Mnyukano mkubwa Ofisi ya Rais: Sefue vs Hosea

Mnyukano mkubwa Ofisi ya Rais: Sefue vs Hosea

Chakaza

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2007
Posts
41,026
Reaction score
74,704
Baada ya siku kadhaa zilizopita Katibu mkuu kiongozi kutoka ofisi ya Rais kujitokeza na kuwasafisha viongozi wa serikali waliohusishwa na sakata la Tegeta Escrow.

Kiongozi mwingine kutoka ofisi hiyohyo ya Rais naye amejitokeza na kumpinga Sefue kwa kusema uchunguzi unaendelea na mwenye mamlaka ya kusafisha watuhumiwa ni mahakama pekee tuu.

Kiongozi huyo Bw Hosea ambaye ndiye mkuu wa Takukuru ndiye hasa anayeonekana mhusika mkuu wa kushughulikia sakata hilo.

Kitendo cha viongozi wakuu hao kutoka ofisi ya Rais kutoa matamko ya kupingana hadharani kinatia mashaka juu ya namna ya utendaji wa ofisi hiyo ya juu kabisa nchini.

Chanzo; Magazeti ya leo

=========

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) imesema uchunguzi dhidi ya vigogo wa kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow unaendelea.

Kauli hiyo ilitolewa Dodoma jana na Mkurugenzi wa Takukuru, Dk . Edward Hosea alipokuwa akijibu maswali ya wabunge waliohudhuria semina ya Chama Cha Wabunge Wanaopambana na Rushwa (APNAC).

Kauli ya Dk. Hosea ilitokana na swali la Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), aliyetaka kujua kama taasisi hiyo ilishiriki kwa namna moja au nyingine kuwasafisha watuhumiwa wa Escrow.

Sendeka alihoji ni kwa vipi taasisi nyingine (Ikulu), inawasafisha watuhumiwa wa kashfa hiyo wakati Takukuru inaendelea na uchunguzi wake kitendo ambacho kinaweza kuharibu uchunguzi.

"Au kwa kuwa Takukuru na nyie mpo ofisi moja Ikulu mliwasiliana kuwasafisha watuhumiwa hao? Kama hamkushiriki kuwasafisha mseme Bunge hili kabla halijamaliza muda wake liwasaidie,"alisema Ole Sendeka.

Akijibu swali hilo, Dk. Hosea alisema taasisi yake haijamsafisha yeyote na bado inaendelea na uchunguzi wake.

"Sisi tunafanya kazi kwa mujibu wa sheria siyo kwa maelekezo kutoka kwa mtu yeyote… waliofikishwa mahakamani hatuwezi kuwasafisha na wale ambao bado uchunguzi unaendelea,"alisema.

Alisema Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue aliwasafisha watuhumiwa hao katika eneo lake na kwamba Takukuru inaangalia eneo lake.

Itakumbukwa hivi karibuni, Sefue alisema imebainika aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi aliyesimamishwa kazi kupisha uchunguzi dhidi yake, wote hawana hatia.

Rushwa kwa mitandao
Dk.Hosea pia alitoa onyo kwa wagombea wakiwamo wa nafasi za ubunge waliojiandaa kutoa rushwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kutuma fedha kupitia mitandao za kiganjani.

"Kwa sasa, Serikali imetuwezesha kudhibiti rushwa kwa njia ya mtandao, tunaye mtaalamu ambaye amesomeshwa kwa ajili hiyo, tunayo mitambo ya kisasa.

"Nawaambia wale waliojipanga mwaka huu kutoa rushwa kwa kutumia M-Pesa, Tigo- Pesa mwaka huu mjue mtaumia sana,"alisema.

Akizungumzia wagombea hasa wa nafasi ya urais ambao wameonyesha nia na baadhi wameanza kuchangia michango mbalimbali ikiwamo kwenye harambee, Dk.Hosea alisema kuwakamta watu hao inahitajika busara.

"Unapowakamata watu kama hao inabidi utumie ushahidi wa kutosha, hatumuogopi mtu, hata hivyo suala la uchaguzi ni nyeti na linasimamiwa na vyombo vingine pia,"alisema.

Aliwataka wabunge wenye malalamiko ya watu wanaotoa rushwa kwa wananchi kwenye majimbo yao wawasiliane na ofisi yake.

Alisema kwa wale wabunge wa majimbo wanaruhusiwa kutoa misaada ya maendeleo kwa wananchi wao, lakini kwa mujibu wa Sheria ya Gharama ya Uchaguzi, hairuhusiwi kutoa misaada hiyo kwa mtu mmoja mmoja.

Baadhi ya wabunge walilalamikia baadhi ya walioonyesha nia ya kugombea katika majimbo yao wakisema wanajipitisha na kugawa vitu mbalimbali kwa wananchi.

Mbunge wa Dole, Sylvester Mabumba (CCM) alitaka kujua nafasi ya Takukuru kwa Watanzania walioonyesha nia ya kugombea ambao wengine wameanza kuendesha harambee na kutoa misaada kanisani na misikitini.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy, (CCM) alitaka kujua jinsi Takukuru inavyoshughulikia rushwa ya ngono na rushwa kwa njia ya mtandao.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) aliitaka taasisi hiyo iwashughulikie wabunge wanaotoa misaada ya fedha nyingi katika majimbo yao tofauti na kipato chao.

Mbunge wa Muhambwe, Felix Mkosamali (NCCR-Mageuzi), alihoji kama taasisi hiyo ilishawahi kumkuta na hatia mgombea yeyote kwa kutumia Sheria ya Gharama ya Uchaguzi.

Alitaka pia kujua kama Takukuru ina uwezo wa kumuondoa mgombea wa urais hasa CCM iwapo atathibitika katoa rushwa.

Awali akifungua semina hiyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika, aliitaka taasisi hiyo ianze kazi sasa isisubiri hadi Oktoba kwa kuwa majimboni tayari rushwa imeanza kutolewa.


Chanzo: Mtanzania
 
katika hili mkuu chakaza i hate to say mwamini Hosea ingawa naye amekuwa ni mzigo na sijui kama ni mtu makini kwanini mpaka hii leo hajajiuzulu. Sefue hana anachojua zaidi ya kutumiwa na wakubwa ili kutuliza hali ya hewa lakini Hosea na Ofisi ya CAG wanao wataalam wa kutosha wa uchunguzi pamoja na kwamba serikali imekuwa ikiwaangusha to execute the resolutions. Sefue mpaka hii ameshindwa ni nani hao aliowatumia kufanikisha uchunguzi huo kwani hawezi kuwa yeye ndiye mwendesha mashitaka halafu pia akawa ni mzee wa baraza na halafu yeye akajigeuza kuwa jaji na kutoa hukumu na ndicho alichokifanya kwenye hili unless atauambie makosa ya ripoti ya CAG na PCCB kabla ya kutoa hukumu nyingine mpya huku akishindwa kutuambia makosa ya hukumu iliyotolewa na vyombo hivyo huru likiwemo bunge
 
Ni kweli mkuu ikulu kusafisha uvundo kama ule ni janga. Kalidharaulisha bunge, takukuru , polisi n.k inabidi sefue aachie tu ngazi. Unajua huyu ni tofauti na yule aliyeondoka luhanjo. Luhanjo alikuwa anaongea mara chache sana.
 
Sefue hajamsafisha mtu. Alichokifanya ni kutangaza matokeo ya uchunguzi uliofanywa na tume husika.
 
baada ya siku kadhaa zilizopita katibu mkuu kiongozi kutoka ofisi ya rais kujitokeza na kuwasafisha viongozi wa serikali waliohusishwa na sakata la tegeta escrow.

Kiongozi mwingine kutoka ofisi hiyohyo ya rais naye amejitokeza na kumpinga sefue kwa kusema uchunguzi unaendelea na mwenye mamlaka ya kusafisha watuhumiwa ni mahakama pekee tuu.

Kiongozi huyo bw hosea ambaye ndiye mkuu wa takukuru ndiye hasa anayeonekana mhusika mkuu wa kushughulikia sakata hilo.

Kitendo cha viongozi wakuu hao kutoka ofisi ya rais kutoa matamko ya kupingana hadharani kinatia mashaka juu ya namna ya utendaji wa ofisi hiyo ya juu kabisa nchini.

Chanzo; magazeti ya leo hii.

Hii ni sababu ya brn=best rest now
 
Sefue ana mahusiano gani na wale wezi? Au yeye ni mmoja wa wabeba viroba wa stanbic?
 
Baada ya siku kadhaa zilizopita Katibu mkuu kiongozi kutoka ofisi ya Rais kujitokeza na kuwasafisha viongozi wa serikali waliohusishwa na sakata la Tegeta Escrow.

Kiongozi mwingine kutoka ofisi hiyohyo ya Rais naye amejitokeza na kumpinga Sefue kwa kusema uchunguzi unaendelea na mwenye mamlaka ya kusafisha watuhumiwa ni mahakama pekee tuu.

Kiongozi huyo Bw Hosea ambaye ndiye mkuu wa Takukuru ndiye hasa anayeonekana mhusika mkuu wa kushughulikia sakata hilo.

Kitendo cha viongozi wakuu hao kutoka ofisi ya Rais kutoa matamko ya kupingana hadharani kinatia mashaka juu ya namna ya utendaji wa ofisi hiyo ya juu kabisa nchini.

Chanzo; Magazeti ya leo hii.

Hosea ana ushahidi wa jinsi maswi alivyonunua nyumba afrika kusini kwa fedha za escrow, hosea ana ushahidi wa sefue kununuliwa nyumba new york kwa fedha za escrow, hosea ana ushahidi wa jinsi werema alivyowekewa fedha za escrow kwenye mojawapo ya akaunti yake iliyoko afika kusini, ni suala la muda tu kila kitu kitakuwa wazi.
 
Japo huyo hosea ni chui asie na meno yupo sahihi
 
Hivi mnyukano maana yake hasa ni ipi mbona maneno haya yanatumika kihuni tu sijaona huo mnyukano unaousema wewe.
Unasukumwa na ushabiki tuu. Katibu mkuu kiongozi ni mamlaka makubwa sana na yuko ofisi ya Rais, pia Mkurugenzi wa Takukuru naye sio mtumdogo na yupo katika ofisi hyohiyo ya Rais.
Ni muono hafifu kama hawa watendaji wa Rais wanatofautiana katika jambo kubwa kama hili lililo yumbisha nchi na kuona wako sawa. Wote wanamwakilisha Rais sasa tujue jee mwenyewe yupo upande upi kati ya hawa wasemaji wake? Au yuko neutral?
Kama yuko hivyo basi hapo ndio kuna tatizo
 
Sefue hajamsafisha mtu. Alichokifanya ni kutangaza matokeo ya uchunguzi uliofanywa na tume husika.
Kama ulimsikia Sefue, alisema ripoti hiyo baada ya yeye kuisoma haitatolewa popote tena.
Nini msimamo wako kwa kauli hiyo?
 
Baada ya siku kadhaa zilizopita Katibu mkuu kiongozi kutoka ofisi ya Rais kujitokeza na kuwasafisha viongozi wa serikali waliohusishwa na sakata la Tegeta Escrow.

Kiongozi mwingine kutoka ofisi hiyohyo ya Rais naye amejitokeza na kumpinga Sefue kwa kusema uchunguzi unaendelea na mwenye mamlaka ya kusafisha watuhumiwa ni mahakama pekee tuu.

Kiongozi huyo Bw Hosea ambaye ndiye mkuu wa Takukuru ndiye hasa anayeonekana mhusika mkuu wa kushughulikia sakata hilo.

Kitendo cha viongozi wakuu hao kutoka ofisi ya Rais kutoa matamko ya kupingana hadharani kinatia mashaka juu ya namna ya utendaji wa ofisi hiyo ya juu kabisa nchini.

Chanzo; Magazeti ya leo hii.
Ikulu walisema hawahusiki na kuwa Tume ndiyo waliohusika kuwasafisha, sasa hapa inakuwaje pale kiongozi mwenye dhamana ya uchunguzi yani mkuu wa takukuru yeye aingiliwe kwenye utendaji wake.
 
Back
Top Bottom