Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
MNATAKA WENZENU WALE WAPI?

Anaandika, Robert Heriel

Unajua kuna watu ukiwatafakari utabaki unawashangaa Sana. Sijui wanafikiri kaa kutumia kiungo gani. Maana Kama wangetumia ubongo wasingefikiri Kwa namna hiyo.

Unapojadili Jambo lolote lazima ushirikishe akili yako vyema ili usijidhalilishe.

Unaposema watu wasiende kwenye makanisa ya upako au manabii wa dot.com, unataka HAO manabii na wenye makanisa Wale wapi?

Ikiwa hawavunji sheria yoyote ya nchi. Unataka Wale wapi?

Wenzenu wamejiajiri wanahangaika na maisha kufanya kile wanachoona kitawapa ugali, alafu mnageuka wachawi kuwazuia wateja wao wasiende huko. Mnataka hao manabii wawe majobless? Come on! Tumia akili yako hiyo.

Unaposema watu waache kushinda mitandaoni, unataka kina Maxence Mello Wale wapi kunguni weee! Hawa mods humu unataka waje hapo kwako uwape kazi ya Kuosha vyombo? Hivi hamjui kuwa moja ya maombi ya waanzilishi wa Apps ni kupata wafuatiliaji wengi na members wengi katika Apps zao. Hao ndio wateja wao. Kupitia hao wanapata pesa Kwa kupata matangazo Kwa makampuni mengine, lakini wewe na akili yako ya Mbuzi hujui Hilo. Elewa kuwa kila KAZI inawateja wake hivyo kabla hujaongea fikiri Kwanza kabla ya kutenda mbona wahenga walishasemaga.

Unapowaambia watu waache kwenda Kwa waganga wakienyeji unatumia Akili au matundu ya pua yako kufikiri? Eehe!

Unataka waganga wakale Kwa Bibi yako sio, wewe Kama huamini mambo ya uganga kinachokuuma ni nini wengine wakienda huko. Mbona wao hawakuingilii na mambo yako.

Unajua ni watu wangapi wamejiajiri kwenye uganga.

Kwa akili zako finyu unafikiri KAZI ni Ile tuu unayoifanya wewe! Tumia Akili.

Jambo kama sio kosa kisheria achana kuwaponda wanaolifanya.

Unapowaambia watu waache kunywa pombe uliwahi wafikiria wenye viwanda vya pombe? Walioajiriwa viwandani, uliwahi wafikiria madereva wanaosafirisha hizo pombe, uliwahi fikiria wahudumu wa Bar na wamiliki wa Bar.

Uliwahi wafikiri wamiliki WA vyombo vya habari wanaopata pesa za matangazo kupitia makampuni ya pombe?
Au unaongea tuu Kama Mpumbavu!

Wewe unataka wenzako wakale wapi? Kisa wewe mtoto wa Sheikhe au mchungaji unafikiri watoto wote ni wachungaji?

Kisa wewe ni mtoto wa msabato kama Taikon unafikiri kila mtu ni Msabato?

Unataka watu wakale wapi kenge maji wewe!

Kitu Kama sio kosa kisheria Acha watu wajiajiri waendeshe maisha yao.

Unaposema watu waache uchawa na upambe ulitaka HAO watu Wale wapi?

Mtu kajaliwa mdomo, anajua kuzungumza bila ya haya lakini havunji sheria ulitaka akalime viazi kama wewe kisa unaminguvu? Sio kila mtu ananguvu Kama wewe, sio kila mtu ni domo zege Kama wewe!

Acheni watu wafanye kazi wazipendazo bila kuvunja sheria waendeshe maisha Yao.

Kuna waliochagua kuwa machawa na wapambe wa dini na miungu yao tukawaita wachungaji na masheikhe mbona hao hamuwasemi?

Na wapo walioamua kuwa machawa na wapambe wa binadamu wengine tunawaona kwenye Siasa kutwa kucha kuwasifu watawala hasa Rais, huku wengine wakiwasifu matajiri na watu mashuhuri. Kwao mbona mnaona nongwa?

Mlitaka watu Wale wapi?

Oooh! Usanii na muziki ni haramu sijui ni dhambi! Hivi mnaposema haya mliwahi kufikiria wamiliki wa Bar, Casino, na Club wataendeshaje Club zao pasipo hao wanamuziki?

Mliwahi fikiri mtu ataburudikaje Kwa chakula kitamu na pombe bila wanamuziki?

Mliwahi fikiri Vyombo vya habari hasa Redio zitaendeshwaje pasipo muziki?

Hao Wasanii mlitaka wale wapi na Kwa namna ipi?

Sikiliza Gospel au Kaswida kama hutaki mambo ya kidunia. Lakini elewa kuwa wapo wanaoishi Duniani na wanapenda mambo ya Duniani ukiwemo muziki wa kidunia.

Waacheni wale Kwa kazi zao. Kama hawavunji sheria za nchi.

Alafu mbona wapo wazi Kabisa kuwa mambo hayo ni Kwa wenye kuanzia miaka 18 kuendelea yaani watu wazima. Kosa ni lako Kama utawaachia watoto Luninga.

Unataka Wale wapi?
Elewa kuwa kila Jambo linawatu wake. Ila Kama linavunja sheria ndio unayohaki ya kuongea. Au kama linadhuru jamii unayohaki ya kuongea.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom