Je, akili inaweza kuudhibiti moyo?

Je, akili inaweza kuudhibiti moyo?

OMKEIT 93

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2026
Posts
248
Reaction score
371
“Kuna minyororo ambayo haionekani kwa macho, lakini humfunga mtu kuliko chuma.

Minyororo hiyo ni hisia.”
Moyo unataka kile kinachokufurahisha leo.
Akili inapaswa kujiuliza: “Hiki ninachotaka leo, kitanigharimu nini kesho?”

Ndiyo maana mtu anaweza kujua kabisa kwamba jambo fulani linamuumiza, lakini bado akarudi kulifanya.
Anaweza kujua mtu fulani hamfai, lakini bado akampenda.
Anaweza kujua matumizi fulani yanamfilisi, lakini bado akaendelea kutumia.
Anaweza kujua hasira itamletea matatizo, lakini bado akasema maneno ambayo baadaye atayajutia.

Kwa nini?
Kwa sababu katika maamuzi ya mwanadamu, hisia na fikra za kimantiki hufanya kazi kwa kushirikiana; maeneo kama amygdala yanahusika katika thamani na hisia, huku prefrontal cortex ikihusika sana katika kupanga na kutathmini hatua zinazowezekana.

Kama akili inajua jambo ni baya lakini moyo bado unalitaka, nani anapaswa kushinda?
👉 Moyo unaosema: “Nataka.”
au
👉 Akili inayosema: “Usifanye, utajuta.”
Na je, kujizuia kufanya jambo unalolitamani ni udhaifu wa moyo—au ni nguvu ya akili?

Huenda ushindi mkubwa wa mwanadamu si kupata kila kitu anachokitamani.
Huenda ushindi mkubwa ni kuwa na uwezo wa kusema “HAPANA” kwa kitu ambacho moyo wako unakitamani sana, kwa sababu akili yako imeona madhara yake.

Sasa wewe unaonaje: JE, AKILI INAWEZA KUUUDHIBITI MOYO, AU MWISHO WA SIKU HISIA NDIZO HUWA NA NENO LA MWISHO?
 
Inaonekana hata hujui kazi ya moyo,
hakuna uhusiano wowote kati ya moyo na akili/Brain katika maamuzi ya Binadamu,

Moyo ni Pump inayo sukuma damu through your body,

Kazi ya kufikiri,memory,movement feeling na automatic action kama kupumua na mapigo ya moyo hufanywa na part of the brain inayoitwa Celebrum,

Huo moyo wenyewe unafanya kazi kwa maamuzi ya brain kwa kupokea tiny electrical and chemical signal kwa kupitia kwenye nerves kutoka kwenye brain,hata mapigo ya huo moyo hupata amri kutoka kwenye brain ''Celebrum''
 
Kama akili inajua jambo ni baya lakini moyo bado unalitaka, nani anapaswa kushinda?
👉 Moyo unasema ''Nataka''
au
👉 Akili inasema ''Usifanye utajuta''
Na je, kujizuia kufanya jambo unalolitamani ni udhaifu wa moyo—au ni nguvu ya akili?
Kwahiyo hapa Moyo unabishana/unashindana na Human brain katika kufanya maamuzi sio?

Futa hii tusije kuja kuchekwa na kizazi kijacho huko mbeleni,au waambie Mod's waipeleke kwenye jukwaa la vichekesho.
 
Inaonekana hujui kazi ya moyo,
hakuna uhusiano wowote kati ya moyo na akili/Brain katika maamuzi ya Binadamu,

Moyo ni Pump inayo sukuma damu through your body,

Kazi ya kufikiri,memory,movement feeling na automatic action kama kupumua na mapigo ya moyo hufanywa na part of the brain inayoitwa Celebrum,

Huo moyo wenyewe unafanya kazi kwa maamuzi ya brain kwa kupokea tiny electrical and chemical signal kwa kupitia kwenye nerves kutoka kwenye brain,hata mapigo ya huo moyo hupata amri kutoka kwenye brain ''Celebrum''
Kwanini ukiachwa moyo ndiyo unaomuia moyo ndiyo unaovunjikavunjika
 
Watu wengi hudhani moyo hua una feel au ndio wenye maamuzi kama vile kupenda! hakuna kitu kama hicho,kila kitu kinaanzia kwenye Brain,

Eti utasikia Moyo wangu umekupenda,
Toka lini moyo ukawa na hisia ya kupenda!
"Ubongo wangu umekupenda"🤣🤣🤣🤣
Nadhani Neno "moyo" hutumika kuelezea "Nia" au "Dhamiri" ya mtu na sio kiungo cha mwili kinachosukuma damu!.
 
mnachokosea ni kwamba hamjui ya kuwa moyo ndipo panapo beba hisia na uhai kwenye vitabu vya dini inasema linda sana moyo wako ndipo chemchem ya uhai ilipo

Mit 4:23​

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima
 
Hata dhambi huanzia moyoni ndiyo maana tunaambiwa kutamani mwanamke tayari uneshazini kunbe ulianza moyo kupenda akili ufuata kuweka mipango ya kutimiza haja
 
mnachokosea ni kwamba hamjui ya kuwa moyo ndipo panapo beba hisia na uhai kwenye vitabu vya dini inasema linda sana moyo wako ndipo chemchem ya uhai ilipo

Mit 4:23​

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima
Walio andika vitabu vya dini hawakua na uelewa wa mambo , ubongo ndio unafanya maamuzi, ni vile tu kwa lugha ya kijamii moyo humaanisha hisia.
 
mnachokosea ni kwamba hamjui ya kuwa moyo ndipo panapo beba hisia na uhai kwenye vitabu vya dini inasema linda sana moyo wako ndipo chemchem ya uhai ilipo

Mit 4:23​

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima
Mkuu kinachomaanishwa hapo ni "Nia" au "Dhamiri" sio moyo unaosukuma damu!.

Uovu au Wema wa mtu upo kwenye Dhamiri yake!
 
mnachokosea ni kwamba hamjui ya kuwa moyo ndipo panapo beba hisia na uhai kwenye vitabu vya dini inasema linda sana moyo wako ndipo chemchem ya uhai ilipo

Mit 4:23​

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima
Hii ni issue ya kisayansi sio issue ya kidini,
Toka lini Moyo ukabeba hisia? Kama ni imani basi endelea kuamini ila uhalisia haupo hivyo,

Huwezi kusema kinachokula chakula ni miguu wakati chakula hupitia mdomoni,yani kazi inayofanywa na brain wewe unataka kutuaminisha kua kazi hiyo hufanywa na Moyo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom