MO,MANJI,BAKHRESA MSIBA HAMJAUSIKIA

MO,MANJI,BAKHRESA MSIBA HAMJAUSIKIA

Yaani katika yote ya kuandika ndo ukaona uandike hili ndo la maana. Habari za nani kahudhuria nani hakuhudhuria zina faida gani kwa maisha yako? ..😀😀😀😀😀
 
Mi kuzika naenda lakini Kuaga Hapana.
 
sijwasikia social media TV media Wala karimjee kumuaga mpendwa wetu mbona wengine tunajitoa mkipata matatizo .sio poa
Nimemuona Patel peke yakee
Ooo hao wanafurahia mkuuuu maana mpianzani wao kibiasharaa ndio ametanguliaa haswaa
 
Kuna watu wanatetea ujinga hapa Eti ushiriki sio lazima mtu afike msibani huo sio utamaduni wetu wa africa, tumefundishwa kuzikana ndio mana hata leo ndugu wa marehemu wanaweza wasishiriki kumzika marehemu ila atazikwa tu na community, Kama msiba mpaka mkuu wa nchi anahudhuria hao mabilionea wameshindwa nini? Tuache kutetea ujinga wangefika tu pale na kusaini kitabu walau waonekane
 
sijwasikia social media TV media Wala karimjee kumuaga mpendwa wetu mbona wengine tunajitoa mkipata matatizo .sio poa
Mengi inaonekana alikuwa na ugomvi na matajiri hawa wenye asili ya Asia . Inasemekana serikali ya zilizopo ilikuwa ikiwapa fursa hawa waAsia lakini sio watu weusi Kwa kuhofia wakiwa na pesa wanaweza kuipindua serikali. Kwahiyo Reginald Mengi alikuwa anapinga hiyo Tabia Katika uhai wake kuanzia kipindi cha mwl Nyerere alipowabana watu weusi wasiwe na Mali. Mengi ilimuwea rahisi kuanza kutengeneza utajiri waje kipindi cha Mzee Ruksa . Lakini inaonekana kwamba viongozi wengi hawakumpenda wakihofia anaweza kuja kugombea Urais kutokana na jina lake kuwa kubwa na kuweza kushinda. Kumbuka ugomvi wa Reginald Mengi na Manji, ugomvi wa Rostam Aziz na Mengi .kuna kipindi serikali ya awamu ya tatu walitakaga kumfikilisi. Hata hivyo hawa matajiri wenye asili ya Asia hawakumpenda Mengi. Kwasababu alikuwa anawachana laivu kwamba serikali inawapendelea kuwapa fursa za kiuwekezaji kuliko watanzania weusi. Awa matajiri wekiAsia wote wamepata hela Kwa njia za mkato Kwa kubebwa na viongozi wetu
 
Mo aliachiliwa alipotekwa sio kwa sababu ya kelele za watu. Ni kuwa walipanga wamteke,wamalizane naye Kisha wamuachie.

Hizo kampeni hazijafanya kazi kwa watu kibao.
Serikali hii haisikilizi maoni ya watu kwa vile inaamini watu hawawezi kuifanya chochote
 
Kuna watu wanatetea ujinga hapa Eti ushiriki sio lazima mtu afike msibani huo sio utamaduni wetu wa africa, tumefundishwa kuzikana ndio mana hata leo ndugu wa marehemu wanaweza wasishiriki kumzika marehemu ila atazikwa tu na community, Kama msiba mpaka mkuu wa nchi anahudhuria hao mabilionea wameshindwa nini? Tuache kutetea ujinga wangefika tu pale na kusaini kitabu walau waonekane
Ndio ujue Wahindi sio ndugu zenu wamekuja kutafuta hela tuu. Mengi alikuwa mpinzani wao mkubwa kubishara kwahiyo hawampendi. Awamu hii nafikiri Wahindi wanaisoma namba serikali zilizopita waliziweka mifukoni mwao. Walijua pesa itawalinda
 
sijwasikia social media TV media Wala karimjee kumuaga mpendwa wetu mbona wengine tunajitoa mkipata matatizo .sio poa
Kwenye Islam,kuaga mwili hakupo aslan. Hivyo unaweza kukuta sababu ni hizo. Kuzika sawa,ila kwenda kuaga mwili kwa sheria za Uislam,haipo. Sasa kwa mtu kama mzee Bakhresa,sidhan kama anaweza kwenda kuaga mwili,japo anaweza kwenda kuzika. Kuaga mwili na kuzika ni vitu tofauti.
 
Nyie wengine showing off nyingi na kujipiga selfie kumbe wenzenu ndio wamekodi ndege ya kwenda KIA.. Usikute hata huo ubwabwa mliokuwa mkila hapo msibani na dada yako Joyce Kiria bill analipa Mo
 
Watanzania tuache upumbavu wa kifikra. Hujasikia wewe lakini sio lazima kila kitu kiwe public, watu wengine hawapendi kiki hasa kwenye mambo kama misiba.

Salamu zao za rambirambi utajuaje kuwa wamezifikisha kwa familia ya marehemu privately?

Acheni ujinga fanyeni mambo ya msingi.

Tunasafari ndefu sana kama taifa kiwango cha ujinga wa mitandao ni kikubwa sana hata tunakoelekea sijui itakuwaje Mungu atusaidie sana
 
Waarabu na wahindi wote ni maboya tu, kwanza hawa tuhusu achaneni nao tu
 
watu wanaishi kwa Code ... we tulia waachie mambo yao .. hao na wewe mnaishi dunia mbili tofauti ... na fasiri yako ya matukio kama haya ni tofauti sana na hao jamaa wanavyoya tafsiri
Heshima kwako mkuu, Jibu lako ni wachache wataelewa
 
Inaonekana walikuepo Ila sio watu wa maonyesho kama wabongo tulivyo. Ingekuwa ajabu sana wasingefika msibani
mbona niliwaona mo,manji,bakhresa na Yule Patel.
wabongo kwa lawama hatujambo.
 
Tunasafari ndefu sana kama taifa kiwango cha ujinga wa mitandao ni kikubwa sana hata tunakoelekea sijui itakuwaje Mungu atusaidie sana
Aliye mitandaoni ana nafuu/advantage kulinganisha waliobaki kwa hiyo hizi ndio mbegu bora tulizonazo.

Kuna mwingine tulipopata habari za msiba fikra zake zikampeleka kuwaza kuilinganisha "amsha amsha" ya msiba wa clouds media na utakavyokuwa huu.
 
Back
Top Bottom