SoC02 Ushauri kwa Serikali kuhusu utatuzi wa changamoto ya ajira kwa vijana wenye taaluma (wasomi)

Stories of Change - 2022 Competition

Mabogo Jr

Member
Jan 27, 2018
33
44
Tangu kuanza kwa Karne ya 21, imekuwepo changamoto ya ajira kwa vijana wengi wenye taaluma (Wasomi) katika mataifa mengi duniani ikiwemo Tanzania. Changamoto hii imekuwa kikwazo kwa vijana wengi kutimiza ndoto zao katika maisha, hivyo wengi wao wakijikuta wakiishi maisha yasiyo endana na uthamani walio nao, hali inayoweza pelekea kushindwa kuwa mifano bora katika jamii wanazo ishi. Janga hili la karne ya 21 linasababishwa na sababu mbalimbali kulingana na jamii (Taifa) husika. Kwa mfano maendeleo ya teknolojia katika baadhi ya maeneo ya shughuli za kiuchumi kama viwanda yamechangia sana katika kupunguza umuhimu na uhitaji wa nguvu kazi watu katika maeneo mbali mbali ya uzalishaji nk. Hivyo sababu zinaweza tofautiana kati ya taifa moja na jingine. Nikijikita zaidi katika jami yetu (Tanzania) Changamoto hii ambayo inatokana na sababu mbalimbali ikiwemo upungufu wa fursa za ajira kulingana na wingi wa wenye sifa na uhitaji, lakini pia aina ya mfumo wetu wa elimu hasa elimu ya juu. (Vyuo vikuu). Kwa kuzingatia takwimu zilizopo, zifuatazo ni sababu ni baadhi ya sababu za msingi zinazo changia ukuaji wa changamoto hii hapa Nchini.

Mfumo wa elimu hapa Nchini.
Mfumo wa elimu yetu hapa nchini unawajenga na kuwaandaa vijana (wanafunzi) kuwa wafanyakazi wa kuajiriwa, hivyo mafunzo mengi yaendana na dhana hiyo. Jambo hili hupelekea wanafunzi kusoma kwa bidii katika kutafuta matokeo (sifa) yenye kuwawezesha kuwa washindani kwenye soko dogo la ajira lililopo nchini. Hivyo mfumo wa elimu hauwapi mwanafunzi fursa ya kufikiria jambo nje ya ajira inayo endana na elimu yao. Hii inapelekea wahitimu wengi kupoteza muda wao mwingi wakijaribu kutafuta ajira jambo ambalo kwa miaka ya hivi karibuni limekuwa kama mchezo wa bahati nasibu.

Uchache wa nafasi za ajira.
Kulingana na sheria ya ajira ya hapa nchini, kama ilivyo katika mataifa mengine mtumishi wa umma ana fursa ya kuwa kazini mpaka wakati wa kustafu kwa mujibu, miaka 60. Jambo hili linamfanya mwajiriwa awepo kazini kwa muda mrefu kiasi cha kuwanyima fursa watu wengine wenye sifa na ambao hawakuwahi kupata nafasi za ajira. Hii inachangia kuwepo kwa utitiri wa wahitimu mtaani wasio na ajira rasmi, hivyo kwasababu hii idadi inaongezeka kila mwaka

Dhana potofu kuhusu.
Ni jukumu la kila mzazi kumuelewesha mtoto waelimu ili apate kuitafuta kwa bidii, kama haki yake ya msingi. Hata hivyo, umekuwepo utamaduni miongoni mwa wazazi au walimu kuwaasa watoto wao kuhusu manufaa ya elimu katika mfumo wa ahadi, mfano; "Soma mwanangu uje kuwa daktari kama mjomba wako" Hii injenga imani ya mtoto kwamba baada ya kumaliza masomo nitapata kazi fulani. Hata hii mioto ya shule, mfano; "Elimu ni ajira" inayo nafasi kubwa katika kumhakikishia mwanafunzi kile anacho kiwaza, kwamba nikimaliza kusoma nitakuwa mwalimu kama alivyo mwalimu fulani.

NINI KIFANYIKE ILI KUPUNGUZA CHANGAMOTO HII?

