Mnyika: Sina mpango wa kuhama CHADEMA

Mnyika: Sina mpango wa kuhama CHADEMA

Kwa nini Mnyika asijitokeze mwenyewe kwenye public na kumaliza hizi tetesi? Atumie ata twitter au jamiiforums kukanusha.
Mnyika hana muda wa kupoteza kwa kuwajibu hao kina kwangu pakavu wa ccm
 
Kwa nini Mnyika asijitokeze mwenyewe kwenye public na kumaliza hizi tetesi? Atumie ata twitter au jamiiforums kukanusha.
Waliotunga labda ndio wenye tatizo la kutoa tungo tena ni kipi kinaedelea. Ili kujitoa kimasomaso. PIA, Wengine mjifunze kuacha kushabikia tungo za wahuni.
 
Bali ccm ndio imeiokota hiyo dira siyo?dira ya kutuuzia sukari kilo moja sh 4000?dira ya kuyafanya mafuta ya taa kuwa ni almasi?dira ya kutuongezea kodi kwenye miamala ya fedha siyo?dira ya kununua vivuko vibovu kwa mabilioni siyo?
Ni kosa sana kwa CHADEMA kuifanya CCM kama ndiyo litmus paper yake
CCM inafanya makosa mengi sana ambayo CHADEMA inashindwa kuya capitalize
Na kwa makada wa CCM sasa kuwa DED na kwa vile sijaona kauli yyt ya upinzani kwenda Court kupinga teuzi hizi basi 2020 tayari Magufuli kaisha jiandalia mazingira ya kushinda kwa kishindo

Kumbuka ma DED hawa akina Abubakar Assenga na akina Anne William Shijja walioshindwa kura za maoni ndani ya CCM 2015 ndiyo watasimamia uchaguzi mkuu 2020!

Wake up my son!
 
Naibu Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika amekanusha taarifa zinazodai kuwa anataka kuachana na chama hicho.

Mnyika amesema hayo jana alipopigiwa simu ili azungumzie taarifa hizo. Mbunge huyo wa Kibamba amesisitiza kwamba huo ni uzushi.

“Hakuna kitu kama hicho na wala sina mpango wa kuhama,” amesema.

Habari za kujiuzulu kwa Mnyika zilianza kusambaa katika vyombo vya habari kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kufukuzwa uanachama.

Uvumi ulienea kwenye mitando kwamba amejivua nyadhifa zake zote na kwamba ameshakabidhi barua yake kwa katibu mkuu wakati huo, Dk Willibrod Slaa.

Chanzo:Mwananchi online

Hivi kuna ugumu gani kwa yeye kuitisha press conference na kukana hadharani? Mbona wakati ule Lowassa akiwa ccm na CHADEMA mkimtukana kuwa ni fisadi namba moja Mnyika alikuwa anaitisha press conference na kutaka Lowassa achukuliwe hatua za kisheria?
 
Hata Zitto alisema atakuwa mtu wa mwisho kuhama chadema, wakati huohuo akawa anaiandaa ACT. Tunawatambua watu kwa matendo, sio maneno.
 
Kwa Taifa la TANZANIA lilipo sasa hv ushabiki wa vyama si tija kwa nchi tena. Viongozi wa focus kwenye matatizo ya wananchi na waache ushabiki uchwara wa vyama.

Ushabiki wa vyama ndo unazidi kudidimiza Taifa la Tanzania. Watu hawaangalii tena ni hoja ipi yenye nguvu ikubalike kuivusha Tanzania kwenda mbele wamebakia kushabikia vyama tu.

Leo hii kiongozi wa CCM akitoa hoja yenye nguvu inayoweza kuvusha Tanzania kwenda mbele basi kwa kuwa kaitoa mtu wa CCM upinzani kwa nguvu zote watapinga. Leo kiongozi wa UPINZANI akitoa hoja yenye nguvu ya kuwezesha kuleta maendeleo kwa wananchi basi kwa kuwa imetolewa na UPINZANI viongozi wote wa CCM. wataipinga kwa nguvu zote kwa sababu tu imetolewa na UPINZANI.

Huu ni upofu wa akili, sijui wamelogwa🙁🙁. Sisi kama watanzania hatuhitaji kujua ni CCM au ni UKAWA wamefanya tunahitaji maendeleo kwa Watanzania. Ukisikiliza mijadala inayoendelea bungeni sometimes ungekuwa na uwezo unaweza chapa watu bakora.

Jamani tushikane kwa pamoja tuendeleze Taifa letu. Tuacheni ushabiki usio na maana wa kuleta siasa kwenye kazi. Taifa hili halitajengwa kwa migawanyiko ya kisiasa, tutapiga hatua na kusonga mbele tu kwa kushikana pamoja katika umoja wa kweli. Tukatae mabaya na yale mazuri ya kutuvusha mbele tuyashikilie kwa pamoja kama TAIFA tusonge mbele, tusibaguane kwa vyama, udini, ukanda au ukabila. Haya mambo yatalibomoa Taifa na hatutafika popote.

Well said Mwanawao, ubarikiwe sana!
Chama changu ni UTANZANIA, kwa umoja tutafika.
Well said Mwanawao! Barikiwa sana.
Naibu Katiba Mkuu wa Chadema, John Mnyika amekanusha taarifa zinazodai kuwa anataka kuachana na chama hicho.

Mnyika amesema hayo jana alipopigiwa simu ili azungumzie taarifa hizo. Mbunge huyo wa Kibamba amesisitiza kwamba huo ni uzushi.

“Hakuna kitu kama hicho na wala sina mpango wa kuhama,” amesema.

Habari za kujiuzulu kwa Mnyika zilianza kusambaa katika vyombo vya habari kwa mara ya kwanza mwaka 2013 baada ya aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe kufukuzwa uanachama.

Uvumi ulienea kwenye mitando kwamba amejivua nyadhifa zake zote na kwamba ameshakabidhi barua yake kwa katibu mkuu wakati huo, Dk Willibrod Slaa.

Chanzo:Mwananchi online
 
Ni kosa sana kwa CHADEMA kuifanya CCM kama ndiyo litmus paper yake
CCM inafanya makosa mengi sana ambayo CHADEMA inashindwa kuya capitalize
Na kwa makada wa CCM sasa kuwa DED na kwa vile sijaona kauli yyt ya upinzani kwenda Court kupinga teuzi hizi basi 2020 tayari Magufuli kaisha jiandalia mazingira ya kushinda kwa kishindo

Kumbuka ma DED hawa akina Abubakar Assenga na akina Anne William Shijja walioshindwa kura za maoni ndani ya CCM 2015 ndiyo watasimamia uchaguzi mkuu 2020!

Wake up my son!
Sasa hapo ndio umechangia kitu gani zaidi ya kutabiri mvua kipindi cha masika?
 
kwan Zito na Slaa walivoondoka CDM imekufa au Lipumba alivoachia ngazi CUF imekufa, hawa jamaa watakuja kisha watapita ila vyama vitadunda na kuzidi kuimarika tu cku hadi cku
 
Kwa sababu Mbowe ni myopia HAWEZI ona ya 2020
Angeona ya mbali jana angekuwa Mahakamani kuomba mwongozo wa Mahakama iweje Manji wa Yanga awe refarii wa mechi ya Simba na Yanga 2020?

Nina uhakika kwa majina haya ya DED wapya,Mahakama ingefanya kitu kutupa uwanja sawa 2020
 
kwan Zito na Slaa walivoondoka CDM imekufa au Lipumba alivoachia ngazi CUF imekufa, hawa jamaa watakuja kisha watapita ila vyama vitadunda na kuzidi kuimarika tu cku hadi cku
Ok!Kuimarika na wabunge 20+ wa Majimbo kati ya Majimbo zaidi ya 200+?Wakati watz waliisha ichoka CCM uchaguzi wa 2015 wakakosa uongozi thabiti wa wapinzani huku Bara?Mnadhani nafasi ya CCM goi goi kama ya JK itarudi tena?

Haya basi sawa
 
Hata lowasa na genge lake kuhama ccm ilianza na tetesi
Zito kuanzisha chama alianza natetesi
Na hii ya myika ni mwendelezo wa tetesi misho itakua kama hayiooo
 
Hivi kuna ugumu gani kwa yeye kuitisha press conference na kukana hadharani? Mbona wakati ule Lowassa akiwa ccm na CHADEMA mkimtukana kuwa ni fisadi namba moja Mnyika alikuwa anaitisha press conference na kutaka Lowassa achukuliwe hatua za kisheria?
kama kila tetesi ya mtaani ataita press conference itabidi ahamie CHUMBA CHA HABARI MAELEZO kabisa!
 
Hata Dr. Slaa na Prof. Lipumba hawakuhama vyama. Mnyika ni rafiki yangu. Ninachojua ni kwamba John Mnyika na Halima Mdee wanaenda ACT-Wazalendo ambapo anaenda kuwa GS. It's a matter of time.
unaongea usingizini.ukiamka tuletee habari kamili.
 
Hii awamu ya tano ndo hovyo kabisa,ushabiki umeanzia kwa mkuu wa kaya hadi kwa Mjumbe wa nyumba kumi.awamu ya tano imejikita zaidi kujenga chama kuliko nchi.nchi inaendeshwa kwa mfumo wa kishabiki na mashindano,so sad,

Back
Top Bottom