Mnyukano mkubwa Ofisi ya Rais: Sefue vs Hosea

Mnyukano mkubwa Ofisi ya Rais: Sefue vs Hosea

Hata Sefue awasafishe kiasi gani, Hawa safishiki wamesha fubaa
Tatizo bado lipo kwa watendaji wakuu ofisi ya Rais kwa nini wanyukane hadharani na ofisi hiyo ya Rais isimchukulie hatua aliyepotoka kati yao?
Jee hawa hawaoni kuwa wanawafanya wasiiamini tena ofisi hiyo katika kauli zake kwani zinakuwa sio za ofisi tena bali Individuals statement as they wish
 
Hivi mnyukano maana yake hasa ni ipi mbona maneno haya yanatumika kihuni tu sijaona huo mnyukano unaousema wewe.

Mnyukano wa mawazo maana yake ni kutofautiana mawazo, yaani Hosea ametofautiana mawazo na Balozi Sefue.
 
tunasubiri majina ya stanbinc bank.kuna mtia nia ya urais kajichotea kupitia stanbinc
 
Tatizo bado lipo kwa watendaji wakuu ofisi ya Rais kwa nini wanyukane hadharani na ofisi hiyo ya Rais isimchukulie hatua aliyepotoka kati yao?
Jee hawa hawaoni kuwa wanawafanya wasiiamini tena ofisi hiyo katika kauli zake kwani zinakuwa sio za ofisi tena bali Individuals statement as they wish

Na mkuu wa nchi alivyo dhaifu atabaki anacheka cheka tu.
 
Sefue hajamsafisha mtu. Alichokifanya ni kutangaza matokeo ya uchunguzi uliofanywa na tume husika.
Tume ni kina nani wako wapi...tume ya Warioba inajulikana, tume ya Mwakyembe na wenzie inajulikana...ripoti ya tume inasomwa na nani...Warioba alisoma ripoti yake mwenyewe na kikosi chake, vivyo hivyo kwa Mwakyembe nae...sasa hii ya ESCROW na TOKOMEZA mmmhh..jamani mbona Sefue anawapa kazi sana Wanaccm kuanza kusafisha vitu ambavyo Wananchi walishaanza kusahau.

Haya chacha uku kunaitwa bomoa bomoa Mama tutajenga kesho...japo kwa wenye ufahamu si tatizo sana cha msingi ni kuwaengua kimya kimya waliosafishwa wasishiriki siasa za uchaguzi kupunguza ATOMIC Bom ambalo laweza zaliwa ghafra pasipo kutalajiwa...uku kuna RICHMOND bado imemngangania mtu HAPUMUI WALA AEHEMI yukp ICU sasa wanaongeza ESCROW na TOKOMEZA....maweee watu wanaweza kuludi mpaka kwenye EPA binadamu bila huwa wanatabia ya kupumua [Relief] yani kwa kuwafanya yale yalio pita yasikumbushiwe na kulundikwa kwa wakati mmoja [Kapu Moja la Mayai].

Sasa kwa kusanya lundo moja la mayai RICHOND-Lowasa, TOKOMEZA-Nchimbi na wenzie, ESCROW-Muhongo na wenzie wakawa ndani ya kapu moja la mayai HAPA NDIO kweli CCM inaweza kuwapa nafasi Wananchi waka REACT kwa hamaki...na daima maamuzi ya ghafra uwa yana madhara sana.Muhemuko wa ghafra kwa SABABU ya HASIRA unaweza kuleta MAJANGA kwa TAIFA.

Wananchi wakiwa triggered na FACT ambazo kidogo wanazo wakaja kushibishwa na FACT chache na kukamilisha kitu kizima cha ufahamu wao hakika MUZIKI wake AMANI ya NCHI itakuwa mashakani.

