Mnatuchukua vijana kutulimisha JKT, Ajira zikitokea mnaajiri watoto wenu

Great YHC

Senior Member
Jan 1, 2024
167
596
Acheni kutuchukua vijana Kwenda JKT mkatulimisha kisha mkatuacha MTAANI, Ajira zikitokea mnaajiri watoto wenu ambao hata JKT HAWAJAPITA, halafu mtaani wanajisifu, Watu wamekaa JKT miaka 3 halafu mnambiwa mkajiajiri kujiajiri nyoko madako yenu.
 
JKT lengo lake kubwa sio kutoa ajira bali ni kumjenga kijana kwa kumpa mafunzo ya awali ya ulinzi na usalama, kumfundisha kazi na ukakamavu haya ya kutumika kama chujio la ajira ni secondary aims Kama vile ambavyo lengo la elimu ni kutoa ujinga na sio ajira, Ajira itakuja baada ya kutoa ujinga.

Cha msingi unapokuwa JKT jaribu kuigeuza kama fursa kwako fanya kazi, kuwa mbunifu, acha uvivu na kufuata mkumbo, kuwa mdadisi show them why they have to take you utapata tu hizo nafasi tena nafasi nzuri tu mkuu, Wako vijana wenye uthubutu na ambao wapo vizuri upstairs Serikali inawahitaji hasa kwenye kada za ulinzi na usalama.

Tatizo letu huwa tunakumbuka shuka na kushakucha ingawaje sipingi kuwa connection zipo na hii ni kila sehemu kwenye kila sector ndio mfumo wa dunia mkuu.

All in all usikate tamaa omba kila nafasi zikitoka na mtangulize Mungu.
 
Akuna ujuzi unaopata kule kaka zaidi ya kufanya kazi zawatu tuu ,
Ujuzi upo mkuu kule si kuna range mnalenga shabaha, kwata, unafundishwa kutumia silaha japo ni basic tu, kuna vitengo mbalimbali unaweza jifundisha ufundi wa magari au ujenzi n.k
Lengo langu ni kuwa kwenye kila kitu iwe kinaonekana kidogo mbele za watu wewe kigeuze kuwa fursa mfano mnaenda range msikilize kamanda vizuri kisha lenga shabaha zako kwa usahihi na usihishie hapo muulize maswali ni jinsi gani unaweza kuwa bora katika ulengaji shabaha hiyo itamfanya akuone kwanza unajiamini pili unataka kujifunza kumbuka hao makamanda ambao mpo nao kila siku ndio wanaajira zenu hasa hasa hao ma staff sergeant mpka luten .
 
Brother ilikua zamani ,sasa hivi jeshi la kimkakati JKT sasa wanafanya miradi ya serikali,mafunzo ni sehemu ndogo sana ya jkt
Haya ninayoyasema unatakiwa kuyafanya tangu siku ya kwanza unafika JKT kwani kipindi kile cha kozi huwa muda mwingi ni mazoezi maovyoovyo kama yote na mafunzo mengine hilo la JKT kujihusisha na miradi ya kiserikali huwa mtafanya baada ya kumaliza kozi na hilo kwa JKT haliepukiki ndio maana likaitwa Jeshi la Kujenga Taifa hivyo ni wewe kujua jinsi ya kwenda nalo.
 
Acheni kutuchukua vijana Kwenda JKT mkatulimisha kisha mkatuacha MTAANI, Ajira zikitokea mnaajiri watoto wenu ambao hata JKT HAWAJAPITA, halafu mtaani wanajisifu, Watu wamekaa JKT miaka 3 halafu mnambiwa mkajiajiri kujiajiri nyoko madako yenu.
Hayo mafunzo ya miaka 3 ni dili kubwa sana kwenye mchakato wa kuipata Tanzania mpya. Ni vile tu bado hamjagundua.
 
Wanipotezea mda wangu Nina hasira sio ya kitoto
kweli nimeona una hasira sio ya kitoto,..😆😆😃😅😂🤣

Sitakaa nisahau, nilivyomaaliza sori za viatu kwa mwaka na nusu hivi, maofisini kuomba ajira, hadi watu wa karibu tu walinisusa..🥲

Pole sana mkuuu unaenda huko, unalimishwa kama punda na fimbo juu, kisha wanasema sasa umeiva waweza kujiajiri,umeiva kamanda, upo tayari kulipigania taifa lako bila mtaji wa jembe wala shamba wala soko la uhakika.....

Tatizo la Ajira lisikie tu..😓😓😞
 
Haya ninayoyasema unatakiwa kuyafanya tangu siku ya kwanza unafika JKT kwani kipindi kile cha kozi huwa muda mwingi ni mazoezi maovyoovyo kama yote na mafunzo mengine hilo la JKT kujihusisha na miradi ya kiserikali huwa mtafanya baada ya kumaliza kozi na hilo kwa JKT haliepukiki ndio maana likaitwa Jeshi la Kujenga Taifa hivyo ni wewe kujua jinsi ya kwenda nalo.
Kwa kuongezea ukiona miradi sensitive kwa Taifa au matukio maalum kama maafa huko ndipo pakukimbilia maana huwa panakuja na NEEMA.
 
Back
Top Bottom