Mnaotumia bidhaa mpya ya microsoft ya windows 10 someni tena hapa mjue hatari inayowakabili

Mada hii imeshajadiliwa na wenzetu kabla. Hata hivyo kutokana na umuhimu wake ni muhimu kuijadili katika vipembe vingine kuzidi kuifahamu

Microsoft wameshatangaza kuwa toleo la windows 10 liliopo sasa litafikia ukomo ifikapo oktoba 2025.Watumiaji wake wataachwa kujikongoja na toleo hilo na kupata muda wa kufanya mabadiliko kuhamia toleo jipya mpaka 2028.

Watakaoshindwa kufanya mabadiliko hayo ambayo yatakuwa ya gharama basi itapelekea mamia ya mamilioni ya kompyuta duniani kutokuwa na kazi tena.

Pamoja na kuwa uamuzi huo utaongeza tatizo na kuongezeka kwa plastic duniani ambazo haziozi lakini hilo litakuwa lazima kwa kampuni hiyo ya microsoft ili kufikia malengo yake ya ifikapo mwaka 2030 kuwa carbon negative.

Haya wataalamu wa mambo ya electronic na mawasiliano ya kimtandao tupeni elimu zaidi kutuepusha na hasara.

Yahoo news​

Wewe ni mgeni?
 
Hizo biti ni kwa wale wanaotumia PC zao kwenye maofisi labda na shughuli rasmi...

Lakini kuna wadau wanaohitaji environment tu ya windows kupiga mzigo, hawana hata habari na hizo new updates...

No even maofisi mengi sikuizi ya latest pc. Most of computer utazonunua kipindi hiki zina support windows 11
 
Official sawa ila ukiweka iso machine yoyote inaingia 11, Nina Vimeo kibao hapa vingine vya zaidi ya miaka 10 iliopita vina win 11
Kuna Acer TravelMate5730 hapa ya jamaa, mzigo wa 2009 una run windows 11 kama kawaida na uko chap.. Windows 11 kuna namna ukicheza nayo inainstall kwenye mashine nyingi tu kwenye bios za kizamani.
 
Back
Top Bottom