Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 36,979
- 45,866
Inaweza kua bahati mbaya au nzuri kwa wanaubungo kwana kwa miaka ya hivi karibuni wamekua wakichagua wabunge ambao ni wa kitaifa zaidi.
Kabla ya mbunge huyu wa sasa aliyepo, aliyepita alijikita zaidi katika muda wake wa ubunge kwa kushughulika na mambo ya kitaifa, alisahau wajibu wake, na kushindwa kutatua matatizo yaliyodhahiri ya waliomtuma kwenda bungeni, shida ya maji ambayo ni tatizo la muda mrefu halikuwahi kutatuliwa na mbunge aliyemaliza muda wake, jambo lililo mfanya kusoma nyakati na kukimbilia jimbo lingine la uchaguzi akijua wazi kua alifanya makosa ambayo yaligharimu ubunge wake.
Huyu wa sasa nae, yupo karibia kwenye kila kichwa cha habari kwa kujihusisha na mambo yasiyo na faida kwa jimbo lake moja kwa moja, kwani ni wazi kabisa kwamba uchaguzi wa umeya kwa manispaa ambayo haipo chini ya jimbo lake hauna faida ya moja kwa moja kwa wanaubungo wala hauwasaidii kutatua kero zao.
Tunakwenda kuona mbunge mwingine wa ubungo akikimbia jimbo kwa sababu ya kulitekeleza mwenyewe na kutumia muda kwa mambo ambayo hayana uhusiano wa moja kwa moja na wapiga kura wake.
Ni wakati sasa kwa wanaubungo kuwa makini na uchaguzi wao wa wawakilishi, ama la watabaki kusikia maendeleo kwa wengine.