kama leo hii Rostam anaweza kusema huyu jamaa alikuwa mtu mzuri..., Mara nyingine ulitafuta sana kitu unaweza ukakiona hata pale ambapo hakipo....

Kuhudhuria misiba au kulia sana sio kwamba ndio mtu ameguswa sana wengine siku hizi wanatumia hii issue kama fursa ya kuuza sura...

By the way wewe ulikuwa unaomboleza au unachunguza nani yupo na nani hayupo ?
 
sijwasikia social media TV media Wala karimjee kumuaga mpendwa wetu mbona wengine tunajitoa mkipata matatizo .sio poa
Inawezekana wana sababu zao. Lakini mengi wala familia yake sijawahi iona msiba wowote kitaa kwetu. Old saying "no coincidence in intelligence"
 
Back
Top Bottom