Mnyukano mkubwa Ofisi ya Rais: Sefue vs Hosea

Mnyukano mkubwa Ofisi ya Rais: Sefue vs Hosea

Ni kweli mkuu ikulu kusafisha uvundo kama ule ni janga. Kalidharaulisha bunge, takukuru , polisi n.k inabidi sefue aachie tu ngazi. Unajua huyu ni tofauti na yule aliyeondoka luhanjo. Luhanjo alikuwa anaongea mara chache sana.

Luhanjo kweli hakuwa anaongea sana lakini yeye na mwenzie Jairo walikuwa very corrupt na ndio maana wameweza kununua mashamba makubwa huko Njombe!! Luhanjo alitumia weakness ya Ikulu kujilimbikizia mali; kajenga mahekalu hukoTegeta etc.

Luhan
 
Ni kweli mkuu ikulu kusafisha uvundo kama ule ni janga. Kalidharaulisha bunge, takukuru , polisi n.k inabidi sefue aachie tu ngazi. Unajua huyu ni tofauti na yule aliyeondoka luhanjo. Luhanjo alikuwa anaongea mara chache sana.

Luhanjo kweli hakuwa anaongea sana lakini yeye na mwenzie Jairo walikuwa very corrupt na ndio maana wameweza kununua mashamba makubwa huko Njombe!! Luhanjo alitumia weakness ya Ikulu kujilimbikizia mali; kajenga mahekalu hukoTegeta etc.
 
Hivi mnyukano maana yake hasa ni ipi mbona maneno haya yanatumika kihuni tu sijaona huo mnyukano unaousema wewe.

Mkuu bado upo. Naona umebakiza siku tatu za kujidai. Sijui safari hii utalamba miguu ya nani
 
Hosea yupo sahihi Mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusafisha mtu
 
TAKUKURU haina tofauti na JOKA la kibisa(hutumika kuchezea ngoma) linatisha ukiliona lakini halina madhara yoyote kwa mtu jasiri!
 
Mkuu Chakaza halafu mkubwa wao wa kazi Kikwete kauchuna kimyaaaaa bila kutia neno kwamba katika hili sakata ni nani kati ya Sefue na Hosea anayesema kweli kuhusu hili sakata. Kweli Rais tunaye!
 
Last edited by a moderator:
Kuna vyombo viwili hapa vinahusika na swala moja. Ofisi ya Miiko na Maadili ipo chini ya rais na Sefue anazungumza kama mwakilishi wa Ofisi ya rais na TAKUKURU nao wana Uchunguzi wao. nadhani Sefue alichofanya ni kuwasafisha katika hoja na miiko na maadili kuwa ivongozi wale hawana makosa.

Sasa inapokuja swala la TAKUKURU kuwa bado wapo ktk uchunguzi inatoa picha mbaya zaidi kwa serikali na maamuzi yao kwa sababu ilitakiwa Ofisi ya maadili isuburi uchunguzi wa TAKUKURU kabla ya ufikia maamuzi yake. Aidha Sefue kapandishwa mkenge kwa kuambiwa uchunguzi umekwisha ama kuna uvunano mkubwa baina ya vyombo hivi viwili. Kifupi tu ni kwamba tume ya Miiko na Maadili ilitakiwa kuwa kamati ya Bunge na sio tume ofisi ya rais kwa sababu kazi yake ni kuisimamia serikali hivyo haiwezi kuwa chini ya serikali. Bora hata ingekuwa chini ya CAG ili kuharakisha utelekezaji..
 
Hosea ana ushahidi wa jinsi maswi alivyonunua nyumba afrika kusini kwa fedha za escrow, hosea ana ushahidi wa sefue kununuliwa nyumba new york kwa fedha za escrow, hosea ana ushahidi wa jinsi werema alivyowekewa fedha za escrow kwenye mojawapo ya akaunti yake iliyoko afika kusini, ni suala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi.
JF kwa tetesi ni kiboko. Halafu mtu anaongea kwa uhakika utadhani kweli ana ushahidi.
 
Hosea yupo sahihi Mahakama pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusafisha mtu
Mahakama haiwezi kumsafisha mtu ambaye hajafunguliwa mashtaka. Utawala wa sheria unasema mtu hana hatia mpaka pale mahakama inapothibitisha pasipo shaka yoyote kuwa kavunja Sheria. Kwa hiyo mpaka sasa Maswi na Muhongo hawana hatia na ni wasafi mpaka hapo mahakama itakapoamua vinginevyo iwapo kweli kesi zitafunguliwa.
 
Baada ya siku kadhaa zilizopita Katibu mkuu kiongozi kutoka ofisi ya Rais kujitokeza na kuwasafisha viongozi wa serikali waliohusishwa na sakata la Tegeta Escrow.

Kiongozi mwingine kutoka ofisi hiyohyo ya Rais naye amejitokeza na kumpinga Sefue kwa kusema uchunguzi unaendelea na mwenye mamlaka ya kusafisha watuhumiwa ni mahakama pekee tuu.

Kiongozi huyo Bw Hosea ambaye ndiye mkuu wa Takukuru ndiye hasa anayeonekana mhusika mkuu wa kushughulikia sakata hilo.

Kitendo cha viongozi wakuu hao kutoka ofisi ya Rais kutoa matamko ya kupingana hadharani kinatia mashaka juu ya namna ya utendaji wa ofisi hiyo ya juu kabisa nchini.

Chanzo; Magazeti ya leo

=========

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema uchunguzi dhidi ya vigogo wa kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow unaendelea.

Kauli hiyo ilitolewa Dodoma jana na Mkurugenzi wa Takukuru, Dk . Edward Hosea alipokuwa akijibu maswali ya wabunge waliohudhuria semina ya Chama Cha Wabunge Wanaopambana na Rushwa (APNAC).

Kauli ya Dk. Hosea ilitokana na swali la Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), aliyetaka kujua kama taasisi hiyo ilishiriki kwa namna moja au nyingine kuwasafisha watuhumiwa wa Escrow.

Sendeka alihoji ni kwa vipi taasisi nyingine (Ikulu), inawasafisha watuhumiwa wa kashfa hiyo wakati Takukuru inaendelea na uchunguzi wake kitendo ambacho kinaweza kuharibu uchunguzi.

“Au kwa kuwa Takukuru na nyie mpo ofisi moja Ikulu mliwasiliana kuwasafisha watuhumiwa hao? Kama hamkushiriki kuwasafisha mseme Bunge hili kabla halijamaliza muda wake liwasaidie,”alisema Ole Sendeka.

Akijibu swali hilo, Dk. Hosea alisema taasisi yake haijamsafisha yeyote na bado inaendelea na uchunguzi wake.

“Sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria siyo kwa maelekezo kutoka kwa mtu yeyote… waliofikishwa mahakamani hatuwezi kuwasafisha na wale ambao bado uchunguzi unaendelea,”alisema.

Alisema Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue aliwasafisha watuhumiwa hao katika eneo lake na kwamba Takukuru inaangalia eneo lake.

Itakumbukwa hivi karibuni, Sefue alisema imebainika aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi aliyesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yake, wote hawana hatia.

Rushwa kwa mitandao
Dk.Hosea pia alitoa onyo kwa wagombea wakiwamo wa nafasi za ubunge waliojiandaa kutoa rushwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kutuma fedha kupitia mitandao za kiganjani.

“Kwa sasa, Serikali imetuwezesha kudhibiti rushwa kwa njia ya mtandao, tunaye mtaalamu ambaye amesomeshwa kwa ajili hiyo, tunayo mitambo ya kisasa.

“Nawaambia wale waliojipanga mwaka huu kutoa rushwa kwa kutumia M-Pesa, Tigo- Pesa mwaka huu mjue mtaumia sana,”alisema.

Akizungumzia wagombea hasa wa nafasi ya urais ambao wameonyesha nia na baadhi wameanza kuchangia michango mbalimbali ikiwamo kwenye harambee, Dk.Hosea alisema kuwakamta watu hao inahitajika busara.

“Unapowakamata watu kama hao inabidi utumie ushahidi wa kutosha, hatumuogopi mtu, hata hivyo suala la uchaguzi ni nyeti na linasimamiwa na vyombo vingine pia,”alisema.

Aliwataka wabunge wenye malalamiko ya watu wanaotoa rushwa kwa wananchi kwenye majimbo yao wawasiliane na ofisi yake.

Alisema kwa wale wabunge wa majimbo wanaruhusiwa kutoa misaada ya maendeleo kwa wananchi wao, lakini kwa mujibu wa Sheria ya Gharama ya Uchaguzi, hairuhusiwi kutoa misaada hiyo kwa mtu mmoja mmoja.

Baadhi ya wabunge walilalamikia baadhi ya walioonyesha nia ya kugombea katika majimbo yao wakisema wanajipitisha na kugawa vitu mbalimbali kwa wananchi.

Mbunge wa Dole, Sylvester Mabumba (CCM) alitaka kujua nafasi ya Takukuru kwa Watanzania walioonyesha nia ya kugombea ambao wengine wameanza kuendesha harambee na kutoa misaada kanisani na misikitini.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy, (CCM) alitaka kujua jinsi Takukuru inavyoshughulikia rushwa ya ngono na rushwa kwa njia ya mtandao.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) aliitaka taasisi hiyo iwashughulikie wabunge wanaotoa misaada ya fedha nyingi katika majimbo yao tofauti na kipato chao.

Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), alihoji kama taasisi hiyo ilishawahi kumkuta na hatia mgombea yeyote kwa kutumia Sheria ya Gharama ya Uchaguzi.

Alitaka pia kujua kama Takukuru ina uwezo wa kumuondoa mgombea wa urais hasa CCM iwapo atathibitika katoa rushwa.

Awali akifungua semina hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika, aliitaka taasisi hiyo ianze kazi sasa isisubiri hadi Oktoba kwa kuwa majimboni tayari rushwa imeanza kutolewa.


Chanzo: Mtanzania

Ccm ni kundi la komedi la futuhi
 
Tume gani na iliundwa na nani ?? wakina nani waliounda tume na waliteuliwa na nani? na hadiju za rejea alitoa nani? na ripoti ya hiyo tume iko wapi??

Mwaka huu tutashuhudia mengi kutoka ccm
 
Mkuu Chakaza halafu mkubwa wao wa kazi Kikwete kauchuna kimyaaaaa bila kutia neno kwamba katika hili sakata ni nani kati ya Sefue na Hosea anayesema kweli kuhusu hili sakata. Kweli Rais tunaye!

Bora mkuu BAK umeliona hilo. Hii inaleta ukakasi wa aina fulani. Iweje wateule wake tena kutoka ofisi yake watofautiane naye akae kimya? Hana maamuzi?
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
...labda ndio kishajichokea kama alivyosema hivi karibuni anasubiri miezi minne iliyobaki ikatike akalime mananasi "na uhifadhi wa wanyama wetu kwenye mbuga za wanyama" Anajua Watanzania hatuna lolote la kufanya.

Bora mkuu BAK umeliona hilo. Hii inaleta ukakasi wa aina fulani. Iweje wateule wake tena kutoka ofisi yake watofautiane naye akae kimya? Hana maamuzi?
 
Back
Top Bottom