Hii habari ya watu wako kwenye RICHMOND, ESCROW, EPA, TOKOMEZA TUPA KULE.....usiweke karibu na Wananchi chama chao cha CCM kitakuwa na AUENI ya kupumua kwenye UMMA.Uchaguzi sio kupoteza muda kumsafisha NANI kafashanya nini Uchaguzi ni kunadi sera za vyama na kuwaconvince Wananchi kuwa Wakipewa NAFASI watawajibika kwa Wananchi kuwaletea maendeleo.

Hii habari ya kumpandisha mtu jukwaani anatakiwa kutumia saa moja na nusu kujieleza na kunadi sera za chama chake matokeo anatumia Saa zima Kujisafisha na bado Wananchi wanamshambulia kwa maneno, kisha anatumia nusu saa kunasi sera.Kesho front line za magazeti zinasema ''MWANAFODODO ASEMA AKUWEKA SAHIHI YEYE KWENYE DOCUMENT YA RICHMOND, YA ESCROW, YA EPA, WALA YA TOKOMEZA''.Wakati ukweli ni kuwa magazetini kesho yake yanatakiwa kusema ''MWANAFODODO ASEMA ELIMU YA CHUO KIKUU ITATOKA BURE KWA KILA MTANZANIA MWENYE UWEZO WA KUINGIA CHUO KIKUU''.au ''MWANAFODODO ASEMA WAKULIMA WATAPATA SOKO LA MAZAO YAO PALE PALE KIJIJINI''

Hayo ndiyo Watanzania wanapaswa kuandaliwa kuyapokea kwenye njia POSITIVE na sio NEGATIVE PERCEPTION.

Hii habari ya KUSAFISHA WATU IACHWE kwa faida ya CHAMA CHAO vinginevyo Maweeeee...
 
Wanatutania tu muajiri mkuu ni sefue , hata yeye Hosea anapopewa kazi karibu mkuu kiongozi ana weka maneno kama anafaa , Hosea anatutania tu aiseee .movie hapa ndio imeisha .
 
Mnyukano wa mawazo maana yake ni kutofautiana mawazo, yaani Hosea ametofautiana mawazo na Balozi Sefue.
Asante kwa kiumsaidia kufahamu tafsiri hiyo ya kawaida tuu. Nadhani ipo katika somo la kiswahili kidato cha pili. Hivyo GT wa JF akiwa haelewi hilo inatia mashaka
 
Wanatutania tu muajiri mkuu ni sefue , hata yeye Hosea anapopewa kazi karibu mkuu kiongozi ana weka maneno kama anafaa , Hosea anatutania tu aiseee .movie hapa ndio imeisha .
KUWA BOSI WAKE hakumfanyia kuwa sahihi kuingilia kazi yake!!!Bosi mwenye ufahamu kwa kujua watu hawa wanatuhuma Politically lakini jamii ina perception pia hawa watu wanatakiwa kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za rushwa kuhusika.Yeye Kama Boss kapewa ripoti na tume HARAKA za NINI kwenye kwenye MEDIA bila kuwasiliana na vikosi kazi vyake vingine kama PCCB, Mwanasheria Mkuu wa Serikali [AG], Mwendesha Mashitaka Wa Serikali [DPP] na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai [DCI], Mkurugenzi wa Usalama Wa Taifa apewe STATUS ya swala zima la Watuhumiwa KITAIFA kwa sasa likoje kabla ya ofisi yake aijaamua kuchukua jukumu la kusoma Taarifa ya KUSAFISHA WATUHUMIWA mbele ya UMMA.

Ndio maana Hosea kwa kuona ilo anakuja na hoja yenye mashiko....kama amesema ofisi yake aihusiki yeye aliisoma kwanini?Ni kwa heshima yake ndio maana kaamua kumcofront kwa style ya dialogue.Vinginevyo ingekuwa tume ndiyo iliyosoma habari hiyo basi nae angeenda kwenye vyombo vya HABARI na kusema kuwa TAASISI anayoingoza bado inaendelea na UCHUNGUZI wake pale pale kuwahusu watuhumiwa.
 
Huwa sioni mantiki ya kuunda Tume za Uchunguzi ilhali kuna Taasisi za Kiserikali ambazo zipo kwa ajili ya kazi hizo.
 
Huwa sioni mantiki ya kuunda Tume za Uchunguzi ilhali kuna Taasisi za Kiserikali ambazo zipo kwa ajili ya kazi hizo.
Hiyo ni dalili kuwa haziaminiki au jambo husika linawagusa na wao pia. Lakini mbaya zaidi ni hii ya wateule wakuu kuja na majibu yanayo kinzana hadharani na kutuacha wananchi tusijue lipi ni lipi
 
Hiyo ni dalili kuwa haziaminiki au jambo husika linawagusa na wao pia. Lakini mbaya zaidi ni hii ya wateule wakuu kuja na majibu yanayo kinzana hadharani na kutuacha wananchi tusijue lipi ni lipi

Wakati mwingine "wakubwa" hukimbilia kuunda Tume kwa kuwa "Hawaziamini" Taasisi za Kiserikali kuwa zitaweza "Kuwalinda"...
 
Wanabodi ktk magazeti ya leo tar 18-5-2015,kuna taarifa ndefu toka kwa mkurugenzi wa takukuru bw Edward Hosea akidai eti takukuru bado wanachunguza wizi wa fedha za tegeta escrow.

Ukweli ni kuwa hakuna uchunguzi unaoendelea hapo,pamoja kwamba Dr Hosea anajitahidi sana kupambana na wizi ktk taasisi mbalimbali hapa nchini hili la tegeta escrow, ikulu imeisha lifunga kwa taarifa aliyoitoa katibu mkuu kiongozi bw.Sefue Ombeni ktk vyombo vya habari.

Kama takukuru wanataka tuwamini basi wawataje wale waliobeba manoti kwa magunia pale ktk benki ya stanbic vingenevyo ni nja ya kusahaulisha wanainchi kwa hilo.

Nawasilisha.
 
Kwa utendaji huu wa ofisi ya juu kabisa nchini si ajabu sheria ya mitandao kupitishwa kwa kasi ya umeme. Wengi tutafungw
 
baada ya siku kadhaa zilizopita katibu mkuu kiongozi kutoka ofisi ya rais kujitokeza na kuwasafisha viongozi wa serikali waliohusishwa na sakata la tegeta escrow.

Kiongozi mwingine kutoka ofisi hiyohyo ya rais naye amejitokeza na kumpinga sefue kwa kusema uchunguzi unaendelea na mwenye mamlaka ya kusafisha watuhumiwa ni mahakama pekee tuu.

Kiongozi huyo bw hosea ambaye ndiye mkuu wa takukuru ndiye hasa anayeonekana mhusika mkuu wa kushughulikia sakata hilo.

Kitendo cha viongozi wakuu hao kutoka ofisi ya rais kutoa matamko ya kupingana hadharani kinatia mashaka juu ya namna ya utendaji wa ofisi hiyo ya juu kabisa nchini.

Chanzo; magazeti ya leo

=========

taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru) imesema uchunguzi dhidi ya vigogo wa kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya sh bilioni 300 kwenye akaunti ya tegeta escrow unaendelea.

Kauli hiyo ilitolewa dodoma jana na mkurugenzi wa takukuru, dk . Edward hosea alipokuwa akijibu maswali ya wabunge waliohudhuria semina ya chama cha wabunge wanaopambana na rushwa (apnac).

Kauli ya dk. Hosea ilitokana na swali la mbunge wa simanjiro, christopher ole sendeka (ccm), aliyetaka kujua kama taasisi hiyo ilishiriki kwa namna moja au nyingine kuwasafisha watuhumiwa wa escrow.

Sendeka alihoji ni kwa vipi taasisi nyingine (ikulu), inawasafisha watuhumiwa wa kashfa hiyo wakati takukuru inaendelea na uchunguzi wake kitendo ambacho kinaweza kuharibu uchunguzi.

“au kwa kuwa takukuru na nyie mpo ofisi moja ikulu mliwasiliana kuwasafisha watuhumiwa hao? Kama hamkushiriki kuwasafisha mseme bunge hili kabla halijamaliza muda wake liwasaidie,”alisema ole sendeka.

