Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Kero ya kukatwa umeme na Tanesco imekuwa kubwa na sasa umeme wakatwa nchi nzima katika mikoa mbalimbali.
Lakini ningependa kufahamu kama umeme huu wakatwa katika sehemu zote nyeti, ofisi za kibalozi, viwandani, maeneo ya uzunguni na katika makazi ya watu muhimu katika nchi hii?
Je, umeme huo hukatwa katika sekta binafsi hususan katika kumbi za starehe, maduka makubwa na maeneo yote ambayo ni lazima yawe na umeme?
Hivi karibuni nikiwa katika safari zangu huko ugahibuni nikakutana na habari kwamba umeme huenda ukawa wakatwa nyakati za mchana tu ambapo watumiaji wa majumbani huwa ni wachache kwa kuwa huenda makazini na majumbani hakuna mtu.
Sababu ya umeme kukatwa huko Ughaibuni ni mgogoro wa Ukraine na Urusi ambao umesababisha kupanda kwa bei ya gesi ambayo ndo hutumika kuleta umeme katika nchi nyingi za Ulaya. na hiyo ni kwasababu Urusi wameamua kupunguza kiasi cha gesi wanoiuza kwenda barani Ulaya.
Lakini tatizo hilo (la kukata umeme) lilikuwa ni la wiki chache sana na baada ya hapo wananchi wa Ughaibuni hawajawahi kukosa umeme. Ukisikia Ughaibuni kuna tatizo la umeme basi fahamu ni kutokana na kutokea kwa gharika, au janga la mvua kali na upepo ambao huweza kuathiri njia za umeme na vituo vya kufulia umeme huo.
Serikali za Ulaya zinatambua kuwa umeme ukikatwa bila maelezo ya kutosha na bila miongozo wala sababu za kueleweka basi serikali hizo huingia matatizo makubwa ikiwemo wananchi kutishia mstakabali wa serikali iliyopo.
Sasa bila kuchosha sana na mada hii lengo ni kutaka kufahamu kwamba pale Tanesco wanapoukata umeme nchini je, umeme huo unokatwa ni ule uendao katika maeneo fulani tu nchini khasa makazi ya watu wa kawaida yaani wale hohehahe au pia huathiri maeneo yote niloyataja hapo juu, na kwa kuongezea maeneo ya jeshi, magereza na mashuleni?
Siwezi kusema umeme ukatwe katika mahospitali lakini angalau sehemu hizo zingine nazo zipate mgao wa masaa machache ili nao watambue kuwa kuna tatizo la umeme nchini.
Au ndo mradi wa Tanesco na wafanyabiashara wa majenereta umeshika kasi?
Ukisema ni majenereta wazungumzia suala zima la mazingira na tabia nchi ambapo moshi huathiri hali ya hewa na uoto wa asili.
Sasa waziri aneshughulikia mazingira nae ameona hili suala la majenereta kuwa ndo chanzo kikuu cha umeme na si malengo ya makusudi ya kuathiri watanzania kiafya kwa kuvuta hewa chafu ya moshi na gesi?
Hayati John Magufuli alisema kuwa kulikuwa na mtindo wa kufunga maji ili kuweka level ndogo na kila mtu alielewa hili kuwa ni hujuma.
Kwa nini Serikali yachukulia hujuma hii ni ya kawaida?
Masuali ni mengi lakini ndo hayo.