Mnyika, Balille, Rostam Aziz na kisa cha sms!

Saaaaaafi sana Mnyika. Hawa sasa ni kazi moja tu kuwagusa kwa majina na hadhi zao

Call a spade a spade and not a spoon.

Big up Mnyika
 
Siku ile ile niliposoma lile tamko la Mnyika (CHADEMA) niliandika lile tamko halikutakiwa kutolewa maana lilikuwa linaingiza siasa kwenye kifo cha Wangwe. Lile tamko lilikuwa linakaribisha Wajanja wengine kuingia kwenye kamchezo ka wanasiasa (ku SPIN). Na haikupita muda RA na genge lake wakawa nao wamepata greenlight na kuingiza spins zao.

Pili, Mnyika kumwandikia ujumbe RA kwenye simu yake ni utoto wa kisiasa. Anaonyesha ana hasira wakati kwenye siasa hasira ni kitu cha mwisho, alikuwa anatumia hoja ya manguvu kuliko nguvu ya hoja. kwa kufanya hivyo anaweza kufurahisha wafuasi wake wachache lakini akaudhi watu wengi neutral na independent ambao ndio CHADEMA inawahitaji zaidi ili kushinda uchaguzi.

State ya siasa za TZ iko chini mno. Siasa imeingiliwa kama tu fani ya uandishi wa habari.

Hali mbaya ya nchi yetu sasa haitoi nafasi ya kuwa neutral. Objective yes lakini sio kuwa neutral. Ur either with FISADI's or AGAINST FISADI's. Sasa kama wewe unadhani utakuwa neutral kuhusiana na ROSTAM basi ujijue una tatizo. Na hawa so called neutral people ndio chachandu ya kuendelea kuwa na mfumo fisadi tulio nao.

Na kusema kuwa MNYIKA anaingiza siasa ni ujinga. Siasa zilishaingia tangia hatua za mwanzo wa taarifa za kifo cha wangwe. Waliokimbilia kuconclude kuwa CHADEMA wanaweza husika na kifo hiki kwa sababu ya tofauti zilizokuwepo kati ya marehemu na viongozi wenzake huko ndio waliliingiza hili suala kisiasa. Ama ulitaka MNYIKA anyamaze ili hii sumu itapakae bila ya kupambana nayo. Masuala ya kunyamaza kuacha hizi propaganda hovyo zikitapakaa bila kukabiliana nazo uso kwa uso ndio tatizo kubwa tuliokuwa nalo kwa miaka mingi nchini kiasi cha kufanya hadi leo wote tukaaminishwa kuwa kina Sokoine, Kolimba na wengine wengi ni lazima wawe wameuawa.

Uzuri wa hili unanifanya kujipanua zaidi kimawazo na kuanza kujifunza kuacha misimamo inayobase katika hisia bila ya kuwa na uweli.

Kwa mimi niliyekuwepo TARIME kuanzia mwili wa marehemu ulipoingia hadi siku ya kuzikwa nashukuru wengi wenu hapa jinsi mnavyochemsha kwani mnaniwezesha kujielimisha mambo mengi ikiwemo hili suala la kujenga imani kwa misingi ya hisia zilizokosa chembe ya ujuvi......

Tanzanianjema
 
Mkuu RA ni fisadi! Atashida kwa sababu wanaompigia kura {IGUNGA kama sikosei} hawamjui! Kwanza anawafisadi na kuwalewesha! Kwa hiyo atatumia ufisadi kupata ubunge!

Wanamjua vizuri lakini wao kama walivyo watanzania wengi wamelishwa ujinga wa kuwa na taswira kuwa UBUNGE ni UFADHILI na sio UWAKILISHI wao katika masuala ya kutunga SHERIA na Kutetea SERA za taifa lao....

Lakini lazima mjue siri ya uhusika wa ROSTAM hapa sio tu kuwageuzia kibao WASEMA MAFISADI bali pia kuhakikisha kuwa ifikapo 2010 kina MWAKYEMBE na wenziwe wapatao 70 ndani ya bunge hawana upenyo wa kutokea CCM wakihsalimwa vichwa kama ilivyokuwa kwa wakina KITINE 2005. Wanaamini kuwa endapo hakutakuwa na chama mbadala cha kukimbilia wakati huo ambao utakuwa mchache kwa kuanzisha chama kipya na kujijenga basi ni wazi "USHUJAA" wao utakwisha na kelele dhidi ya UFISADI itapungua kama sio kwisha kabisa....


Tanzanianjema
 
Hali mbaya ya nchi yetu sasa haitoi nafasi ya kuwa neutral. Objective yes lakini sio kuwa neutral. Ur either with FISADI's or AGAINST FISADI's. Sasa kama wewe unadhani utakuwa neutral kuhusiana na ROSTAM basi ujijue una tatizo. Na hawa so called neutral people ndio chachandu ya kuendelea kuwa na mfumo fisadi tulio nao.

Na kusema kuwa MNYIKA anaingiza siasa ni ujinga. Siasa zilishaingia tangia hatua za mwanzo wa taarifa za kifo cha wangwe. Waliokimbilia kuconclude kuwa CHADEMA wanaweza husika na kifo hiki kwa sababu ya tofauti zilizokuwepo kati ya marehemu na viongozi wenzake huko ndio waliliingiza hili suala kisiasa. Ama ulitaka MNYIKA anyamaze ili hii sumu itapakae bila ya kupambana nayo. Masuala ya kunyamaza kuacha hizi propaganda hovyo zikitapakaa bila kukabiliana nazo uso kwa uso ndio tatizo kubwa tuliokuwa nalo kwa miaka mingi nchini kiasi cha kufanya hadi leo wote tukaaminishwa kuwa kina Sokoine, Kolimba na wengine wengi ni lazima wawe wameuawa.

Uzuri wa hili unanifanya kujipanua zaidi kimawazo na kuanza kujifunza kuacha misimamo inayobase katika hisia bila ya kuwa na uweli.

Kwa mimi niliyekuwepo TARIME kuanzia mwili wa marehemu ulipoingia hadi siku ya kuzikwa nashukuru wengi wenu hapa jinsi mnavyochemsha kwani mnaniwezesha kujielimisha mambo mengi ikiwemo hili suala la kujenga imani kwa misingi ya hisia zilizokosa chembe ya ujuvi......

Tanzanianjema

Hivi huwezi kujadili hoja bila kuita watu wengine wajinga? Una uhakika gani wewe ni mwerevu kuliko hao wajinga?

Sorry, sina muda wa kujadiliana hoja na watu wanaocha hoja na kuingia kwenye personal attacks, nitakuwa napoteza muda wangu. Kuna mambo mengi mengine ya maana kuliko personal attacks JF.
 
Hivi huwezi kujadili hoja bila kuita watu wengine wajinga? Una uhakika gani wewe ni mwerevu kuliko hao wajinga?

Sorry, sina muda wa kujadiliana hoja na watu wanaocha hoja na kuingia kwenye personal attacks, nitakuwa napoteza muda wangu. Kuna mambo mengi mengine ya maana kuliko personal attacks JF.

Mimi nakwambia bado tu wachanga kwenye mijadala. Kuna watu wanataka kila mtu afikiri wanavyofikiri wao, na bado wanaamini wao ni wajanja!!
 
kwanza nianze kwa kumpongeza Mh Mnyika kwani ni Dunia yetu hii ni duara na katika dunia kuna mambo mengi ambayo yanahusisha viumbe vilivyo hai na moja ya kiumbe chenye changamoto pana na kinachojibadilisha na kukarahisha kwa wakati huo huo ni sisi binadamu hivyo kwa binadamu huwa tunaamini ili mchawi aache kukuloga lazima umwambie kuwa wewe ni mchawi ili kusudi ajue kuwa unajua na siyo kunyamaza wakati mhusika akiwa hajui ya kuwa wajua yale ayafanyayo

Baada ya kusema hayo naomba nirudi katika suala zima la kupongeza gazeti la Tanzania daima kwa kuwa moja ya chombo cha habari ambacho naweza kutumaini uandishi wake na namna kinavyoweza kuweka habari bila ya kumfanya msomaji ni limbukeni wa kuchanganua habari na pia kumpatia uwezo kuona mambo yalivyp pongezi mhariri wa gazeti la Tanzania daima pongezi waandishi wote wa gazeti hili

Hakuna jambo baya kama kumsadikisha binadamu jambo lisilo la kweli nasema hivi kwa kuwa sisi twazungumza mengi kwa vinywa vyetu kwa maandishi yetu lakini ukweli hujudhihiri wenyewe kadri muda unavyokwenda hakuna namna ambavyo waweza kusema moto haupo wakati moshi unafuka. Mwaka 2005 walikuwa na a great hope political slogan i have never heared it in my life time experince of being a voter in my country Tanzania that is new zeal, vigour and speed, tukateuliwa waziri mkuu wa kwanza Mh E N. L naye akaapa kuwa
@NITAWATUMIKIA WATANZANIA KWA UMAHIRI NA UMAKINI MKUBWA lakini je leo umakini upo wapi? ( hili ni suala la muda tu) leo umahiri upo wapi (nalo ni muda tu) wazungu wanasema a moment of truth shall prevail in our promises. Hakuna ukweli usiyojulikana hata kama ni baada ya miaka kadhaa kupita kubali msikubali a moment of truth shall take its position to every promise and every did in our life prospects hivyo ya PM aliyepita umahiri tuliuona na umakini tumeuona na ufisadi tumeushuhudia katika umakini na umahiri je na hili Mh Mnyika nakupongeza kwani badala ya kusubiri muda uielimishe jamii tatizo lipo wapi umeamua kutuelimisha tunashukuru sana

Kinachoniumiza sana akilini ni suala la protection kwa wale wanaothubutu kusema ukweli kabla ya muda kutueleza ukweli kama Mh. Mnyika na wale waliopo upande wa upinzani bungeni pale Dodoma na waliopo katika usaidizi wa ofisi zao kwa kweli hili lililotokea kwa Mh. wa Tarime tujifunze kuona vitu katika matabaka zaidi ya moja kwa maana ya kuwa in economy they say no free service if you manage to have free service some where remember there is another person somewhere pay for you either direct or indirect hivyo nawatakieni wanachadema wote muwe makini kwa hili lisijekuwa na madhara ama kisiasa au kufunga upeo wenu wa kutoa maoni mbali mbali

MWISHO NAPENDA KUTOA WITO KWA WATANZANIA WANAOFAHAMU AMA AMBAO WANAPENDA KUONA TANZANIA IKIENDELEA WAKATI NI HUU TUNAHITAJI MABADILIKO YA KWELI NA MOJA YA NJIA SAHIHI YA KULETA MABADILIKO SIYO KWA KUSOMA YALIYOANDIKWA NA VYOMBO VYA HABARI VINAVYOTUDANGANYA NA KUTUNYIMA HAKI YA KUJUA UKWELI BALI NI KUTEKELEZA YAFUATAYO

1. kama upo shule iwe sekondari ama chuo hakikisha una watu 30 wa kuwaelimisha nini maana ya kupiga kura na nini umuhimu wa kuchagua kiongozi unayemtaka kwani ni muhimu mno kwa hili

2. endapo unafanya kazi ama ulishamaliza elimu ya chuo hakikisha una nakala ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania elewa katiba yako na majukumu yako ili kwa kujua itakupatia mawanda mapana ya kuona Mh. Mnyika ana haki ya kuita mtu fisadi kwa maana anatenda kinyume na Katiba husika msije kuchangia mawazo hapa bila ya kusoma. Na ukishakusoma elimisha watu 50 umuhimu wa kuijua katiba na haki za msingi za Raia hivyo tukisema magazeti fulani yagungiwe kwa maandamano serikali ijue ya kuwa wapo watanzania wanasema kwa kujua haki zao.

3. Ninapenda kumsifu sana Mh Hayati Chacha Wangwe kwani ni Baba halisi wa haki na alijua vyema Katiba na kanuni za bunge ndo maana leo tunamwona shupavu ushupavu wake upo kwa kuwa alijua haki yake katika katiba na haki yake katika kanuni za bunge hivyo kwa mimi ninapenda kutamka wazi nitamwita BABA WA HAKI YA KWELI YA MTANZANIA MLALAHOI

4. Ninawaomba watanzania waliopo katika ajira za serikali ambazo haziruhusu siasa ama kuwa sehemu ya siasa waweze kuwa chachu kubwa ya kuwaumbua viongozi wao wa wizara, mikoa, wilaya, manispaa za miji wanafanya kazi kinyume na maadili kama huwezi kusema andika katika jamiiforums ili watu wayaseme. Endapo unaelewa taratibu zimekiukwa za namna yeyote katika kuendesha jambo lolote sema wakati ni huu siyo kuficha kwa kuwa babu alikuwa mjumbe wa kamati kuu ama mwanasiasa au kwa kuwa ajira yako uliandikiwa kinoti na waziri ama katibu mkuu kumbuka kupitia employment and labour relation act 2004 act no 6 na 7 kama zilivyotungwa na bunge na kuanza kutumika Desemba 2005

tuwe wepesi kusoma na kuona kusoma ndiyo njia pekee ya kuishi kwa kuzijua haki zako za msingi

asante kwa kusoma tuelemishane kwa mambo mengi ya msingi
 
Mimi nakwambia bado tu wachanga kwenye mijadala. Kuna watu wanataka kila mtu afikiri wanavyofikiri wao, na bado wanaamini wao ni wajanja!!

Kaka KITILA,

Kwa kuwa mimi na wewe tunajuana naomba nikuulize swali moja...NI KWELI UNAAMINI MANENO YAKO KUWA mimi ni mchanga katika mijadala?

Hivi Kusema kuwa tuache ujinga ni shambulio binafsi? Hivi kama hoja haikumbana MTANZANIA ni kwanini akimbilie neno moja tu la maelezo yangu yote na kuacha msingi wa hoja yenyewe......

Nijibu swali la kwanza tafadhali na kumbuka katia ya wengi humu ni mimi ndiye niliyekuwepo TARIME muda wote nikifatilia kwa karibu hali ilivykuwa huko....

Tanzanianjema
 
Dogo Mnyika anatumiwa na akina Slaa na Mbowe kama buffer zone ya kukinga bullets zote zinazoelekezwa kwao. Dogo angalia hao wazee wasikuue kisiasa. Usifikiri wanakupenda wanaogopa nyota yako isizidi yao. Chunga sana. Slaa is sly and shrewd. He has his ambaitions. Huyo anajua hila za kivatican. Tafuta kitabu kilichoandikwa na David Yallop 'In God's Name'. Slaa hawezi kukubali umzidi katika medani za siasa ndani ya CHADEMA. Usiende kichwa kichwa watakuumiza. Hata huyo RA anaweza akaungana na Slaa kukumaliza. Hiyo ndiyo siasa dogo.
Haya ni mawazo mgando ya mtu aliyekata tamaa kama suleiman. Nampa pole.
 
Kama ni kweli,hakuna shaka kwamba kumtumia mtu msg za namna hiyo ni tabia za 'utoto' maana inaonyesha mnyika ameshindwa kukabiliana 'hisia' zake'!! With due respect, Mnyika unahitaji kukomaa kisiasa katika hilo eneo...maana mimi ninavyofahamu tabia za kutumiana msg za matusi/hasira ni za 'kitoto.
 
Kama ni kweli,hakuna shaka kwamba kumtumia mtu msg za namna hiyo ni tabia za 'utoto' maana inaonyesha mnyika ameshindwa kukabiliana 'hisia' zake'!! With due respect, Mnyika unahitaji kukomaa kisiasa katika hilo eneo...maana mimi ninavyofahamu tabia za kutumiana msg za matusi/hasira ni za 'kitoto.

Una maana kuwa corrupted na kuendelea kutumia old fashion politics za kumuita FISADI kwa jina la MHESHIMIWA ama amuache ROSTAM aliendelea na mipango yake ya kishenzi hadi atakapofanikiwa ndipo MNYIKA asimame kumuomba ajiheshimu...

Kuna maana gani ya kuwa na wanasiasa vijana kama tutawalazimisha kuiga style za kizamani namawazo ya kizee.....

MNYIKA usimwachie huyo, najua kesho atakuja na story nyingine dhidi yako lakini simama kidete na tuko pamoja.......FISADI ni FISADI na anapaswa kukabiliwa uso kwa uso......

Tanzanianjema
 
Now wait a minute, Mnyika tuwekee namba ya Rostam kwenye PM zetu, ili wale wenye ubavu na uchungu na taifa letu tumtumie more SMS zaidi,

Enough is enough, kama haelewi huo ujumbe wa Mnyika, basi tupe namba yake tumtumie SMSs zaidi, kitendo ulichokifanya ni kikubwa sana kuliko hata kumfikisha mahakamani, haya sasa atuuuwe wote na ajali kama anaweza!

Yes I said it! tumechoka sasa!


Mkuu I support this by 100%, Mnyika tu Pm hiyo number ya RA atambue hasira yake. Na nyie mnaosema eti hizi ni siasa za kitoto kwa hiyo mnataka kutuambia RA na kundi lake ndio wana siasa za kiutu uzima. Au ile press conference ya RA pale Kempiski ndio siasa za kiutu uzima???????
 
Mnyika ni PM hiyo namba ya fisadi nami nimtumie sms yakumwambia kwamba yeye ni fisadi mtandao.
 
Namba ya Rostam Aziz niliyoona kwenye kitabu cha simu za wabunge ni hii hapa:0754555555.

Mbona huyu dogo Mnyika hasikiki tena kwenye vyombo vya habari toka siku ile? Au ndio ameshamalizwa kisiasa?

PM
 
Mnyika nilimkanya waarabu wa Tabora sio wakuzoea, ccm wenyewe wanawagwaya.
 
Hivi nani alisoma siasa za wajamaa wa njozi? Mnafikiri fisadi atabadilika kwa kuzomewa? watauchuna tu sana sana na kubadilisha namba.

Fisadi wanatakiwa kupelekwa mahakamani, hayo mambo mengine yote ni sawa sawa na kelele za chura ambazo hazimzuii ng'ombe kunwa maji.
 
Dogo Mnyika uso kwa uso na Balille+Rostam Aziz

Katika hali inayoashiria kwamba sasa mambo yaliyonyuma ya pazia yanaanza kujitokeza hadharani. Dogo Mnyika ameanza kugongana vichwa na Ballile+Rostam Aziz. Katika kikao cha Jukwaa la Wahariri za jana, baada ya Sakina Datoo kueleza wazi wazi jinsi habari za magazeti matano zilivyofanana na Zitto kueleza jinsi gani habari hizo zilivyokuwa si za kweli. Mhariri wa gazeti la RAI hakuweza kukanusha hali hiyo badala yake alipopata muda kueleza hali hiyo, akasema kwamba wa kulaumiwa kutokana na kuliingiza taifa katika hali hiyo ni John Mnyika ambaye kauli zake ndizo zilizoliingiza taifa kwenye matatizo.


Bwana Ballile alitumia muda wote kumshambulia Bwana Mnyika. Ndipo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Sakina Datoo, alipompa nafasi Bwana Mnyika naye kuweza kufafanua hali hiyo. Katika majibu yake kwa Ballile, Bwana Mnyika alitangaza wazi kuwa gazeti la RAI ndilo lililopotosha na kuudanganya umma, na kuliingiza taifa kwenye hisia tofauti kuhusu Kifo cha Chacha Wangwe. Bwana Mnyika akarejea taarifa za gazeti la RAI la alhamisi ya 31 Julai, 2008 lililokuwa na Kichwa cha Habari “Wangwe kauwawa” kuwa ndilo lilochochea hisia miongoni mwa wananchi kuhusu mauji na hatimaye yakatokea yaliyotokea Tarime siku hiyo na baadaye magezeti ya Ijumaa 1 Agosti, 2008 nayo yakabeba habari zisizo za kweli kuhusu Mbowe kukaribia kukatwa na mapanga na kuhusisha kifo hicho na Risasi. Bwana Mnyika alieleza wazi kwamba habari hiyo ukusara wa Mbele ambayo ilikuwa na by line inayosema “Wataka Polisi iwabane Mnyika na Mallya”, ililenga kujenga hisia za wasomaji kumhusisha yeye na kifo cha Wangwe.


Bwana Mnyika alielezea kwamba siku ya pili baada ya habari hiyo kutoka waandishi wa habari walifika kutaka msimamo wake kuhusu habari hiyo lakini alikataa kusema chochote kwa kuwa hiki ni kipindi cha maombolezo badala ya malumbano. “Leo naomba niwaambie wahariri, kwamba naendelea kutafakari kuhusu habari hiyo, na pindi kipindi cha maombolezo kitakapokwisha, nitawaita waandishi kueleza hatua nitakazochukua kuhusiana na gazeti hilo’, alisema Bwana Mnyika. Akiichambua habari hiyo, Bwana Mnyika amesema pamoja na kichwa cha habari kutaka polisi wamhoji, ndani ya habari yenyewe hakuna mahali popote ambapo chanzo chochote kimesema ahojiwe na polisi.

Akichambua aya ya kwanza na ya pili ya habari, ambayo inaeleza kwamba msimamo wa “wazawa wa Tarime” kuwa “chacha ameuwawa’ umechochewa na kauli yake, Bwana Mnyika akamhoji Balille mbona habari yenyewe haitaji kauli ya Bwana Mnyika inayolalamikiwa na ‘wazawa’ hao wala katika habari yenyewe hailezwi popote wazawa hao kuhusisha kauli zao na msimamo wa Bwana Mnyika. Akichambua aya za mwishoni mwa Habari hiyo, ambayo inataja kwamba msimamo wa Dr Slaa ulikuwa ni kutaka uchunguzi ufanyike wakati Bwana Mnyika alitoa taarifa kwamba vyombo vya habari kuwa kifo hicho hakitokani na mgogoro ndani ya CHADEMA.

Chini ya maneno ya habari hiyo, gazeti la RAI likaweka maswali yafuatayo: Kwanini Mnyika akimbie kutoa kauli hii? Je, Mnyika ni polisi kutangaza mazingira ya kifo cha Wangwe?Je, Mnyika alikuwepo eneo la tukio?, Je, Ni kinga ipi anayotaka kuweka Mnyika? Kutokana na Habari hiyo kuwa na maswali hayo, Bwana Mnyika aliweka bayana kwa Ballile kwamba maswali hayo yaliongezwa na RAI ili kujenga hisia kwa msomoji kwamba yeye anahusika na kifo cha Wangwe. Akichambua mapungufu ya hoja hiyo. Alisema, anasikitika kwamba katika kipindi chote cha msiba mpaka Ballile anaibua hoja hiyo katika Jukwaa la Wahariri, gazeti la RAI halijawahi kufanya mahojiano yoyote na yeye wakati wowote.

Mnyika akaendelea kuelezea kwamba wao kama CHADEMA wanafanya kazi kama timu, na pindi habari za msiba walipozipata usiku walipeana taarifa kamili. Na hata asubuhi waliendelea kupeana taarifa mbalimbali ili kutoa misimamo bila kukinzana. Akasema kwamba siku hiyo ya Jumanne 29 Julai 2008, waandishi wa habari walimfuata ofisini kuuliza jinsi CHADEMA ilivyopokea msiba huo mzito. Alieleza bayana kwamba waandishi wengi walifika baada ya kikao cha sekretariati ya chama hicho ambayo yeye kama kaimu katibu mkuu, alikuwa Mwenyekiti wa Kikao. Anasema akawaeleza waandishi hao jinsi ambayo wamekipokea kifo hicho kwa mshtuko na masikitiko makubwa na kwamba wataendelea kumkumbuka Chacha kama kiongozi jasiri aliyesimamia yale aliyoyaamini.

Anasema mara baada ya kuhitimisha kutoa kauli hiyo ya chama ya jinsi ambavyo chama kimepokea msiba huo, waandishi wa Mwandishi wa Habari wa Mtanzania, na wa TBC1 waliuliza maswali, wakati yule wa Mtanzania akiuliza swali kwamba habari za mitaani zinasema kwamba CHADEMA ndio imemuua Chacha nini kauli ya chama kuhusu suala hilo? Yule wa TBC1 aliuliza kama kifo hicho hakitokani na mgogoro ndani ya CHADEMA? Bwana Mnyika alisema kwamba CHADEMA haihusiki na kifo hicho wala hakihusiani na mgogoro ndani ya chama hicho, na kwamba taarifa za awali walizozipokea toka kwa Kamanda wa Polisi ni kwamba kifo hicho kimetokana na ajali.

Bwana Mnyika alisema kwamba alilisitiza kuwa watu wasianze kuitizama CHADEMA badala yake vyombo vya usalama ndio vinawajibu wa kutoa taarifa kamili. Katika jukwaa la Wahariri, Bwana Mnyika aliweka bayana kwamba huu ndio uliokuwa msimamo wa pamoja, na ni msimamo huo huo ulitolewa na viongozi wengine wa CHADEMA siku hiyo akiwemo Dr Slaa, na hata viongozi wa kiserikali akiwemo Spika wa Bunge na Rais wa nchi katika salamu zao. Bwana Mnyika akamhoji Balille kwamba ni vipi kati ya watu wote walionukuu taarifa ya polisi kuwa kifo hicho kimetokana na ajali hawakuandikwa na RAI kwamba wamekurupuka kujikinga na kutaka wahojiwe na polisi kama alivyoandikwa yeye na gazeti hilo? Bwana Mnyika akaendelea kusema kwamba kinachoshangaza zaidi ni kuwa Jumatano ya tarehe 30 Julai, 2008 yeye mwenyewe alimwandikia Barua IGP kutaka uchunguzi wa utata wa mazingira ya ajali uliotokana na kauli tofauti tofauti ambazo zilitolewa na Deus Mallya ukilinganisha na watoto wa marehemu kuhusiana na ajali hiyo.

Wakati vyombo mbalimbali vya habari viliinukuu barua hiyo, ikiwemo gazeti dada la Mtanzania, Gazeti la RAI halikutumia kabisa habari hiyo. Bwana Mnyika akahitimisha kwa kumwambia Balille hadharani kwamba kwa mwelekeo wa Habari hiyo umeonyesha wazi kwamba aliyekuwa analengwa kuchafuliwa ni Mnyika na kwamba habari hiyo imekiuka misingi ya maadili ya uandishi wa habari na hivyo akaeleza wazi wazi kwamba anatarajia kuchukua hatua juu ya gazeti hilo. “ Hapa si mahali pake kuzungumzia hilo, bado tuko kwenye maombolezo, na hapa tulikuja kukutana na Jukwaa la Wahaririri. Pindi wakati ukifika nitawaita waandishi wa habari na kuwaeleza hatua nitazochukua”, alisema Mnyika.

Wakati huo huo, mmiliki wa Kampuni ya Habari Corporation yenye gazeti la RAI, Bwana Rostam Aziz amelalamika kwa baadhi ya wabunge, baadhi ya viongozi wa vyama vyama vya siasa na na baadhi ya wahariri kwamba Mnyika amemtukana kupitia simu yake ya mkononi. Hata hivyo alipotakiwa kueleza ametukanwa matusi gani, bwana Rostam hakuwa tayari kueleza. Kwa upande wake Bwana Mnyika alipoulizwa amekana kumtukana Bwana Rostam na kutaka aulizwe na atoe ushahidi ametukanwa nini. “Mimi nimemwambia kuwa nimesibitisha kuwe yeye ni fisadi. Sasa kama anasema mimi kumuita fisadi ni matusi basi aende mahakamani”.

Na nimemwambia wazi wazi , sikutaka kuzunguka, nimemwandikia kwenye SMS kuwa yeye ni fisadi. Na sijajificha kwa kweli. Nimewandikia kwa namba yangu na nimeandika jina langu ili abaki na ushahidi akipenda aende mahakamani. Wadadisi wa mambo, wanasema kwamba uamuzi huu wa Bwana Mnyika unaweza kuzua mivutano kati yake na Ballille+Rostam. Itakumbukwa kwamba mara baada ya uchaguzi mkuu 2005, wakati Makamba anafanya jitihada za kumnunua Mnyika kwenda CCM alimtumia Bwana Rostam Aziz. Hata hivyo, Bwana Mnyika alikataa kata kata akieleza kwamba yeye hana bei(price less).

Suala hili la CCM kutaka kumnunua Mnyika liliwahi kuwekwa hadharani na Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe. Kwa mujibu wa vyanzo vilivyo karibu na Bwana Balille, mara baada ya kikao hicho cha Jukwaa la Wahariri, Bwana Balille alimjulisha Rostam mambo yote na umuhimu wa kuandaa mbinu ya kumkabili Bwana Mnyika katika suala hilo. Kwa mujibu wa chanzo hicho, imekuwabaliwa kwamba kikao kitafanyika ikiwemo kupanga mbinu ya kukabiliana na Zitto Kabwe kutokana na uamuzi wake wa kukabiliana na wahariri wa vyombo vya habari kutokana na kuruhusu habari ya uongo ya kupikwa kuweza kutolewa na vyombo vyao. Katika mkakati huo, imeelezwa kuwa kiongozi mmoja wa upinzani aliyekwenda mazikoni Tarime atashirikishwa.

PM

Kwa maoni yangu huu ndio mwanzo wa kifo cha kisiasa cha Bwana Mnyika
Maandishi marefu sanaaaa kama Uandishi wa John Mnyika,KULIKONI?
 
Namba ya Rostam Aziz niliyoona kwenye kitabu cha simu za wabunge ni hii hapa:0754555555.

Mbona huyu dogo Mnyika hasikiki tena kwenye vyombo vya habari toka siku ile? Au ndio ameshamalizwa kisiasa?

PM
Jamani kuweka simu za watu hadharani inafaa? naona itolewe kuweka heshima kwa Rostam,hata kama hatumpendi.
 
Jamani kuweka simu za watu hadharani inafaa? naona itolewe kuweka heshima kwa Rostam,hata kama hatumpendi.

Mbona Kikwete alisema simu yake iko hadharani. Na IGP Mwema aliweka simu yake kwetu na kutuelekeza tuichape gazetini na tukaitoa? Rostam si mbunge wa Igunga? Kama hataki wananchi wa asili ya jimbo lake waliosambaa kote duniani waone namba yake basi aseme. Angetaka private life ya kutofuatwa na mapaparazi asingeingia kwenye siasa. Halafu mbona pamewekwa namba za watu wengi tu hapa JF sijakusikia ukilalamika?

PM
 
Kama huwezi kumwambia FISADI kwamba wewe ni FISADI na hufai kwenye jamii huna haja ya kupambana na ufisadi kwa kupiga kelele

Namba yake hiyo hapa kwa yeyete anayetaka kumwambia katuchosha na mambo yake ya kifisadi
Tupo pamoja Mnyika..
 
Back
Top Bottom