Akijibu swali hilo, dk. Hosea alisema taasisi yake haijamsafisha yeyote na bado inaendelea na uchunguzi wake.

“sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria siyo kwa maelekezo kutoka kwa mtu yeyote… waliofikishwa mahakamani hatuwezi kuwasafisha na wale ambao bado uchunguzi unaendelea,”alisema.

Alisema katibu mkuu kiongozi, ombeni sefue aliwasafisha watuhumiwa hao katika eneo lake na kwamba takukuru inaangalia eneo lake.

Itakumbukwa hivi karibuni, sefue alisema imebainika aliyekuwa waziri wa nishati na madini, profesa sospeter muhongo na katibu mkuu wa wizara hiyo, eliakim maswi aliyesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yake, wote hawana hatia.

Rushwa kwa mitandao
dk.hosea pia alitoa onyo kwa wagombea wakiwamo wa nafasi za ubunge waliojiandaa kutoa rushwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kutuma fedha kupitia mitandao za kiganjani.

“kwa sasa, serikali imetuwezesha kudhibiti rushwa kwa njia ya mtandao, tunaye mtaalamu ambaye amesomeshwa kwa ajili hiyo, tunayo mitambo ya kisasa.

“nawaambia wale waliojipanga mwaka huu kutoa rushwa kwa kutumia m-pesa, tigo- pesa mwaka huu mjue mtaumia sana,”alisema.

Akizungumzia wagombea hasa wa nafasi ya urais ambao wameonyesha nia na baadhi wameanza kuchangia michango mbalimbali ikiwamo kwenye harambee, dk.hosea alisema kuwakamta watu hao inahitajika busara.

“unapowakamata watu kama hao inabidi utumie ushahidi wa kutosha, hatumuogopi mtu, hata hivyo suala la uchaguzi ni nyeti na linasimamiwa na vyombo vingine pia,”alisema.

Aliwataka wabunge wenye malalamiko ya watu wanaotoa rushwa kwa wananchi kwenye majimbo yao wawasiliane na ofisi yake.

Alisema kwa wale wabunge wa majimbo wanaruhusiwa kutoa misaada ya maendeleo kwa wananchi wao, lakini kwa mujibu wa sheria ya gharama ya uchaguzi, hairuhusiwi kutoa misaada hiyo kwa mtu mmoja mmoja.

Baadhi ya wabunge walilalamikia baadhi ya walioonyesha nia ya kugombea katika majimbo yao wakisema wanajipitisha na kugawa vitu mbalimbali kwa wananchi.

Mbunge wa dole, sylvester mabumba (ccm) alitaka kujua nafasi ya takukuru kwa watanzania walioonyesha nia ya kugombea ambao wengine wameanza kuendesha harambee na kutoa misaada kanisani na misikitini.

Mbunge wa nkasi kaskazini, ally keissy, (ccm) alitaka kujua jinsi takukuru inavyoshughulikia rushwa ya ngono na rushwa kwa njia ya mtandao.

Mbunge wa iringa mjini, mchungaji peter msigwa (chadema) aliitaka taasisi hiyo iwashughulikie wabunge wanaotoa misaada ya fedha nyingi katika majimbo yao tofauti na kipato chao.

Mbunge wa muhambwe, felix mkosamali (nccr-mageuzi), alihoji kama taasisi hiyo ilishawahi kumkuta na hatia mgombea yeyote kwa kutumia sheria ya gharama ya uchaguzi.

Alitaka pia kujua kama takukuru ina uwezo wa kumuondoa mgombea wa urais hasa ccm iwapo atathibitika katoa rushwa.

Awali akifungua semina hiyo, waziri wa nchi, ofisi ya rais, utawala bora, kapteni george mkuchika, aliitaka taasisi hiyo ianze kazi sasa isisubiri hadi oktoba kwa kuwa majimboni tayari rushwa imeanza kutolewa.


chanzo: mtanzania

unlike.
 
Back
Top Bottom