TANESCO yaelezea undani wa tatizo la umeme wa mgao, yataja uhaba wa maji na matengezo ya mitambo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharage Chande amezungumia kinachoendelea kuhusu mgao wa umeme Nchini akitaja sababu na mipango yao ya wanachokifanya ili kukabiliana na changamoto zinazojitokeza.

Amesema kuna upungufu wa Megawats 300 hadi 350 kwa siku kutokana na changamoto kadhaa ambapo kubwa ni mbili:

Maharage Chande.jpg

Maharage Chande


Upungufu wa maji
Amesema kubwa ni upungufu wa maji katika vituo vyao vinavyotumika kuzalisha umeme, akitoa mfano Kituo cha Kihansi kinachozalisha megawati 17 badala ya megawati 180 kwa hiyo megawati 163 hazizalishwi.

Pangani kinachozalisha megawati 10 badala ya megawati 68 kwa hiyo megawati 58 hazizalishwi.

Mtera kinachozalisha megawati 75 badala ya megawati 80 kwa hiyo megawati 5 hazizalishwi na Nyumba ya Mungu kinachozalishaji megawati 3 badala ya megawati 8 za umeme, kwa hiyo megawati 5 hazizalishwi.

Matengenezo ya mitambo
Amesema kutokana na matengenezo ya mitambo napo kumechangia upungufu wa umeme, Kituo cha Kidatu kinachozalisha megawati 150 badala ya megawati 200, kwa hiyo megawati 50 hazizalishwi.

Ubungo III kinachozalisha megawati 37 badala ya megawati 112, kwa hiyo megawati 75 hazizalishwi na Kinyerezi II kinachozalisha megawati 205 badala ya megawati 237, kwa hiyo megawati 32 hazizalishwi.

Ameongeza kwa kusema “Kituo cha Hale kipo katika matengenezo makubwa, kituo cha Kidatu kuna mashine moja ipo nje kwa matengenezo kinga.

“Baadhi ya vituo vilitakiwa kufanyiwa matengenezo Mwaka 2018, tunavibembeleza tunabalansi ili kuendelea kupata umeme.”

Mikakati waliyoweka
Amesema kuna wanaohoji kuhusu uwezo wa kutengeneza Megawati 1700 na kuwa ziko wapi, huo uwezo upo lakini haufiki kutokana na changamoto zinazojitokeza tulizozitaja.

“Pia tunaharakisha matengenezo ya mtambo mmoja katika kituo cha Ubungo III ili kuingiza megawati 35 za umeme tarehe 25 Novemba 2022, pia katika Ubungo III ili ili kuingiza megawati 40 za umeme mwishoni mwa Disemba 2022

“Kukamilisha matengenezo ya Kituo cha Kidatu ili kuingiza Megawati 50 kufikia tarehe 30 Novemba 2022, upanuzi cha Kinyerezi I ili kuingiza megawati 90 kabla ya mwisho wa mwezi Disemba 2022.

“Ukarabati ukikamilika kama ulivyopangwa, itatupatia jumla ya megawati 277 kwenye uzalishaji.”

Ameongeza kuwa wanafanya marekebisho katika vituo vya gesi kituo cha kwanza ni Ubungo No# 3 (Megawats 80), Kidatu (Megawats 50), upanuzi wa Kinyerezi 1 (Megawats 90).

Matumaini makubwa Bwawa la Mwalimu Nyerere
Amesema pamoja na yote hayo mambo yatabadilika kama mvua zitaanza kunyesha lakini matumaini yao makubwa ni Bwawa la Mwalimu Nyerere likikamilika litapunguza changamoto nyingi kwa kuwa ni bwawa kubwa na litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji mengi.

PRESS RELEASE UPUNGUFU WA UMEME NCHINI NA MIKAKATI YA KUKABILIANA NAZO_page-0001.jpg
 
Back
Top Bottom