Wandugu,
Licha ya kuwa mtanzania mweusi nachukizwa na viongozi na baadhi ya watu kuwaita wazungu mabeberu.
Ni wazi neno beberu linatumika kuwabagua watu weupe hasa wa nchi za magharibi.
Kuendelea kutumia maneo ya aina hii kwenye dunia ya kisasa iliyounganika karibu kwa kila kitu kunaonesha ni kwa kiasi gani watanzania bado tupo gizani na tuna safari ndefu kuyafikia maendeleo ya kweli.
Ni wazi mfumo wa uchumi wa kidunia unainyonya Africa.
Lakini hauzuii nchi za Africa kunufaika ikiwa viongozi wake watakuwa wajanja kung'amua namna ya kupata kitu kutoka mfumo uliopo bila ya kuzua ugomvi.
Mzee JK aliwahi kusema 'ruhusu kuliwa ili nawe ule'.
Kauli hii inamaanisha kuwa ukijifanya mbabe dhidi ya mataifa yalioendelea tangu zaidi ya miaka 200 iliyopita na kuwaita mabeberu utaula wa chuya.
Kuwaita wazungu mabeberu ni ujima na ujamaa ambao haujawahi kufanikiwa na hautofanikiwa.
Tunachekelea na kuona inapendeza kuwaita wazungu mabeberu ilihali wao wakituita "tundu la choo cha shimo la udongo" nchi nzima mapovu.
Fikiria mfano meingine uwe London wazungu waanze kukuita "mweusi mweusi mweusi" dunia yote italipuka. ..ooh ubaguzi ubaguzi....lakini sisi tunaona raha kuwaita "mzungu mzungu mzungu" wapitapo kwenye mitaa yetu.
Tujifunze ku balance na kuheshimu utu wa watu wote, weusi kwa weupe.
Usiku mwema.