Mamlaka zake za elimu iboreshe mfumo wa elimu nchini.
Serikali kupitia mamlaka za elimu pamoja na wadau wengine wa elimu nchini nchini wakae na watafute njia mbadala ya kuelimisha wanafunzi, namaanisha uwepo ubunifu katika utoaji wa elimu kulingana na ngazi husika. Katika hili wataalamu wa elimu wajikite zaidi katika kufundisha elimu ya kujitegemea kwa wanafunzi ambayo kimsingi iambatanishwe na fani fulani ambayo inaendana na ndoto ya mwanafunzi husika. Ikishindikana sana basi uwekwe mfumo wenye kuambatanisha elimu ya ujasiriamali katika taaluma nyingine zitolewazo, Elimu ya ujasiriamali itakuwa kama njia mbadala ya kuwapatia kipato vijana wanao hitimu wakati bado hawajapata kuingia katika mfumo wa ajira rasmi.

Mamlaka za serikali ziandae muswada wa kupunguza muda wa mwajiriwa kustaafu kwa mujibu.
Binafsi, napenda kuishauri serikali itafakari kuhusu kupunguza muda wa mwajiriwa kuitumikia serikali. Muswada huu unaweza kuandaliwa kwa namna ifuatayo; #Mtumishi aitumikie serikali kwa miaka 15 tu kuanzia alipo ajiriwa kisha atatakiwa kustaafu kwa mujibu wa sheria hyo mpya. Hii itasaidia kupunguza idadi ya wasio ajiriwa ilihali wanazo sifa. Pia watu kujipambanua, kuwekeza (kujiajiri) mapema pindi tu wanapo anza kazi kuepuka adha ya kukaa bila kazi baada ya kustaafu. Ikiwa serikali italipitisha hili basi tutapata kuona unafuu wa changamoto hii kuanzia miaka 15 ijayo. Vijana sasa watapata fursa ya kuitumikia serikali yao kabla umri hauja watupa mkono kisha kuachia nafasi kwajili ya vijana wengine. Zipo faida za utekelezaji wa ushauri hili ni hizi.

#1.
Kuwepo kwa nafasi za ajira ambapo itakuwa karibu kila kijana atakuwa na nafasi ya kupata ajira mapema kama dhamira ya wengi ilivyo, lakini pia nafasi ya kujiajiri kupitia fedha yake mwenyewe tena katika umri mdogo kuliko kusubiri mafao ya uzeeni akiwa na miaka yake 60 nakuendela, hapo kuchanganyikiwa ni kugusa tu maana utakuta alijisahau kipindi yupo katika ajira kwa jeuri ya miaka 60, akabaki akiwashangaa vijana wasio na ajira jinsi gani hawaeleweki mtaani sambamba na kuwaita vibaka. Hivyo mamlaka za serikali kama zitaona busara katika hili, basi tutapata kuona vijana wetu wakipata ajira kama walivyo pewa motisha na wazazi wao tangu walipo kuwa shule ya msingi. Kwa mfumo huu taifa litashuhudia ongezeko la mapato ya ndani yatokanayo na ukusanywajin wa kodi kutokana na kuwepo kwa wimbi kubwa la ajira binafsi (kujiajiri).

#2.
Muelekeo wa taifa, yaani dira ya taifa sasa itakuwa kama ilivyo kauli mbiu zetu "vijana ndio nguvu kazi ya taifa". Hili litakuwa dhahiri maana nina imani hakuna kijana utamkuta mtaani hana kitu wakati kila mwaka wastaafu ni wengi na wanafungua miradi nabado kila mwaka wanao ajiriwa ni wengi. Suala la mzunguko wa fedha litarudi mikononi mwa vijana na hiyo ndiyo maana halisi ya vijana kuwa nguvu kazi ya taifa. Yote haya ni mawazo yangu, natamani serikali ilielewe hili maana hakika kwa njia hii, kama taifa tutakuja kuwa mfano wa kuigwa kwasababu tatizo la ajira ni la dunia nzima hvyo mataifa mengi yataiga kutoka kwetu. Kama taifa la leo, na tuthibitishe kwa watoto wetu (taifa la kesho) kuwa #Elimu ni ufunguo wa maisha.

Je ni upi mtazamo wako?

-Ernest C. M. Mabogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom