Mnyika jimbo la Ubungo umeshalikosa

Mnyika jimbo la Ubungo umeshalikosa

Mkuu nitakupa shule kidogo,
Kazi ya mbunge ni kwenda kutuwakilisha sisi mbele ya serikali/Bunge.Yeye ndiye wa kwenda kuitolea macho serikali na kuwaambia NO lazima mtenge fedha kwa ajili ya utanuzi wa bomba ambalo linapeleka maji sehemu kadha wa kadha,bila hivo serikali inapeleka hela sehemu nyingine,sasa kama hata kazi hii ya kutuhakikishia tunapata maji imemshinda ndani ya miaka 5 ataweza nini? Tunamsubiti kwa hamu baada ya bunge kuvunjwa,sisi sio wa kudanganywa

kasome kwanza ule mpango wa miaka 5 kwanza. mambo hayaendi hivyo.
 
tumia akili kidogo tu mkuu. nani anakusanya kodi? ukosefu wa maji dar hausababishwi na mbunge. mtambo wa kuleta maji dar uliojengwa na wajerumani ulikuwa wa kukidhi watu wasiozidi laki8. leo hii dar ina watu wangapi? nambie kwa mtambo upi unataka ulete maji ya kutoshereza jiji?

na wewe tumia akili ndogo mnyika alivyokua anaahidi alidhani atafanya miujiza?
 
Anza kwanza kujipima wewe umefanya nini kuleta maji kama huna acha excuse.Unawajibika kama raia kufuatilia maji wazara ya maji na si kusubiri miaka mitano uulize kwenye mitandao.Ila kama bado unania ya kupata maji ubungo hilo swali ni zuri sana ila umeuliza wrong person or place nenda wizara ya maji.Na majibu utuletee pia hapo utakuwa umewajibika

nilichofanya cha kwanza ni kumchagua yeye alipwe ili atatue matatizo yangu namlipa milioni 11 kwa mwezi ili alete maji
 
Kaka amechanganya ma file ila sio mbaya nikimjibu najua alinilenga mimi,
Wewe ndugu Amagere,huna sababu ya kumtetea Mnyika atakuja ajitetee mwenyewe kama anaweza,aliyekwambia maji yanafika kwa wananchi kwa sisi kwenda wizara ya maji ni nani? ndi mana tukawa na wawakilishi wa kuifanya hiyo kazi,ku-push government ku-fund projects za maji etc,kama hujui how the system works ni bora utulie.Ndio mana tukawa na wabunge na ndio mana na wao wanakuja na ahadi za kuweza kufanya yale yote tunayomtaka akatuwakilishe.Hili swala litamsumbua sana mana asilimia kubwa ya jimbo halina maji,Kimara ndio majanga,cha ajabu kuna sehemu inaitwa Kibamba,diwani wao tu ameweza kufanya follow up na pushing za kutosha wanachezea maji watakavyo japo mwanzo kwao ilikuwa ni tatizo pia,yeye leo Mbunge amekalia kumpa mipasho Zitto kabwe,Ngoja bunge livunjwe tunakusubiri huku.

Kama unadhani namtetea mnyika your wrong.Na kama unaona unajua sana how system works endelea kujua.Hakuna haja ya debate katika hili.We seburi aje ajitetee ila akili yangu finyu najua kama mwananchi unao wajibu na jukumu ya serikali inayojali wananchi kifanya hayo kazi ya mbunge kama sehemu ya bunge ni kuisimamia serikali.I do not discuss mnyika nilidhani hoja yako ni ukosefu wa maji ila kama hoja mnyika nadhani hilo halikupaswa kuwa posted hapa we need to discuss issues not individuals above all we need ti act and make things happen and not otherwise.
 
nilichofanya cha kwanza ni kumchagua yeye alipwe ili atatue matatizo yangu namlipa milioni 11 kwa mwezi ili alete maji

Kasome katiba ya Tanzania uone majukumu na kazi ya mbunge.Vinginevyo tutakuwa tunapoteza muda
 
Mnyika aligerezea kwa Zitto sasa ana kazi duniani bora ata ange hama nchi maana anajua ubungo siyo yake kabisa
 
Tatizo la maji ubungo na sehemu nyingine za Tanzania litakwisha kwa kuiondoa madarakani serikali dhaifu ya ccm na kuweka serikali makini itakayojali wananchi wake. Mnyika amejitahidi sana kuahughulikia tatizo la maji ubungo hadi kufikia kupeleka hoja binafsi bungeni lakini serikali dhaifu ya ccm imeshindwa kutatia kero hii hapo iliahidi kulifanyia kazi.
 
Mnyika aligerezea kwa Zitto sasa ana kazi duniani bora ata ange hama nchi maana anajua ubungo siyo yake kabisa
Mnyika atarudi bungeni kwa kishindo na amini nakuambia ayatullah Zitto harudi bungeni kamwe. Kupitia jimbo lipi kama jimbo lake kalikimbia?
 
Maji ni janga la Dar es Salaam yote na janga hili ni la muda mrefu kutokana na mipango mibovu ya serikali...

Miundombinu bado ni ya mkoloni, ujenzi wa makazi ya watu upo kiholela na mengineyo...
 
Kama unadhani namtetea mnyika your wrong.Na kama unaona unajua sana how system works endelea kujua.Hakuna haja ya debate katika hili.We seburi aje ajitetee ila akili yangu finyu najua kama mwananchi unao wajibu na jukumu ya serikali inayojali wananchi kifanya hayo kazi ya mbunge kama sehemu ya bunge ni kuisimamia serikali.I do not discuss mnyika nilidhani hoja yako ni ukosefu wa maji ila kama hoja mnyika nadhani hilo halikupaswa kuwa posted hapa we need to discuss issues not individuals above all we need ti act and make things happen and not otherwise.
kaka naona unajaribu kukwepa ukweli wa mada,mada ni maji ubungo maji ambayo mbunge wa jimbo husika ana wajibu wa kuyasimamia upatikanaji wake kama ilivyokuwa ahadi yake,sisi wananchi tuna wajibu wetu na tunauchukua ila kama mbunge ana nafasi ya kipekee katika kulifanikisha hili,nafasi yake ina mruhusu kuwa na mkutano,mijadala,phone call etc na wahusika au wadau wenzie katika utekelezaji wa hili na ndio maana ya kuwa na wawakilishi.Ajiandae kwa maswali lakini muhimu zaidi aandae majibu ya kueleweka.
 
kabla ya mnyika,wewe kilaza ulikuwa unapata maji huko ubungo?fedha za maendeleo ambazo ndio kodi zetu ccm ndio wenye mamlaka ya kuziallocate.....na ulivyokuwa mpumbavu unasema anahujumiwa.sasa kama anahujumiwa na wewe unalijua hilo,basi shiriki nae mnyika katka kupambana na hujuma hizo.........unalalamika unalalamika,wewe umefanya jambo gani ktk jimbo hilo mpaka sasa?.....ndio tatizo ya mikaka inayoishi kwa dada,anasubiri shemeji alete chakula ili lile......fufafu we!
 
Nchi nzima kilio cha maji na umeme,mnyika afanyeje.?
 
hahahaha store za vijiweni ukute ubungo anapafaham sababu alifikia hapo wakati anawasili tokea kijijini mwao sitimbi muda wa muajiri wake anautumia vibaya kuandika habari ambazo hata hazielewi
 
Muheshimiwa wakati wa kampeni ya uchaguzi 2010 ulituahidi kuwa utamaliza kero ya maji Ubungo, tukakupa kura zetu. Tukakesha wote pale loyola kuhakikisha kura hazichakachuliwi, peoplez power tukalibeba na kulipindua gari la wizara ya mambo ya ndani wakati lilipolazimisha kuingia pale getini mimi Dar es salaam nimekuja mwaka 90 nilifikia Gongolamboto ambapo nakumbuka tulikuwa tunakunywa maji ya kisima na yenye chumvi.

Niliendelea kunywa maji ya chumvi mpaka mwisho wa miaka ya tisini ndiyo ilikuwa mwisho wa kunywa maji ya chumvi..leo karne ya 21 miaka 50 ya uhuru kwa mara ya kwanza na kunywa maji ya chumvi. Kweli tunasifu juhudi zako za kufichua maovu huko bungeni lakini kura zetu sahau. Umeshindwa kusoma alama za nyakati kwamba wakuu wamekuundia zengwe Ubungo pasipatikane maji ili uonekane hufanyi chochote. Ungeweza hata kuleta maji ya kununua kwenye malori tunge appriciate uwajibikaji wako sasa huku maji hakuna hata ya kununua hakuna. Ukipata ubunge 2015 walahi natembea uchi. "maana tumechoka sasa"

Kwani mnyika ndo anakusanya kodi sikuhizi? Miaka hamsini ya uhuru mmeshindwa kuleta maji mnataka miujiza ya miaka mitano,
 
Muheshimiwa wakati wa kampeni ya uchaguzi 2010 ulituahidi kuwa utamaliza kero ya maji Ubungo, tukakupa kura zetu. Tukakesha wote pale loyola kuhakikisha kura hazichakachuliwi, peoplez power tukalibeba na kulipindua gari la wizara ya mambo ya ndani wakati lilipolazimisha kuingia pale getini mimi Dar es salaam nimekuja mwaka 90 nilifikia Gongolamboto ambapo nakumbuka tulikuwa tunakunywa maji ya kisima na yenye chumvi.

Niliendelea kunywa maji ya chumvi mpaka mwisho wa miaka ya tisini ndiyo ilikuwa mwisho wa kunywa maji ya chumvi..leo karne ya 21 miaka 50 ya uhuru kwa mara ya kwanza na kunywa maji ya chumvi. Kweli tunasifu juhudi zako za kufichua maovu huko bungeni lakini kura zetu sahau. Umeshindwa kusoma alama za nyakati kwamba wakuu wamekuundia zengwe Ubungo pasipatikane maji ili uonekane hufanyi chochote. Ungeweza hata kuleta maji ya kununua kwenye malori tunge appriciate uwajibikaji wako sasa huku maji hakuna hata ya kununua hakuna. Ukipata ubunge 2015 walahi natembea uchi. "maana tumechoka sasa"

Nitakukumbusha kutembea uchi mkuu nime quote ili October 27 nikukumbeshe kutembea uchi ahadi ni deni na jiandae kuilipa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom