nakuunga mkono asee,hapo kuna mawili either kweli mwanamke anasumbuliwa au anamsaliti huyu mdau kwa makusudi ila anajaribu kutafuta huruma kwa mpnz wake ili kuchiti kwake kuwe hali,aiwezekani askar anayejua mamlaka zote za kinidhamu aje alalamike/ashitaki kwa mpenz wake ambaye si askari(atamsaidia nini?)kituo chochote kina viongozi kuanzia ngazi ya chini mpk juu ambao naamini aiwezekan wote wakawa upande mmoja,kama kweli anaamini ananyanyaswa kwa sabb ya mapenz akusanye ushaidi ambao utamkonect askar na tuhuma hizo otherwise chenga tuUmeandika maelezo yasiyo sahihi pengine kutokana na kutojua polisi wanafanyeje kazi na hata kwa kuwa umeambiwa kitu kutoka upande mmoja wenye maslahi yako.
Kwanza huyo mpenzi wako anaweza akawa ni tatizo kwa sababu yeye ni askari. Nilitegemea akusanye ushahidi wa kutosha kwanza kuonyesha kama anatongozwa na mkuu wake. Kwa kawaida kuna kipengele fulani katika majeshi ambacho kinakataza maafisa wenye nyota kuwatongoza askari katika mazingira fulani. Lakini iwapo mazingira hayo hayapo, mwanamke yeyote kutongozwa ni kitu cha kawaida.
Kwa ushahidi wa yeye kutongozwa na mazingira yakawa yanaruhusu halafu yeye akakataa, askari huyo angeambatisha ushahidi wa mazingira kuwa ananyanyaswa kwa sababu ya kukataa kuwa mpenzi wa mkubwa wake.
Kwamba amekulalamikia wewe ni sawa kwa sababu wewe ni mpenzi wake lakini ni vyema umshauri akusanye ushahidi sahihi wa nilichokieleza hapo juu kwa sababu tayari hata wewe umeingia katika mtego huo huo wa kupatiliza dhambi bila kuwa na ushahidi wa kutosha.
Kazi za majeshi zina mlolongo wa utendaji kiasi kwamba usipoangalia na hasa kwa jinsia na wasichana wetu wa kisasa wanaopenda kulalamika unaweza kujichanganya na baadaye ukapata hasara. Umewalaumu watu wengi kiasi ambacho kinanipa shida kufikiri kama watu wote hao ni wapuuzi.
Kunyanyaswa kimapenzi kupo lakini kwa mazingira ya teknolojia ya kisasa ni rahisi kupata ushahidi ambao hata kama angetetewa na baba yake mzazi bado kuna siku angemkana. Lakini pia upo ulalamishi wa kizembe unaotolewa na watoto wa kike kwa visingizio vya mapenzi na hasa kunapokuwepo ukiukaji wa taratibu au wakati ambao watu wa shughuli za ulinzi wanapopungua kutokana na majukumu mengine.
Wakati huo, mtu aliyetakiwa kuwa zamu yuko kwingine na hivyo kunafanyika replacement. Bado kuna kazi ngumu kama magwaride na doria. Iwapo mchumba wako ni dot com na pengine anahisia za kunyanyaswa na bosi, hilo pia linaweza kujitokeza.
USHAURI: MWAMBIE HUO MCHUMBA WAKO AKUSANYE USHAHIDI WA KUTOSHA ILI ANAPOPELEKA MALALAMIKO KUWEPO NA LOGIC.
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app