Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,694
- 149,917
Naibu Katiba Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amekanusha taarifa zinazodai kuwa anataka kuachana na chama hicho.
Mnyika amesema hayo jana alipopigiwa simu ili azungumzie taarifa hizo. Mbunge huyo wa Kibamba amesisitiza kwamba huo ni uzushi.
“Hakuna kitu kama hicho na wala sina mpango wa kuhama,” amesema.
Habari za kujiuzulu kwa Mnyika zilianza kusambaa katika vyombo vya habari kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe kufukuzwa uanachama.
Uvumi ulienea kwenye mitando kwamba amejivua nyadhifa zake zote na kwamba ameshakabidhi barua yake kwa Katibu Mkuu wakati huo, Dk Willibrod Slaa.
Chanzo: Mwananchi online