Mnyonge Mnyongeni haki yake mpeni. Kumeanza Mgao wa Umeme na Maji

Kazi kuzua uongo tu, mtu umeme ukikatika nyumbani kwake kidogo huyo anakimbilia JF! Mnaangaika kama kuku anayetaka kutaga!
 
Hii ni ishara katika ulimwengu wa roho kwamba kuna kitu watawala bado wanaendelea kumkosea Muumba wetu, Ishara hii ya mvua kuchelewa si nzuri, bado watawala wetu wana muda wa kujisahihisha...
Amani ya Mungu iwe nawe
 
Mmewaudhi watu wa milk zone ambao ndio wameshikilia idara nyeti hapa nchini,hivyo wanawahujumu.hakuna mchawi hapo
Mama yenu leo anaenda huko milk zone kuwaomba msamaha
Sukuma gang walishatumbuliwa ili wasihujumu.
Huo ndo uwezo wao umeishia hapo.
Je enzi za JK ilikuwa zoni gani?
 
Bila wananchi kuikataa ccm kwa nguvu zote mtaendelea kupata tabu sana. Ccm ni ile ile
 
Malalamiko mengine sijui tumezoea tu kulaumu, hv hamuoni hamna mvua ulitegemea maji yatoke wapi kwa wale wanaotumia chanzo cha maji ya mito.
 
Jamaa yangu anasema ameambiwa aagize China Majenereta 500 kwa kuanzia. Na mtaji kapewa kuongezea.

Wameandikishana na mchakato umeshafanyika mtu mkubwa mmoja kamwambia hawezi agiza kwa jina lake so atamtumia yeye...

Tuache unafiki, mgao wa umeme na maji vyote vilikuwapo ila haikuwa rasmi. Tanesco walipigwa marufuku kutangaza mgao na kuna watu walifukuzwa kazi.
 
Hii hoja sijawahi ielewa, Yaani hao matajiri wazuie umeme ili wauze majenereta kwani wao viwanda vyao havitumii majenereta? Hawajui umeme ukikosekana hata mauzo ya vinywaji vyao havitauzika? Hawajui bei ya bidhaa itapanda hivo itapunguza disposal income ya kununua bidhaa zao etc

Nadhani kama ni dili pengine kampuni binafsi zipewe tenda ya kusaidia kufua umeme kuliko kusema wauze majenereta haya ya reja reja sidhani kama ROI itakua realized long term.

Kingine tuna umeme wa gesi pengine hoja ingekua wakati huu tuna utilize vp umeme wa gesi pale kinyerezi ili tupunguze mgao ikiwezekana capacity iongezwe!! Ila kuanza kulia lia tu kwa propaganda it's not helping
 
Tuache unafiki, mgao wa umeme na maji vyote vilikuwapo ila haikuwa rasmi. Tanesco walipigwa marufuku kutangaza mgao na kuna watu walifukuzwa kazi.

Kabisa, mgao ulikuwepo labda kama sasa umezidi. Maana siku za nyuma ilikuwa kosa la jinai kutangaza mgao.
 
Kongole sana na Mungu akubariki ndugu FUSO .
Bila ya serikali kuacha "ushetani" waufanyao, hii nchi haitapona.
 
Weka ushahidi.
 
Huku niliko maji yanatoka kwa wiki Mara moja tu toka enzi za nabii Nuhu. Hakuna cha mkapa kikwete Magufuli Wala Samia. Huku mpaka Mungu aamue kuleta mvua tunakinga ya mvua ndiyo nafuu yetu.
 
Baada ya gazeti la uhuru kurusha jiwe gizani hangaya yupo bize kupanga safu kuelekea twente twente faivu akianza na makatibu wa chama chakavu nchi nzima, sasa hili la mgao wa maji na umeme atalichukua na kulifanyizia kazi, au nasema uongo ndugu zanguni!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…